RC Hapi afanya ziara ya kustukiza hospitali ya rufaa Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
*RC HAPI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA IRINGA*

Na Dennis Gondwe
Afisa Habari,
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa

Kufuatia malalamiko ya wananchi Juu ya hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Mkoa huo Ally Hapi amefanya ziara ya kushtukiza huku akitembea kwa miguu kutoka ofisini kwake hadi hospitalini hapo.
Hapi amechukua uamuzi huo huku akitoa mwezi mmoja kwa menejimenti ya hospitali hiyo kujipima na kujitathmini ndani kama wanatosha kuendelea kuwa kwenye nafasi zao.

*“Wagonjwa wanalalamikia kauli mbaya za wahudumu, baadhi ya madaktari kulewa saa za kazi, mafaili ya wagonjwa kufichwa makusudi hadi utoe rushwa na uhaba wa dawa kutengenezwa makusudi ili kunufaisha maduka ya dawa ya marafiki zenu..."*

*"Nitaitazama hospitali hii kwa jicho la karibu. Nawapa muda mfupi wa kubadilika.Vinginevyo tutaufumua uongozi wote katika hospitali hii. Katibu Tawala Mkoa usiwe na huruma nao, chukua hatua."*

Mkuu wa Mkoa alionesha kutoridhishwa na asilimia 76 ya upatikanaji wa dawa muhimu hospitalini hapo huku mapato ya Ndani ya hospitali yakiwa shilingi milioni 195 kwa mwezi.
Aidha, aliitaka hospitali hiyo kujipanga kimkakati kuhakikisha dawa zinakuwepo za kutosha na pale zinapoagizwa kutoka bohari ya dawa ufuatiliaji wa karibu ufanyike ili kuhakikisha dawa muhimu zinakuwepo katika hospitali ya rufaa ya mkoa.
 
Kongole kwake Happi!!
 
Madaktari na ma nurse wa serikali sijui kwanini huwa hawajali wagonjwa kazini kwenye hawafanyi kwa moyo, madaktari kuweni na huruma
 
Huyu jamaa mbona bado hajifunzi kwenda na upepo? CD za kushtukiza haziuziki kwa sasa, kuhama hama vyama ndio zipo sokoni.
Abuni kitu kingine.
 
Safi sana - Kila mfanyakazi wa umma kuwajibika ipasavyo na wajue na kuheshimu wananchi kwani ndio wanaowalipa mishahara yao
 
Huyu jamaa mbona bado hajifunzi kwenda na upepo? CD za kushtukiza haziuziki kwa sasa, kuhama hama vyama ndio zipo sokoni.
Abuni kitu kingine.
Ila atawafanya wa hospital wajitume kazini maana huko mahospitalini huwa wanajisahau
 
Anawashwa huyo maana nimeiona habari kwamba hospitali wanapata asilimia karibu 25 kwa dawa wanazoziomba ambapo ni kama 1 kati ya 4 Ndo mwenye kuweza kupata dawa hao wengine hakuna uwezo. Kinachotokea ni mihemko ya kisiasa eti unachukia wakati dawa hupeleki. mara kuna lugha mbofu sasa kwa nini kuna box la maoni msiandike maoni yenu?

Hiyo ni move ya kisiasa ila ndo ivyo mmepitwa na wakati nyie muwalazimishe chadema wahame wote
 
Madaktari na ma nurse wa serikali sijui kwanini huwa hawajali wagonjwa kazini kwenye hawafanyi kwa moyo, madaktari kuweni na huruma
Tatizo liko kwa aliyewaajiri, maana huyo mwajiri(Serikali) huwa hawajali kabisa, nao wanaishia kufanya kazi kama watumwa wenye njaa, hivyo kimbembe kinaishia kwa Wagonjwa.

Kila mtu apambane na hali yake tu.
 
Back
Top Bottom