RC Mghwira atembelea familia ya Ndesamburo na kutoa pole

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,404
24,988
Mkuu mpya wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Moshimjini,marehemu Philemon Ndesamburo.

Picha zote na Happiness Tesha. Kwa ufupi*.

Mghwira ametoa rambirambi kwa familia ya Ndesamburo, aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini kwa awamu tatu mfululizo.*.

Mghwira aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli amewasili katika eneo lake jipya la kazi ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuapishwa na Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutia saini kitabu cha wageni katika ofisi yake mpya leo Alhamisi, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira, ameenda kuhanimsiba wa aliyekuwa mwenyekitiwa Chadema, mkoa huo, marehemu Philemon Ndesamburo.

Mghwira ametoa rambirambi kwa familia ya Ndesamburo, aliyewahi kuwa mbunge wa Moshi Mjini kwa awamu tatu mfululizo.

Mghwira aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli amewasili katika eneo lake jipyala kazi ikiwa ni siku mbili tu baada ya kuapishwa na Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mghwira anaanza kazi wakati Chama cha ACT-Wazalendo kikimuondoa katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa chama hicho kutokana na matakwa ya katiba ya chama hicho.

Hata hivyo, Mgwhira ataendeleakuwa mwanachama wa ACT-Wazalendo.

Chanzo : Mwananchi

c1011dfe257dc4c48c5822128ce69c31.jpg

464425fa8faf1e93f059be18fcc7cc66.jpg
91a2dc2d9ebcecd16379a5e3b0d39ebf.jpg
 
Jambo zuri kuwapa pole familia hiyo kwani mzee Ndesa alikuwa mshauri mzuri kwa wakuu wa mikoa waliopita hapo wengi walimkimbilia kwa ushauri kwa siri walipokuwa na shida
 
Bila shaka yo yote hivi sasa amejivua kabisa ACT Wazalendo!!
 
Imekaa vizuri sana. You can see the difference; wale ambao damu zao ni CCM per-se yaani mahafidhina na huyu ambaye ni "moderate". Utangamano wa kitaifa huanza na mambo kama hayo sio kila mara kutumiana sijui polisi, ubabe, kejeli, dharau, kunyimana haki za kutumia public resources, n.k.
 
Back
Top Bottom