RC Makalla amtaka Dkt. Bashiru kukaa kimya

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally akiendekea kuandamwa na kauli yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amejitosa akimtaka kiongozi huyo kukaa kimya kama hataki kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo Watanzania.

Kauli ya Bashiru inayoonekana kuzua utata ndani ya chama hicho ilitolewa siku za hivi karibuni wakati akihutubia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (Mviwata) uliofanyika mkoani Morogoro, alipowataka kuacha kusifia kila jambo huku wakijua wanachangamoto zinazowakabili.

Makalla akizungumza leo Ijumaa Novemba 25, 2022 wakati anapongeza juhudi za Rais Samia katoa fedha Kwa ajili ya miradi ya maji, baada ya kiongozi huyo kutembelea chanzo cha Maji Ruvu Juu.

"Sisi bado tutaendelea kushukuru jitihada za Rais Samia kama ilivyo utamaduni wetu lakini hizo kelekele hizo zakina Dk Bashiru Ally mi nasema ni kilanga Sisi tunasema tuko saiti akate Simu, tupo saiti tutaendelea kushukuru kwakuwa ni utamaduni wetu, "Na tunajua mradi mkubwa wa kidunda ambao ni tumaini letu unakuja tutaendelea kushuru Juhudi za Rais kuwaletea watanzania maendeleo, kama yeye ananyongo yake ya chuki aache akale ndimu ili kuondoa radha ya nyongo lakini akumbuke sisi tuko saiti tunashukuru ndiyo maana kuna maneno hata ya kiingereza thank you!," amesema

Amesema Watanzania bado wanaendelea kumshukuru Rais kwa Juhudi anazofanya na watu wenye kelele kama Dk Bashiru ni bora wakae kimya.
 
Kazi kweli kweli ingekuwa wanapaza sauti kwa watu wote wanaotafuna pesa serikali basi ingekuwa historia suala la wezi ila watu wanapiga hela wapo kimya wanakuja kuhangaika na bashiru
 
Katiba mpya katiba mpya ndio italeta akili mwa Watanzania. Makala wa Twanga Pepeta
 
Wakati aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally akiendekea kuandamwa na kauli yake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC)...
Kwani kuna Cheo kingine zaidi ya kuwa RC alivyo sasa Amos Makalla anakitaka kutokana na Kujipendekeza Kwake huku Kunakoboa kwa Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan?
 
Back
Top Bottom