ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,368
- 50,737
Aliyetuhumiwa Kumpatia Kiwanja ‘Feki’ RC Makonda, Aeleza Uhalali wa Umiliki wa Eneo Hilo
Baada ya waziri wa ardhi William Lukuvi kudai eneo la ekari 1500 alilopewa RC Paul Makonda kwaajili ya ujenzi viwanda vidogo vidogo kuwa ni eneo la serikali, mmiliki wa eneo hilo mfanyabiashara Mohamed Iqbal ametoa vielelezo vya umiliki wa eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Ijumaa hii Kamugisha Katabara ambaye ni mwakilishi wa Mohamed Iqbar katika ukumbi ya jengo la Red Cross jijini Dar es salaam amesema:
Kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi mnamo tarehe 27, Februari mwaka huu ya kuwa ndugu Mohamed Iqbar alisema kuwa lile sio eneo lake ni mali ya serikali amemdanganya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kumpatia eneo la ardhi lililopo Lingato Kisarawe 11, Kigamboni Dar ambalo si mali yake bali ni mali ya serikali, kufuatia kushindwa kesi kati yake na wananchi.”
Aliongeza, “Kufuatia tuhuma hizo imewasikitisha wataalamu wanaotambua jambo hilo kumuondolea heshima ndugu Iqbal ndipo walipoita waandishi hao kufikisha ukweli kwa umma juu ya mambo haya matatu ikiwa ni pamoja na umiliki wa eneo, utaratibu wa kukabidhi eneo kwa mkuu wa mkoa huyo, na hukumu ya kesi aliyoizungumzia mhe Waziri wa ardhi. Ndugu Iqbal ni mmiliki halali wa eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 3500 lililopo eneo tajwa hapo juu. Eneo hilo alinunua tangu mwaka 2005 kutoka kwa wananchi wa eneo hilo ambao waliuza kwa hiari yao wenyewe bila kushurutishwa na kwa kufuata taratibu zote za kisheria za ununuzi wa ardhi.”
Aidha Katabara alitoa uhalali wa umiliki wa eneo hilo huku akisema kuwa endapo zitahitajika zitawekwa bayana nakala pamoja na picha.
“Ushahidi wa nakala za barua za mawasiliano kati ya ofisi ya serikali ya mtaa wa Lingato,muhtasari ya vikao vya maamuzi ya serikali za mitaa na mikutano na wananchi waliomiliki maeneo hayo ipo. Aidha nakala za risiti zipo na malipo ya ushuru wa serikali kama sheria inavyotaka na mikataba ya mauziano ya maeneo ya ardhi na picha za wamiliki wa maeneo wakipokea fedha za malipo na mauziano ya ardhi zipo na zitawekwa bayana pale zitakapohitajika.”
==============
Ndugu wana habari,
Nimewaiteni hapa kufuatia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi, mnamo tarehe 27, Februari 2017 ya kuwa Ndugu Mohamed Ikbal amemdanganya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda kwa kumpatia eneo la ardhi lililopo Lingato Kisarawe II, Kigamboni-Dar es salaam, ambalo si mali yake bali ni la serikali, kufuatia kushindwa kesi kati yake na wananchi.
Kufuatia taarifa hiyo ambayo imewasikitisha watanzania na hasa wataalamu mbalimbali wanaofahamu ukweli wa jambo hili; na kumuondolea heshima ndugu Ikbal mbele ya macho ya watanzania. Hivyo tumewaita hapa ili mtusaidie kufikisha ukweli kwa umma wa watanzania juu ya mambo makuu matatu;-
1. Uhalali wa umiliki wa eneo
2. Utaratibu wa kukabidhi eneo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es salaam
3. Hukumu ya Kesi aliyoizungumzia Mh. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
1. Uhalali wa Umiliki wa Eneo
Ndugu wanahabari tungependa umma wa watanzania ufahamu kwamba ndugu Mohamed Ikbal ni mmiliki halali wa eneo la ardhi lenye ukubwa wa ekari 3500, lililopo lingato, Kisarawe II, Kigamboni, jijini Dar es salaam. Eneo hili alilinunua tangu mwanzoni mwa mwaka 2005 kutoka kwa wananchi wa eneo hilo; ambao waliuza kwa hiari yao wenyewe bila kushurutishwa na kwa kufuata taratibu zote za kisheria za ununuzi na umiliki wa ardhi.
Ushahidi wa nakala za barua za mawasiliano kati ya ofisi ya serikali ya mtaa wa Lingato, mihutasari ya vikao vya maamuzi vya serikali ya mtaa na mikutano ya wananchi waliokuwa wamiliki wa maeneo hayo ipo. Aidha, nakala za risiti za malipo ya ushuru wa serikali kama sheria inavyotaka, mikataba ya mauziano ya maeneo ya ardhi sambamba na picha za wamiliki wa maeneo wakipokea fedha za malipo ya mauziano ya ardhi zipo na zitawekwa bayana pale itapohitajika.
Kuzuka kwa mgogoro
i. Miaka michache baada ya mauziano ya ardhi, baadhi ya wauzaji walianza kuingiwa na tamaa kutokana na kupanda kwa thamani ya ardhi. Kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali ya mtaa wasio waaminifu walianza kuvamia eneo la ndugu Mohamed Ikbal na baadae kuwasilisha malalamiko kwa Kamishna wa ardhi ya kwamba wananyanyaswa katika ardhi yao na kwamba hawakuuza maeneo yao kwa hiari yao.
Ofisi ya Kamishna wa Ardhi katika barua yake ya tarehe 31/10/2006 yenye Kumb. na. LD/164035/CB iliuomba uongozi wa Manispaa ya Temeke kutoa taarifa juu ya malalamiko ya kundi hilo.
Katika barua yenye Kumb. Na: TMC/MD/M.13/83/79 ya tarehe 18-12-2006 Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke alimjulisha Kamishna wa Ardhi kuwa mgorogoro huo ulishughulikiwa na Kamati ya Rais ya Kushughulikia Migogoro, chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke.
Mwenyekiti wa kamati hiyo (Mstahiki Meya),Diwani wa Kata ya Kisarawe II na wananchi katika eneo lenye mgogoro walifanya mkutano na ilibainika kuwa, wananchi hao waliuza maeneo yao kwa ridhaa yao wenyewe bila kushurutishwa na walilipwa kama ilivyo katika makubaliano kati ya muuzaji na mnunuzi.
Kufuatia majibu hayo Kamishna wa ardhi alilitaarifu kundi hilo la walalamikaji kupitia barua yenye Kumb. Na: LD/164035/VOL.V/39 ya tarehe 26/02/2007.
(ii) Licha ya majibu ya Kamishna wa Ardhi, bado mgogoro uliendelea na kupelekea Mkuu wa Wilaya ya Temeke kufanya mkutano kati ya wananchi wa eneo hilo na ndugu Mohamed Ikbal tarehe 08/10/2007. Mkutano huo uliofanyika katika eneo la Asha Ngoma, Kisarawe II, na baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili alihitimisha mkutano huo kwa kuwataka wale wote ambao wanahisi kudhulumiwa kupeleka malalamiko yao Mahakamani.
(iii) Kufuatia kuendelea kwa uvamizi katika eneo hilo, Ndugu Ikbal aliwasilisha malalamiko yake katika Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Temeke; Ambaye alimuandikia barua Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kipolisi ya Kigamboni, Dar es salaam, kupitia barua yenye Kumb. Na: E.40/9 VOL.I/64 ya tarehe 26, Februari 2008, kumjulisha juu ya malalamiko hayo na kumuomba kuchukua hatua:
Ninanukuu:-
“Nakuletea malalamiko haya na kukushauri raia huyu anayo haki ya kusikilizwa na kusaidiwa na serikali inapodhihirika kuwa anaonewa. Nakuomba umsaidie kuwaondoa hao wavamizi ili nae apate nafasi ya kuyaendeleza maeneo yake”
(iv) Kundi la pili la wavamizi liliwasilisha malalaliko yao kwenye ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia barua yao ya tarehe 04, Machi, 2008.
Baada ya kufuatilia kwa kina ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi iliwajibu kwa barua ya tarehe 09, Mei, 2008 yenye Kumb. Na:EA 71/176/01.B/49, ikibainisha kwamba wananchi hao waliuza maeneo yao kwa hiari yao. Sehemu ya barua hiyo ilisema, ninanukuu:-
“Kufuatia ukweli wote huu uliobainishwa Mhe. Waziri ameona hakuna mgogoro kwa kuwa watu waliuza ardhi yao kwa maelewano, tena nje ya ofisi ya serikali ya mtaa. Hivyo suala hili limefungwa na yeyote ambaye haridhiki na uamuzi huu apeleke suala hili Mahakamani”
Barua ya Ofisi ya Waziri ilifuatiwa na barua ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa Afisa Mtendaji Kata ya Kisarawe II ya tarehe 20 Mei, 2008, yenye kichwa cha barua “MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU MGOGORO WA ARDHI YA BWANA MOHAMED IKBAL NA BWANA MADUHU PIUS NA WENZAKE”.
Nanukuu sehemu ya barua hiyo;-
“Kwa nakala ya barua hii, namshauri bwana Mohamed Ikbar kutoa taarifa kwako na au kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kigamboni, pale anapotokea yeyote kuvamia, kuuza au kuishi katika maeneo yake bila kibali chake. Inapotokea hivyo tafadhali asaidiwe”
(V) Vilevile Wizara ya Ardhi na ofisi ya Mkuu wa Wilaya imekuwa ikitoa matamko mbalimali kuwa Ndugu Ikbal ni mmiliki halali wa eneo la ukubwa ekari 3500 lililopo Lingato. Matamko haya yameripotiwa na Magazeti mbalimbali na Wizara hii hajawahi kukanusha habari hizi. Kwa mfano:
Tanzania Daima, toleo la Decemba 30/2015 uk.18 iliripotiwa kuwa Diwani wa kata ya Kisarawe П Issa Hemedi alisema kuwa mmiliki halali wa eneo hilo ni Ikbali ambaye alianza kununua eeno hilo tangu mwaka 2004.
Jambo leo toleo la tarehe 20/1/2016 uk 4 Sifuani Athumani alisema “wakati mwekezaji ananunua maeneo haya nilikuwepo nikishuhudia watu wakimuuzia maeneo Ikbar”
Habari leo Toleo la tarehe 27/1/2016 Kamishna wa Ardhi alinukuliwa akisema “ardhi hii aliuziwa Mohamaed Ikbal……….”
VI: Aidha katika kikao kingine kilichokaa, mnamo tarehe 18/10/2012 Kilichohudhuriwa na mwenyeketi wa serikali ya mtaa huo ndugu Cosmas Kalimanzila, Diwani wa kata hiyo, wajumbe na wawakilishi wa ndugu Ikbal, zoezi la uhakiki wa mipaka isiyokuwa na migogoro ilikuwa ndio agenda kuu ya kikao hicho. Mwisho wa kikao hicho wote walioshiriki walikubaliana kuwa mipaka iliyooneshwa na Mwenyekiti; Ndugu Kalimanzila ilikuwa halali na jumla ya eneo hilo ni hekta 1304 (sawa na ekari 3500).
Kuthibitisha haya yaliyosemwa hapa, kuna ushahidi wa ramani iliyoandaliwa baada kikao hicho. Ndani ya ramani hii, kuna saini za wote walioshiriki na maelezo ya Mwenyekiti wa serikali ya mtaa vyote vikishuhudia umiliki halali wa Ndg. Ikbal. Nakala ya ramani hii itatolewa kwa yeyote atakayependa kujiridhisha.
Ndugu wana habari,
Kwa maelezo haya ya kina kuhusu utaratibu wa ununuzi wa ardhi, maamuzi ya vikao na mikutano kati ya wauzaji, mnunuzi na viongozi; barua kutoka ofisi ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Ofisi ya Kamishna wa Ardhi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na nukuu mbalimbali kutoka katika vyombo vya habari, inadhihirisha pasi na kuacha shaka kwamba NDUGU MOHAMED IKBAL NI MMILIKI HALALI WA ENEO LA EKARI 3500, LILILOPO KISARAWE II DAR ES SALAAM NA KWAMBA HAKUMDANGANYA, WALA KUMTAPELI YEYOTE KAMA ILIVYORIPOTIWA NA MH. WAZIRI.
2. Utaratibu wa kukabidhi eneo kwa serikali
Ndugu wana habari,
Katika jitihada za kuunga mkono serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli, za kuinua uchumi wa Tanzania kupitia viwanda ndugu Ikbal aliamua kutenga eneo kwa ajili ya serikali bila kushurutishwa na mtu yeyote. Aliwasilisha taarifa ya azma yake ya kukabidhi eneo kwa serikali kupitia Ofisi ya Mku wa Mkoa wa Dar es salaam
Ikumbukwe kwamba kabla ya kufikia maamuzi ya kuja kulitembelea eneo hilo na kuitangaza Nia hiyo, mbele ya waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa aliomba uthibitisho wa uhalali wa umiliki wake. Wataalamu wa ardhi kutoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi kanda ya Dar es salaam, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Maafisa wa Ardhi kutoka Manispaa ya Kigamboni walitembelea kwenye eneo ili kujiridhisha.
NB: Mpaka hatua ya mwisho ya kulitangaza eneo hilo kwenye vyombo vya habari, HAKUKUWA NA PINGAMIZI LOLOTE KUHUSU UHALALI WA BWANA MOHAMEDI IKBAL KUMILIKI ENEO HILO.
Ndugu Wanahabari;
3. Hukumu ya Mahakama ilizungumziwa na Mh. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Kuhusu madai ya Waziri kuwa ndugu Ikbal alifungua kesi kuhusu umiliki wa Ardhi na akashindwa, siyo madai ya kweli, na sidhani kama alishauriana na wanasheria wa Wizara kabla ya kuja kuzungumza jambo hilo. Hakuna Kesi kama hii ambayo ndugu Ikbal alifungua kama alivyodai Mh:Waziri. Nakala ya kufuta shauri ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya ya Temeke iliyoonyeshwa na Mhe: Waziri sio hukumu kwa mujibu wa sheria . Hii ni Miscellaneous Application number 147 ya 2015 yaani ni maombi madogo yaliyotokana na kesi ya msingi namba 298/2015.
Kesi hii Na. 298 ya 2015 ilifunguliwa na Lingato Village council dhidi ya Mohamedi Ikbal kuwa Bwana Ikbal ameshindwa kujenga nyumba za gharama nafuu kwenye ekari 50 alizonunua na kwamba anachimba mchanga eneo hilo. Katika Shauri hilo, kijiji kilikuwa kinaomba Bwana Ikbal azuiwe kuchimba mchanga. Kesi No. 298 ya 2015 iliambatana na maombi ya zuio (injuction) ambayo yalikubaliana siku hiyo hiyo tarehe 4/11/2015. Ndugu Ikbal alifungua maombi madogo number 147/2015 dhidi ya kijiji tarehe 28/11/2015 akiomba yafuatayo:
1) Kwamba baraza limpe nakala ya Maombi namba 298/2015 na
2) Kuomba amri yake ya tarehe 4/11/2015 ya zuio iliyotolewa kwa kusikiliza upande mmoja tu na bila kumpa Ikbal haki ya kusikilizwa ifutwe na kesi ya msingi isikilizwe.
Tarehe 23/11/2015 , Mahakama iliondoa amri yake ya tarehe 4/11/2015 , na baadae kijiji kiliondoa kesi No.298/2015. Hivyo maombi No.147/2015 hayakuwa mbele ya mahakama na Mhe: mwenyekiti hakuwa na maombi yoyote mbele yake ya kufuta. Yaani Serikali ya kijiji ya Lingato kwa kuondoa kesi namba 298/2015 mahakamani, maombi namba 147/2015 hayakuwa na miguu tena ya kusimamia hivyo ndio sababu yakufutwa hiyo tarehe 13/1/2016.
Kwa hiyo sio kweli kwamba shauri hili lilihusu mgogoro wa Ardhi na kwamba ndugu Mohamed Ikbal alishindwa kesi hii.
Tunamsihi Mhe:Waziri atumie wanasheria wa Wizara afuatilie historia ya kesi hii na ajiridhishe na kauli yake aliyotoa kuwa Ndugu Ikbal alishindwa kesi mahakamani kwa kuwa hakuna hukumu ya namna hiyo na mahakama haijawai kurudisha eneo kwa Wananchi kama alivyosema waziri.
Mwisho
Ndugu wana habari,
Kwa kuzingatia maelezo ya kina yaliyotolewa, ni ukweli usiopingika kwamba, Mh. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amepotoshwa kwa kupewa nyaraka isiyo sahihi, na kwamba kupitia nyaraka hiyo ameudanganya umma, hivyo kuchochea upya mgogoro ambao wataalamu wake wanaendelea kuushughulikia. Jambo la Kusikitisha zaidi ni kuwa, wakati huu tunaendelea kuzungumza hapa; wale wananchi wachache wasio waaminifu wanaoendelea kuvamia eneo hili kwa kasi huku wakiwavuta wengine wengi wasioujua ukweli wa suala hili.
Vilevile mchakato wa kulipitia tena eneo hilo ili kukamilisha zoezi la kukabidhi eneo kwa serikali ya Mkoa wa Dar es salaam ili kuwasaidia vijana, uliokuwa unaendeshwa na kamati ya Wataalamu wa Ardhi kutoka Manispaa ya Kigamboni na Mmiliki wa eneo ndugu Ikbal, umesimama kutokana na kauli hiyo; hivyo kukwamisha jitihada za serikali ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli kupanua wigo wa ajira na kukuza uchumi kupitia viwanda.
Tunapenda ifahamike wazi kuwa, taarifa hii haijatolewa kwa nia ya kuleta malumbano katika vyombo vya habari, ila tumeona ni vyema ukweli wote usikilizwe na kila mtanzania ili kuondoa sintofahamu iliyojengeka.
Tunapenda kutoa rai na kuwaonya watu wote wanaendelea kufanya utapeli katika maeneo hayo, kuacha mara moja. Na kwa watanzania wenye nia ya kujipatia ardhi katika maeneo haya ya Lingato wawe makini na wafanye utafiti wa kutosha kupitia ofisi za serikali kujiridhisha kabla ya kutumia pesa zao.
Mungu Ibariki Tanzania. Ahsanteni
IMETOLEWA NA:
NDUGU MOHAMED IKBAL

TAARIFA YA NDUGU MOHAMEDI IKBAL KWA VYOMBO VYA HABARI, KUHUSU UFAFANUZI WA UMILIKI WA ENEO LA EKARI 3500 LILILOPO LINGATO, KISARAWE II, KIGAMBONI-DSM