RC Happi: Serikali haijarejesha ada kwa Shule zake, wapuuzeni wazushi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Mkuu wa mkoa wa Mara Salum Happi amesema serikali haijarejesha Ada katika shule zake.

Happi amewataka wananchi kupuuza uzushi huo.
===

Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Ally Hapi amewataka wananchi kupuuza taarifa za baadhi ya watu wanaosambaza kuwa serikali imerejesha ada mashuleni jambo ambalo niuongo na wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria wanaosambaza uzushi huo.

Hapi ametoa kauli hiyo wakati akikabidhiwa madarasa 113 Wilaya ya Rorya yanayotokana na fedha za maendeleo na UVIKO-19 ambapo wilaya ya Rorya ilipokea bilioni 2.3.

Source: ITV habari
 
Unaweza shangaa akaitwa nanisensi!.. hivi hawajui kwa huyu Bibi wanatakiwa wakae kimya wakiongea tu haswa kwenye mambo kama haya ye ndo anakuja na yake!,yani kitu kinapitishwa Kama vile anamuambia huyo kiongozi aliekataa kumbe ni letu sote.😂
 
Ila mwana amekuwa kimya kweli mara hii. Yale majigambo yake kuongea kwa kujifanya Nyerere na kukunja kimdomo chake ka chuchunge kimya kabisa!

Najua akilala akiamka akila anawaza siku isiyo na jina tu mama atakapomuelekeza Kibla ....................
 
Mtukana wastaafu huyu, hadi aibu,, unamtukana mtu mzima sawa na baba yako kisa ukuu wa mkoa, ile kauli ilikera sana,

Sijui hicho kiburi alikitoa wapi?

Nafikiri wastaafu sasa hv wanamchora tu, wakisema sema suuu, atakuwa nje ya kambi kitamboo
 
“Kuna watu wanapita pita huko wanasema kuwa Ada imerudi, eti ile Elimu bila malipo imefutwa, ni waongo kwa sababu zao wanazojua wenyewe, Elimu bila Ada Elimu bila malipo inaendelea hakuna Mtoto atakayedaiwa ada, pelekeni Watoto wakasome” Ally Hapi Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi amewataka Wananchi kupuuza taarifa za baadhi ya watu wanaosambaza kuwa Serikali imerejesha Ada Mashuleni jambo ambalo ni uongo na wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria wote wanaosambaza uzushi huo.
 
Hii ndiyo shida ya viongozi wengi. Ukisikia jambo, usikanushe kuwa halipo. Fanya utafiti kwanza ujiridhishe. Inawezekana kuna baadhi ya walimu wanadai ada au labda kuna jambo linalohusiana na ada au michango shuleni. Hivyo, ukisikia jambo usikimbilie kusema halipo kabla hujajiridhisha kwanza. Kuna baadhi ya mambo huwa yanakanushwa na viongozi, lakini mwisho wa siku unakuta kuna ukweli. Kuwa kiongozi hakuna maana ya kujua kila jambo. Kiongozi anapaswa kuwa a listening person na siyo kukimbilia kukanusha jambo. Nasema hii as a matter of principle.
 
Nyuki wa mashine tu huyoo
 
Huu uzi ukae hapa mpaka august. Isipotokea ally hapi apewe uspika
 
Hii ndiyo shida ya viongozi wengi. Ukisikia jambo, usikanushe kuwa halipo. Fanya utafiti kwanza ujiridhishe. Inawezekana kuna baadhi ya walimu wanadai ada au labda kuna jambo linalohusiana na ada au michango shuleni. Hivyo, ukisikia jambo usikimbilie kusema halipo kabla hujajiridhisha kwanza. Kuna baadhi ya mambo huwa yanakanushwa na viongozi, lakini mwisho wa siku unakuta kuna ukweli. Kuwa kiongozi hakuna maana ya kujua kila jambo. Kiongozi anapaswa kuwa a listening person na siyo kukimbilia kukanusha jambo. Nasema hii as a matter of principle.
Yaani mkuu wa mkoa asiwe na taarifa ama sera rasmi za kiserikali!

Hiki ni kichekesho cha 2022, tena cha kufungia mwaka!
 
Maoni yangu yalilenga 'hao watu wanaotembetembea' na huenda kuna sehemu watu wanalipishwa ada. Hivyo, ni vizuri kujua hawa watu wanaotembeatembea na kusema hivyo, hizo habari wamezipata wapi? Usije ukakuta kuna watu wanapeleka meseji tofauti kwa wananchi ili wakiombwa ada wakubali kwamba imerudi. Hivyo, mimi nilidhani hizi habari ni za kuzifanyia kazi au siyo?
 
Mkuu wa mkoa wa Mara Salum Happi amesema serikali haijarejesha Ada katika shule zake.

Happi amewataka wananchi kupuuza uzushi huo.
===

Mkuu wa mkoa wa Mara Bw. Ally Hapi amewataka wananchi kupuuza taarifa za baadhi ya watu wanaosambaza kuwa serikali imerejesha ada mashuleni jambo ambalo niuongo na wanapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria wanaosambaza uzushi huo.

Hapi ametoa kauli hiyo wakati akikabidhiwa madarasa 113 Wilaya ya Rorya yanayotokana na fedha za maendeleo na UVIKO-19 ambapo wilaya ya Rorya ilipokea bilioni 2.3.

Source: ITV habari

Kama umeme wamerudisha, hilo ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom