RC Makame ashtukiza mpaka wa Tunduma 'Sijaridhika'

RC Makame ashtukiza mpaka wa Tunduma 'Sijaridhika'

ChekoFagia

Senior Member
Joined
Sep 20, 2025
Posts
115
Reaction score
339
Mkuu wa Mkoa wa Songwe ndugu Jabiri Makame, amefanya ziara ya kushtukiza katika Mpaka wa Tunduma kukagua utekelezaji wa Maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba kuhusu upanuzi wa barabara ya kuelekea Mpaka wa Tanzania na Zambia kwa njia nne ili kurahisisha malori kuvuka mpaka kwa haraka na kupunguza msongamano wa Malori Tunduma.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa kazi hiyo RC Makame alieleza kutoridhika na kasi ya utekelezaji wa Ujenzi wa Mradi huo ambapo mpaka sasa TANROADS wanaendelea na ujenzi wa barabara ya mchepuko na kwa upande wa TRA bado hawajabomoa ukuta kuruhusu upanuzi wa barabara hiyo kwa kigezo cha kusubiri Taasisi zingine zikiwemo TTCL, TANESCO na Mamlaka ya Maji kumaliza kazi yao.

Kufuatia hali hiyo, RC Makame aliagiza Taasisi hizo zote kufikia kesho wawe wamekamilisha kazi zao ya kuhamisha miundombinu, na mkandarasi kukamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuko na kuanza mara moja upanuzi wa barabara hiyo.

Pia Soma: Foleni ya Tunduma mpakani haitatuliwi, kuna Watu wana maslahi Binafsi, inatutesa wengi
 
Back
Top Bottom