Kiongozi makini hapaswi kusikiliza majungu na fitina kisha kufanya maamuzi

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,177
7,749
Hayo yamedhihirishwa leo hii tarehe 13/03/2024 na Rais Samia alipo kuwa akiwaapisha wakuu wa mikoa wapya.

Alitolea mfano wa aliye kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye amehamishiwa Iringa mhe. Serukamba, kuwa alipo kuwa Singida amefanya kazi yake vizuri ila majungu na fitina dhidi yake vilizidi hivyo akaona amuondoe hapo na kumpeleka Iringa.

Pointi ya msingi hapa ni; kama Rais angesikiliza majungu bila kujiridhisha leo hii Serukamba angetupwa nje ila Rais amejiridhisha na kubaini kuwa hakuna ukweli wowote zaidi ya majungu. Serukamba ni mchapa kazi mzuri, mwenye bidii na maarifa lakini alitaka kuharibiwa kwa majungu na fitina.

Hivyo ndivyo kiongozi anatakiwa kuwa, sio kudaka maneno ya majungu na fitina kisha kuumiza walio chini yenu.

Tafiti zinaonyesha majungu na fitina sehemu za kazi yamechangia sana kuwapoteza watendaji wenye uwezo mkubwa kwa kuchafuliwa kwa maksudi.

Viongozi na watendaji wanapaswa kuwa makini sana katika kuongoza kwa haki.
 
Ukiwa boss halafu daily unaletewa majungu,yamaanisha nawe ulipata position nyingi kimajungu na nimtu wa umbeya aka majungu.
Hakuna boss smart atapelekewa majungu kizembezembe.
Na majungu yaendelee🤔
 
Back
Top Bottom