Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,562
- 1,180
MALIMA AWATAKA WAKADIRIAJI MAJENZI KUJITANGAZA
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ameitaka Taasisi ya Wakadiriaji Majenzi Tanzania (TIQS) kutokaa kimya bali ijitangaze Serikalini na katika jamii ili wafahamike kazi wanazofanya na umuhimu wao katika miradi ya ujenzi na teknolojia.
Malima ametoa agizo hilo mkoani Morogoro wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 30 wa mwaka wa Taasisi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa kuwatumia wataalamu wa Taasisi hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali pamoja na Jamii kwa ujumla.
"Mimi ni mdau na nina miradi mingi sana inayoendelea Wilayani na katika Halmashauri, Ninawatambua na nawahitaji. Pia natamani sana katika kila mradi awepo mkadiriaji majenzi”, amesema Malima.
Aidha, Malima ameitaka Taasisi ya Wakadiriaji Majenzi (TIQS) kuhakikisha wanasimamia maadili ya taaluma yao pindi wanapotekeleza majukumu yao.
Amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imefanya mabadiliko ya Sheria ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wataalam wa fani hizo katika usimamizi wa miradi ya ujenzi.
Malima ametoa rai kwa wadau wa Sekta ya Ujenzi kutumia fursa ya mikutano kujitangaza na kujifunza mambo mapya zikiwemo teknolojia mbalimbali zitakazoongeza tija na ufanisi katika Sekta na kuleta maendeleo ya ujenzi wa miundombinu bora.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Umeme na Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Qs. Mwanahamisi Kitogo amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imeandaa mkakati wa kuwawezesha watalaam wazawa katika kushiriki kazi za utekelezaji wa miradi ya ujenzi ili kuhakikisha fursa zinazopatikana zinawanufaisha wataalam wazawa.
Kwa upande wake, Rais wa TIQS, Bernard Ndakidemi ameeleza kuwa kwa sasa Taasisi hiyo ina wanachama waliosajiliwa 1,215 na wanaolipa ada kila mwaka na ilianzishwa mwaka 1987.
Mkutano Mkuu wa 30 wa mwaka wa Taasisi ya TIQS umebebwa na kauli mbiu ya 'Kuongezeka kwa gharama za ujenzi katika miradi ya umma, wakati wa hatua ni sasa'.
Mwisho
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-10-11 at 06.32.22.jpeg60.9 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-10-11 at 06.32.23.jpeg65.6 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-10-11 at 06.32.24.jpeg65.9 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-10-11 at 06.32.25.jpeg64.8 KB · Views: 3
-
WhatsApp Image 2024-10-11 at 06.32.26.jpeg59.1 KB · Views: 4
-
WhatsApp Image 2024-10-11 at 06.32.27.jpeg63.2 KB · Views: 3