RC Hapi Apiga marufuku ufanyaji kazi wa mazoea, majungu, fitina

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
RC HAPI ATEMA CHECHE IRINGA

*Asema hatovumilia watendaji wazembe wanaopuuza wananchi
*Apiga marufuku ufanyaji kazi wa mazoea, majungu, fitina
* Aeleza vipaumbele vyake

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi jana amekutana na kufanya kikao na watendaji mbalimbali wa Mkoa wa Iringa ambapo ameeleza msimamo na muelekeo wa uongozi wake.

RC Hapi alianza kwa kuwataka watendaji wote kuchapa kazi kwa uadilifu na kutatua changamoto za wananchi kwa wakati. Hapi ameonya kuwa hatovumilia mtendaji yeyote ambaye atakua mzembe na chanzo cha kuzalisha chuki kwa wananchi dhidi ya serikali yao.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watendaji wote kuondokana na ugonjwa wa kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuwa wabunifu katika kuwaletea wananchi maendeleo.

"Sitakuwa na huruma na mtendaji mzembe anayesababisha serikali na Chama tawala kuchukiwa. Watendaji wa aina hii hawana nafasi katika mkoa wa Iringa. Kila mmoja lazima ahakikishe changamoto zinazohusu Idara yake anazikabili na kuzipatia majawabu."

Aidha, RC Hapi amekemea tabia ya majungu na fitina kazini na hasa kwa viongozi wapya huku akiwataka kuchapa kazi kwa kumuogopa Mungu.

"Kiongozi ukiwa mgeni mahali kitu cha kwanza unachokutana nacho ni majungu na fitina. Huyu mzuri, yule mbaya, yule hivi; kwangu mimi sitaki majungu. Ukija kwangu uje na jambo lenye ukweli na maslahi ya nchi na wana Iringa." Alisema Hapi.

Mkuu wa Mkoa alianza kwa kutembelea ofisi ya CCM Mkoa wa Iringa na baadae kukabidhiwa ofisi na aliyekua Mkuu wa Mkoa huo Amina Masenza ambapo ameeleza vipaumbele vyake kuwa ni:-
•ulinzi na usalama,
•kuimarisha ukusanyaji na udhibiti wa mapato ya serikali,
•Kilimo (ghala la taifa)
•msukumo uanzishaji wa viwanda vipya
•utatuzi wa migogoro ya ardhi
•mikopo ya vinaja na kina mama kutoka katika mapato ya halmashauri.
 
Kipaumbele cha utalii amekisahau.

Mama Masenza alipigania sana kuipaisha Iringa hasa katika sekta ya utalii. Alipigania eneo la kihesa kilolo ambalo ni zaidi ya ekari 50 kua reserved kwa ajili ya ujenzi wa kanda maalumu ya utalii nyanda za juu kusini.

Sijamsikia mheshimiwa Hapi akizungumzia mbuga ya Taifa ya Ruaha, sehemu za historia kama Kalenga, Isimila nk. Uwanja wa ndege wa nduli
 
Kina Kasesela sasa hamna kitu. ...anayejua kazi Ali Hapi
 
Nakutakia kila la kheri kwa kweli!
Tanzania tunahitaji watu kama hawa sasa!
Kwa kweli tubadilike!
Ngoja nitampelekea matractor kwa ajili ya kilimo!
Nipige pesa!
That’s all!
No fighting no criticism just make money!
KNOW HOW!
 
Kipaumbele cha utalii amekisahau.

Mama Masenza alipigania sana kuipaisha Iringa hasa katika sekta ya utalii. Alipigania eneo la kihesa kilolo ambalo ni zaidi ya ekari 50 kua reserved kwa ajili ya ujenzi wa kanda maalumu ya utalii nyanda za juu kusini.

Sijamsikia mheshimiwa Hapi akizungumzia mbuga ya Taifa ya Ruaha, sehemu za historia kama Kalenga, Isimila nk. Uwanja wa ndege wa nduli
Ametaja vipaumbele vyake sasa we unamlaumu kwa kutotaja vipaumbele vya kwako huoni kuwa unafanya uchochezi mkuu?
 
Mbona yeye kule kinondoni alishindwa wakati ndo miongoni mwa wilaya yenye mapato makubwa,Actions speak louder than empty words,
 
Eti apiga marufuku ufanyaji kazi wa mazoea, majungu, fitina. Kwani kabla yeye hajateuliwa ziliruhusiwa? Mbona Happi unataka kutufanya mbulula hivyo?
 
Back
Top Bottom