RC Makonda agoma kuzungumzia kughushi vyeti

Hii ndio TZ litaibuka jipya muda si mrefu na hili litasaulika kimya kimya.


[HASHTAG]#Team[/HASHTAG] wasaulifuu#
 
Ukiona mtu anakwepa kujibu kashfa kisa zimeanzia wapi sisi ni watu wazima tunakaa kimya...lakini ningezushiwa mimi km taarifa imeanzia mitandaoni navirusha mitandaoni vyeti vyangu au km waandishi wa habari nawaita natoa kuanzia cheti cha kuzaliwa,kipaimara,std-7,4m4,4m6 hadi pale waliposema no education ahead....lakini tuwape mda necta wanamajibu sahihi
 
Mmmh haw jamaa bhana wanaomba chwti hku wakijishtukia, rc akionyesha tayari walishajiaminisha cheti kinapikwa, hamkosagi kujiwekea kinga, kama mnajua kitapikwa sasa bado mnakiomba cheti ili mfanye nn ? Ni kazi bure na ni kazi kweli kweli kwa opposition

Haya bhana ss tunawasubiri 2020 tutwange tena na nina imani mtasema ngoja sasa 2025 tunachukua nchi,mtabaki kama arsenal kombe hadi waliibe
 
Licha ya kuandamwa na tuhuma za kughushi vyeti, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hawezi kuzungumzia suala hilo kwani majibu yake yapo mtandaoni sakata lilipoanzia.

Makonda amesema hayo leo (Ijumaa) alipoulizwa swali na wanahabari kuhusu uhakika wa taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa alinunua vyeti na kutumia jina lisilo lake.

"Maswali ya mitandaoni yanaishia mitandaoni siko hapa kupoteza focus (mwelekeo).Ukiona maneno mengi yanaibuka kwenye ishu ya dawa za kulevya ndiyo ujue vita imefika penyewe,"amesema Makonda.





Chanzo: Mwananchi
Safi sana Makonda Go
 
Anamsubiri Lissu kwenye kesi ya Katiba ya Mbowe, atayasema yote kwa amri ya mahakama.
Swali: Shaidi twambie elimu yako
Jibu: (Kwa kusita kidogo) Nina elimu ya chuo kikuu.
Swali: Unaweza kuiambia mahakama elimu yako kwa kukutajia shule ulizosoma
Jibu: (Kwa kufuta jasho anasita kutoa jibu)
Jaji: Ebu jibu swali uliloulizwa shaidi
Jibu: anatoa majibu kwa kujikanyaga
Swali: Shaidi ebu twambie kama unamjua mtu anaitwa Daudi Albert Bashite
Jibu: Simjui
Swali: Unaweza kutambua picha ya mtu huyu (anatoa kitambulisho chenye picha ya Makonda)
Jibu: Picha ni yangu ila kitambulisho sikijui
Swali: (Akielekea meza ya majaji) naomba kitambulisho iki kichukuliwe kama kidhibiti namba..
Swali: Unamtambua mtu anayejulikana (akimtaja mtu mwenye vyeti vyake)
Maswali yakiendelea: hali ya shaidi inabadilika anapata pressure na mahakama inahairishwa kwa muda
Nimekupenda buuure!nimechekaa
 
hata akivitoa mtasema ni vya kugushi.. kwani mna maana nyie. muacheni aendelee na kazi zake na nyie endeleeni na ya kwenu. hata hivo cheti hicho mnachotaka haikuwa criteria ya kuchaguliwa kwake.
waliwai kudai hati ya muungano ilipoletwa waliikataa katakata . wacha dawa iwaingie hakuna namna
 
Back
Top Bottom