tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mussa Kilakala, ametoa wito kwa wananchi kuacha mara moja kufanya shughuli za kibinadamu kama vile uchenjuaji wa madini na kilimo karibu na vyanzo vya maji, ili kuepusha madhara ya mafuriko yanayolikumba eneo hilo mara kwa mara.
Akizungumza Oktoba 15, 2025 wakati wa zoezi la kufukua Mto Morogoro uliohama mkondo wake na kuharibu makazi ya wananchi wa Mafisa kwa Mambi, Kilakala amesema kuwa shughuli hizo ndizo chanzo kikuu cha mabadiliko ya mkondo wa mito huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kuwa mlinzi wa vyanzo vya maji ili kulinda mazingira na usalama wa jamii.
Soma pia: Kero ya Maji Lukobe - Morogoro
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmassy, amebainisha kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 300 kwa ajili ya kununua mtambo wa kusafishia mito, hatua itakayosaidia kupunguza madhara ya mafuriko kwa wananchi.
Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa kabla ya hatua hizi kuchukuliwa, watoto walikuwa waathirika wakuu kwani walikosa masomo kutokana na mafuriko, huku wakikosa pia fursa za kiuchumi kwa kushindwa kufanya shughuli zao za kila siku.