Rc Hapi na ndoto kubwa ya mageuzi ya kimaendeleo Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
RC HAPI NA NDOTO KUBWA YA MAGEUZI YA KIMAENDELEO IRINGA

(Afanya uzinduzi mkubwa uwanja wa Nduli, Apambana kuishusha Bombardier Iringa)

Wakati Benjamin Netanyahu ambaye ni kiongozi mashuhuri sana duniani akitokea katika taifa la Israeli kutangazwa mara nyingi zaidi kuwa anauwezo mkubwa wa kufikiri na kupambanua mambo magumu na kukadiliwa kuwa na uwezo wa (IQ 180) akiwa ndiye kinara wa kitatua changamoto tofauti tofauti zilizo washinda viongozi wengine na kujiletea sifa na maendeleo katika nchi yake inayosifika zaidi kuwa ina kiwango kikubwa cha teknohama duniani na sisi hatuwezi kuacha kumtaja RC Hapi kuwa ni kiongozi kijana shupavu mwenye weledi mkubwa wa kupambanua mambo yanayohitaji tiba za papo kwa papo, mh RC Hapi amekuwa kivutio na role model wa vijana wengi kwasasa mkoani petu na hata nchi nzima maana wana Iringa wanajua moto wa huyu kiongozi nguli

Huku nikiendelea kufanya tathimini ya kufahamu ni viongozi wangapi vijana ambao waliwahi kuonesha ujasiri kiutendaji na kupambanua mambo tukiachana na Benjamin Netanyahu wa Israeli basi hapa kwetu Tanzania huwezi kuacha kutaja jina la Edward Moringe Sokoine kwa wakati ule alikuwa moto sana, wakati wa kipindi cha ujana sana cha akina mh William Vangimembe Lukuvi (japokuwa mpaka sasa anapiga kazi ni hatari yaani vijana wajipange) lakini enzi zake akiwa na vyeo vya ukuu wa mikoa Mh Lukuvi alikuwa ni kijana wa moto sana kiutendaji hakika kila kijana wa wakati ule basi walikuwa wanapenda sana kufuata nyayo zake, lakini kwa Africa tunamkuta Thomas Isidore Noel Sankara aliyewahi kuwa raisi kijana huko Burkina Faso aliacha alama sahihi Kabisa kama kielelezo cha vijana wanaoaminiwa kushika hatamu za uongozi katika ngazi mbalimbali.

Hiyo yote ilikuwa ni kuonesha nguvu ya mh RC Ally Hapi mkuu wa mkoa wa Iringa ambaye pia ni kijana Kabisa uwezo, kasi ya kuhisi na kutenda na wepesi mh RC Hapi anafuata nyayo za hao viongozi nguli nchini, ndoto zake za kuona anaowaongoza wanakuwa na amani na maendeleo zinanirudisha katika historia kubwa ya Thomas Sankara licha ya umri wake na ukijana lakini aliwamudu raia wake japokuwa alikuwa anakabiliana na upinzani mkali sana kutoka hata kwa rafiki zake wa karibu kimsingi walikuwa hawapendi kuona kijana ana kuwa na kasi kubwa ya kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika nchi ile.

Bila kupepesa macho RC Hapi amefanya kazi kubwa sana hapa kwetu Iringa ingawa tunasikia sana kuwa hata huko Kinondoni alikuwa hakamatiki lakini huko pengine ya udogo wa eneo kwahiyo wengi tukajua akipewa mkoa atachemka kumbe ndo anafunika na kuchapa kazi kuliko vipindi vyote vya utawala wake huko nyuma. Mh Ally Hapi anagusa nyayo za viongozi mashuhuri vijana wanaofanya vizuri licha ya kuwa wamepewa ngazi kubwa na nyeti za uongozi.

Kwa mda mrefu Iringa hatukuwahi kufikiria kuwa katika uwanja wetu wa ndege ambao ulikuwa kuukuu sana, uliokosa matunzo bora, uwanja ambao ulikuwa umegeuzwa kuwa barabara za watembea kwa miguu na bodaboda, uwanja ambao miundombinu ya majengo yake yalikuwa hayavutii hata kwa kutazama kwa mbali na kiuhalisia uwanja ulikuwa gofu tayari kiasi kwamba hata vile videge vidogo visingeendelea kutua kamoja kamoja hapa. Lakini kwa ujasiri wa mkuu wa mkoa uwanja umefufuka tena na miundombinu imeboreshwa na uzuri zaidi hadi rada za kuongoza ndege zimefungwa na kuuweka mkoa wa Iringa kuwa mkoa wa sita Tanzania kwa kuwa na rada hizo, hili ni jambo la kujivunia sana mh RC.

RC Hapi amepambana mpaka sasa wana Iringa wanatarajia Bombardier na Air Bus kutua katika mkoa wetu mapema sana hapo mwezi wa nne tar 29 na safari zitakuwa kila Jumatano, Ijumaa na Jumapili kwa gharama nafuu kabisa ya sh 140,700TZS hili si jambo la kubeza. Ujenzi wa jengo la kisasa la abiria lililo gharimu sh mil 400 za kitanzania limekuwa kivutio kikubwa katika mkoa wetu, uwepo wa mashine ya kukagulia mizigo na abiria na ununuzi wa gari la zimamoto vimekuwa ni vitu ambavyo Mh RC Hapi anasitahili kupongezwa sana kwa hatua hii kubwa ya kimaendeleo katika mkoa wetu.

Iringa kuna vivutio vingi na vikubwa sana katika nchi yetu na duniani maana huku ndiko vitu vingi vya kihistoria vinapatikana Ismila, Kalenga, Iringa Boma, Mkwawa magic site na mbuga kubwa ya Ruaha hivyo vitakuwa vitu vitakavyo itangaza Iringa na Tanzania kimataifa kwahiyo mh RC Hapi aliona fursa ya namna hiyo na kuona kwamba tunaweza kufanya kitu hakuishia kufikiria pekee ila alianza kuingia katika utendaji wa jukumu hili zito ambalo viongozi wengi hawakuliona lakini wewe Mkuu wa mkoa umeamua kusimama na wana Iringa kwa kututengenezea kitega uchumi kikubwa ambacho kitakuwa faida kwetu kama mkoa na kwa taifa mh unasitahili kushangiliwa hata iweje. Iringa maarufu sana katika kilimo cha mbao tunahitaji kupata wawekezaji wengi na hii njia ya anga itasaidia kuleta wawekezaji hao ndani ya mkoa huu wa Iringa.

Nimekusikia ukitoa wito na fursa kuwa wananchi wajiingize na kuwekeza katika kilimo cha parachichi hata mimi natoa wito tuisikie sauti hii na tuingie shambani tupige jembe tulime parachichi

Lakini kabla sijamaliza haya hapa maoni yangu juu ya watu wanaokubeza mh RC Hapi kwa maana watu kama hao wanatabia zifuatazo ambazo inakupasa kuzipuuza Kabisa weka pamba katika masikio yako chapa kazi vijana tunakusapoti sana. Moja, siyo watu wakusikiliza na kujifunza vitu vipya vyenye maendeleo hao wapuuze, mbili kuna watu wao kazi yao ni kupinga kila kitu, hao wapuuze, tatu kuna watu ambao wao kazi yao kukwamisha shughuli za maendeleo bila sababu zozote ili mradi hawapendi unachokifanya hao wapuuze songa mbele kwa ujasiri mkubwa *huku ukiamini kuwa kuna kundi kubwa linalokuunga mkono*

Mwisho ntaendelea kumshukuru mh rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh na Dr John Joseph Pombe Magufuli kwa kuendelea kutuamini vijana na kutupatia heshima ya kutuamini na kutupatia nafasi za kuwatumikia watanzania ambao kwa imani kubwa walikupigia kura na kukuchagua kuwa amiri jeshi wetu mkuu katika taifa hili kubwa lenye jumla ya watanzania wapatao milioni 57.

I R I N G A N I Z A M U Y E TU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa anatumia vibaya madaraka yake, hana heshima ata kwa wakubwa zake.

MGC
 
Swali langu kwako RC(nafikiri hii ni acc yako jf), umejipangaje na mageuzi ya kilimo?
Ukizingatia Iringa ni ipo kwenye ghala la taifa la chakula

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila siku naona clips anavyodhalilisha watu, hasa viongozi wa chini yake kwenye mikutano ya hadhara. Nafikiri kuna umuhimu mkubwa sana wa wateule wa mtukufu kupata mafunzo kabla ya kuingia kazini. Wana zero kabisa! Sijui wamerithi kwa baba au kwa nani.
 
Back
Top Bottom