RC azipa wiki mbili Halmashauri kukamilisha madarasa

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile ametoa muda wa wiki mbili kwa kila halmashauri mkoani hapa, kuhakikisha wanafunzi 3,150 ambao hawajachaguliwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari wanaanza masomo.

Alitoa agizo hilo jana katika kikao cha kujadili tathimini ya usambazaji wa vocha za pembejeo na taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza kilichohudhuriwa na wakuu wa wilaya, wabunge na maofisa wengine kutoka katika halmashauri.

Mwakipesile alisema agizo hilo linapaswa kuanza kutekelezwa kuanzia leo na kumtaka Ofisa Elimu Mkoa, Juma Kaponda kuanza kufuatilia na patakapoonekana kuwa na shida, atoe taarifa mara moja ili hatua za haraka zichukuliwe.

“Nasema agizo hili ndani ya wiki mbili litekelezwe na wanafunzi waanze masomo.

Nimetoa agizo na siangalii sijui halmashauri moja ina idadi kubwa ya watoto wala ndogo, ninachotaka mimi ni wiki mbili watoto wawe darasani.

Kauli nyingine sihitaji,” alisisitiza RC. Pia mkuu huyo wa mkoa alitengua agizo la kuwataka wakuu wa wilaya kutokwenda likizo kabla ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo alilolitoa hivi karibuni, ambapo alisema wakuu hao wa wilaya wamefanya kazi kubwa hivyo
wanaruhusiwa kwenda kupumzika.

Kwa mujibu wa Kaponda, Halmashauri ya Jiji la Mbeya inaongoza kwa kuwa na watoto 1,102 ambao hawajachaguliwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika shule wanazotakiwa kujiunga za Ilomba, Lyoto, Mponja, Ihango, Mwakibete, Sinde na Iyela.

Mbeya vijijini inafuatia ikiwa na wanafunzi 775 wanaopaswa kwenda katika shule za sekondari za Yalawe, Mwaselela, Songwe, Malama na Shibolya.

Wilaya ya Chunya ina wanafunzi 351 ambao wanatakiwa kwenda katika shule za Kapalala na
Chalanga.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ina wanafunzi 342 na wanapaswa kujiunga na sekondari za Rujewa, Igomelo na Mbarali.

Wilaya ya Mbozi inao 253 wanaopaswa kwenda katika shule za Itumpi na Lwati wakati Rungwe wapo 170 wa shule ya Mpandapanda na Kyela ina wapo 155 wa shule ya Mwaya.

Kaponda alisema vyumba vinavyohitajika kwa halmashauri ya jiji iliyo na historia ya kukumbwa na tatizo hilo kila mwaka ni 28 ikifuatiwa na Mbeya vijijini inayohitaji vyumba 21.
 
Back
Top Bottom