Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,084
- 1,077
Maji ya mto weruweru yakiporomoka kutoka juu ya mlima Kilimanjaro, shamba la Mbowe liko mbali na huu mto.
Mfereji wa maji unaoitwa mfereji wa mzungu zamani ulitumiwa na wakulima wa kahawa ya Lambo estates kabila ya mashamba hayo kutaifishwa na serikali, unapata maji kutoka mto weruweru ambao wakulima wa kahawa, migomba, mahindi, maharagwe, viazi, mbogamboga ndio hutumia maji hayo kinyweshea mashamba yao.
Mkuu wa wilaya ya Hai anataka Mbowe asilime mita 60 kutoka kwenye mfereji huu na asitumie pump kujaza tank za maji na kutumia mfumo wa kumwagilia wa drip irrigation.