RC Makalla na Bodaboda, Wakubaliana na Kuunda Kamati ya utaratibu wa vituo na uingiaji na utokaji Mjini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,986
RC MAKALLA NA BODABODA MAMBO SAFI.

- Wakubaliana na Kuunda Kamati ya utaratibu wa vituo na uingiaji na utokaji Mji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa Miezi mitatu kwa Shirikisho la Vyama vya waendesha Bodaboda Jijini humo kuweka Mpango kazi kuwapanga vizuri Bodaboda ikiwa ni pamoja na utaratibu rasmi wa kuingia mjini na kutoka ili kuondoa hali uholela wa kuingia mjini unayoendelea kwa Sasa.

RC Makalla ametoa maazimio hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya Viongozi wa Bodaboda, Jeshi la Polisi, LATRA, TARURA na TANROAD kilicholenga kujadili zuio la Bodaboda kuingia mjini lililokuwa limetolewa na Jeshi la Polisi.

Miongoni mwa maazimio yaliyotolewa na kikao hicho na yanapaswa kufanyiwa kazi na Kamati iliyoundwa ni pamoja na shughuli za Bodaboda kufanyika sambamba na kulinda taswira ya Jiji, Uwepo wa vituo rasmi vya Bodaboda vinavyotambulika, Uvaaji wa Sare, Kofia ngumu pamoja na Bodaboda kuwa sehemu ya kuwafichua wahalifu.

Aidha RC Makalla amesema baada ya kupatiwa Mapendekezo ya Kamati atahitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ili kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha suala la kuingia mjini linafanyika kwa kuzingatia taratibu.

Hata hivyo RC Makalla amesema Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inathamini kazi ya Bodaboda Kutokana na shughuli hiyo kutoa ajira kwa idadi kubwa ya Vijana.

Nao baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya waendesha Bodaboda akiwemo Said Kagomba ambae ndio Mwenyekiti wa Shirikisho ameishukuru Serikali kwa kukaa meza moja na Shirikisho Kuangalia namna Bora ya kushughulikia Jambo hilo na wameahidi kushirikiana na Serikali kuweka mazingira Bora ya biashara hiyo ili Bodaboda wa Dar es salaam wawe mfano mzuri wa kuigwa.
IMG-20211101-WA0008.jpg
IMG-20211101-WA0007.jpg
IMG-20211101-WA0006.jpg
IMG-20211101-WA0010.jpg
IMG-20211101-WA0009.jpg
 
Kulikuwa hakuna jibu jingine mara baada ya Kauli ya Shaka - Katibu Mwenezi CCM. Bila hivyo kazi ilikuwa hali ilikuwa imeshachafuka kati ya Chama na Serikali (Wenyewe kwa wenyewe).
 
Baada ya kuona amechemka kwenye issue ya Wamachinga sasa karukia kwa bodaboda.
 
Kulikuwa hakuna jibu jingine mara baada ya Kauli ya Shaka - Katibu Mwenezi CCM. Bila hivyo kazi ilikuwa hali ilikuwa imeshachafuka kati ya Chama na Serikali (Wenyewe kwa wenyewe).
Ndiyo maana hii nchi haiwezi kusonga mbale kwani siasa imeshika kila pahali.

Kwa wenzetu walio endelea wanaamini professionalism na hayo mambo ya siasa wanawachia wana siasa.
 
Makala ameshindwana na machinga analukia kwenye bodaboda.
Mh makala uliaidi Kama machinga wasipotoka utakuwa hufai na utawajibika vip utakuwa oficin mpka lini?
 
Nimetazama picha, sawa hapo naona makubaliano na bodaboda, mambo sawia sasa.
Lakini pi kuna haja sasa ya kutazama na magari binagsi yanayoingia mjini na yenyewe yatazamwa upya maana yanasababisha foleni isiyokuwa na maana na kupotezea wananchi weni muda barabarani, ni heri sasa magari yote binafsi yaishie nje ya mji, mjini sasa yaingie magari ya serikali na yale ya abiria, inatosha kabisa.
 
Makala ameshindwana na machinga analukia kwenye bodaboda.
Mh makala uliaidi Kama machinga wasipotoka utakuwa hufai na utawajibika vip utakuwa oficin mpka lini?
Hii nchi ingekuwa inafuata utawala wa sheria huyu mtu leo hii asingekuwa kwenye ofisi za serikali
 
RC MAKALLA NA BODABODA MAMBO SAFI.

- Wakubaliana na Kuunda Kamati ya utaratibu wa vituo na uingiaji na utokaji Mji.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa Miezi mitatu kwa Shirikisho la Vyama vya waendesha Bodaboda Jijini humo kuweka Mpango kazi kuwapanga vizuri Bodaboda ikiwa ni pamoja na utaratibu rasmi wa kuingia mjini na kutoka ili kuondoa hali uholela wa kuingia mjini unayoendelea kwa Sasa.

RC Makalla
ametoa maazimio hayo wakati wa kikao Cha pamoja baina ya Viongozi wa Bodaboda, Jeshi la Polisi, LATRA, TARURA na TANROAD kilicholenga kujadili zuio la Bodaboda kuingia mjini lililokuwa limetolewa na Jeshi la Polisi.

Miongoni mwa maazimio yaliyotolewa na kikao hicho na yanapaswa kufanyiwa kazi na Kamati iliyoundwa ni pamoja na shughuli za Bodaboda kufanyika sambamba na kulinda taswira ya Jiji, Uwepo wa vituo rasmi vya Bodaboda vinavyotambulika, Uvaaji wa Sare, Kofia ngumu pamoja na Bodaboda kuwa sehemu ya kuwafichua wahalifu.

Aidha RC Makalla amesema baada ya kupatiwa Mapendekezo ya Kamati atahitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ili kuweka mazingira wezeshi ya kuhakikisha suala la kuingia mjini linafanyika kwa kuzingatia taratibu.

Hata hivyo RC Makalla amesema Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inathamini kazi ya Bodaboda Kutokana na shughuli hiyo kutoa ajira kwa idadi kubwa ya Vijana.

Nao baadhi ya Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya waendesha Bodaboda akiwemo Said Kagomba ambae ndio Mwenyekiti wa Shirikisho ameishukuru Serikali kwa kukaa meza moja na Shirikisho Kuangalia namna Bora ya kushughulikia Jambo hilo na wameahidi kushirikiana na Serikali kuweka mazingira Bora ya biashara hiyo ili Bodaboda wa Dar es salaam wawe mfano mzuri wa kuigwa.
View attachment 1994728View attachment 1994729View attachment 1994730View attachment 1994731View attachment 1994732
😍
 
Back
Top Bottom