RC Chalamila; Kila nyumba Dar iwe na Dustbin

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
443
Reaction score
1,101
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Albert Chalamila, ameagiza kila nyumba kuwa na kifaa cha kuhifadhia taka (dustbin) angalau mbili kama sehemu ya juhudi za kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi na mazingira yanatunzwa.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari leo Septemba 17, 2026, Chalamila amesema hatua hiyo itasaidia kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa safi.

Amesema pamoja na nyumba, magari ya abiria maarufu kama daladala yanapaswa pia kuwa na vifaa maalumu vya kuhifadhia taka ili kuzuia uchafu kutupwa ovyo

​
 
Inabidi wafanye mpango wa dustbin kuuzwa bei rafiki,na usafi wa kutumia dustbin kuna mifuko ya nylon special kwa kuwekea taka inabidi wairuhusu
 
Inabidi wafanye mpango wa dustbin kuuzwa rafiki,nq usafi wa kutumia dustbin kuna mifuko ya nylon special kwa kuwekea taka inabidi wairuhusu
Huyo alietoa hilo tangazo hana hio exposure. Hajui hizo bins ni special kwa magari ya taka maalum likija bin linapachikwa na kuinuliwa automatically kumwaga taka kwenye gari linalosaga taka. Na lazima uweke mfuko mgumu mweusi kwa usafi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…