RC KAGERA: Tumepokea shilingi bilioni 185 kwaajili ya maji huenda tatizo la maji mkoani Kagera likabaki kuwa historia asante Rais Samia

RC KAGERA: Tumepokea shilingi bilioni 185 kwaajili ya maji huenda tatizo la maji mkoani Kagera likabaki kuwa historia asante Rais Samia

Bibianna

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2025
Posts
400
Reaction score
135

1754299924374.png

==​

Akiongea na wanahabari, Katika Sekta ya Huduma ya Maji Mijini na Vijijini, jumla ya Tshs bilioni 184.8 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, ambapo hali ya upatikanaji imeongezeka kutoka asilimia 85 hadi asilimia 93 mijini na kutoka asilimia 76 hadi asilimia 83 vijijini.

Jumla ya miradi 41 ya maji imetekelezwa, ikijumuisha miradi 23 vijijini na 18 mijini, yenye thamani ya Tshs bilioni 164.7. Miongoni mwa miradi mikubwa iliyotekelezwa ni pamoja na upanuzi wa mradi wa maji Bukoba Mjini TZS3.1bn na mradi wa maji Kyaka–Bunazi wilayani Missenyi TZS15.71bil, ambayo yote imekamilika. Miradi mingine ni ule wa Miji ya Kayanga–Omurushaka (Karagwe) wenye thamani ya TZS64.2bn na umefikia asilimia 64 ya utekelezaji, pamoja na mradi wa maji wa Kemondo (Bukoba Vijijini) ambao umetumia TZS4.57bn na umekamilika kwa asilimia 100 kwa mujibu wa mkuu wa Mkoa Jumla ya TZS 184.8bn zimetolewa kwa ajili ya miradi ya maji mkoani Kagera chini ya Rais Samia.


Eneo2020 (%)2025 (%)Ongezeko
Mijini85%93%+8%
Vijijini76%83%+7%

Utekelezaji wa Miradi

  • Jumla ya miradi minne (41) imetekelezwa:
    • Mijini: 18 miradi
    • Vijijini: 23 miradi
    • Thamani ya jumla: Tshs Bilioni 164.7

Baadhi ya Miradi Mikubwa ya Maji na halzi zao,


MradiMahaliThamani (Tshs Bil.)Utekelezaji
Upanuzi wa mradi wa maji Bukoba MjiniBukoba Mjini3.1100
Mradi wa maji Kyaka – BunaziMissenyi15.71100
Mradi wa maji wa Miji ya Kayanga – OmurushakaKaragwe64.264%
Mradi wa maji wa KemondoBukoba Vijijini4.57100
 
Kweli kujipendekeza kunahitaji mtu kujitoa ufahamu. Hela zimetokana na kodi za wananchi, lakini sifa anapewa Samia!
Halafu huyu Hajat RC pamoja na kujipendekeza kwake katika ujumbe wake huo, anashindwa kujua kuwa Tatizo la Maji Mkoano Kagera pamoja na kuwa na vyanzo vingi vikubwa tu, hakuna Awamu ya uongozi ambayo imeweza kulipatia ufumbuzi, tangia awamu ya I, leo hii watu wa Nzega, Tabora , Igunga wanapatiwa maji toka Ziwa Victoria, sisi tulioko Kiilomtre zero tunaishia bado kutumia maji ya kutokwa kwenye madinbwi, na kununua dumu la litre 20 kwa Tzsh 500 hadi 1000/=. Ni Aibu kwa viongozi wetu hasa wabunge, akina Bashungwa and colleagues. It is a shame. I dont buy that this Government will get it solved once and for all, 60 Years after independence bado tunalalamikia upatikanaji Maji kwenye Mamlaka ya Miji na Halmashauri zetu, achilia mbali huko vijijini Hapa Kagera. Prof Tibaijuka mama wa visenti vya mboga mboga, na Mh Lucy Msafiri aliwahi kuliongela Bungeni kuwa wanawake wa Kagera hatuna Maji, Mh Ndugai ( RIP)akadhihaki kwamba hebu rudia hapo na wabunge wakasihia kuleta utani kwenye jambo serious kama hili. Ni kweli wanawake wa Kagera hawana maji, not a joke, wanapata shida sana majumbani.
 
nani ajipendekeza sasa hapo?
Unauliza swali na jibu unalo! RC Kagera ndiye anaye jipendekeza. Hizo hela zinatokana na kodi za wananchi. Na serikali ndiyo inayo tekeleza hiyo miradi. Siyo hela za Samia.
 
ilikuwa ila kwa sasa hakuna hiyo shida tena
Wewe unayesema ilikuwa unaishi Kagera ya wapi, hakuna HALMASHAURI YA MJI wala Mamlaka za miji midogo ukiacha huko vijini, ambako kuna uhakika wa supply ya maji ya uhakika, Mwaka 2005 wakati Mh JK anakuja Kagera kuomba Kura aliahidi kwamba atalimaliza tatizo hili wakati wa kampeni zake, ila miaka 10 ilimalizika na akaogopa hata kuja kuaga maana alijua ataulizwa, the same situation hadi leo.
 
Back
Top Bottom