RC, DCs Morogoro Kazi yenu ni nini? Milima inateketea!

RC, DCs Morogoro Kazi yenu ni nini? Milima inateketea!

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,753
Reaction score
4,866
Jioni ya leo napita hapa Morogoro na kifaa changu cha mawasiliano, na kama kawaida ya mji huu, kivutio kikubwa ni mpangilio wa milima. Lazima uinue uso kuiangalia milima hii.
Ni jambo la aibu sana kushuhudia moshi mkubwa ukifuka milimani juu, kiashilia kwamba kuna moto au 'mioto' inaendelea kuteketeza milima ya uluguru, tukio ambalo hutokea kila mwaka.

Hakuna anayechukuwa hatua tangu ngazi ya kijiji hadi mkoa na hata chuo kikuu cha SUA ambacho kinajidai kutoa digrii ya usimamizi na uhifadhi wa misitu. Mkuu wa chuo mwenyewe ni mtu wa misitu. Nchi hii inakwenda wapi?? Nani yuko madarakani na anaweza kufanya kazi?

RC hajasikika kwa hatua yoyote. DC hajasikika kwa hatua yoyote.

Milima hii ndicho chanzo cha mto Ruvu. Miaka michache ijayo, morogoro hamtakuwa na maji na mji wa Dar jiandaeni kukosa maji kabisa!!
 
ule moto umewa siku mbili yani ukitizama roho inauma sana.alafu huyu mea wa morogoro alishaimaliza miti kwa kusafilisha magogo nje ya nchi
 
Hii nchi mpaka iwe kama barabara ya vumbi
 
Sasa issue nini hapa?mlima kuungua au Binadamu kuchoma mlima? mambo mengine sio ya kuleta hapa,mambo mangapi yanapita uko kimya ili hili la moto ndo linakutoa roho!
 
Kazi ya SUA ni kufundisha, kutafiti, ushauri na huduma kwa jamii , lakini siyo huduma ya kuzima moto mlimani

Hapo wanatakiwa kufanya kwa vitendo na hiyo ni real practical.
 
Mkuu wako busy na utaratibu wa goli la mkono! Ukiwauliza watakuambia hela hawana hata kuwashawishi wananchi tu!
 
hata huyo RC/DC hatakuja na kalipio au agizo la kukataza uchomaji wa misitu... na wala sio jitihada za kuzma moto.
 
Back
Top Bottom