Lorenzo Samike
JF-Expert Member
- Jun 18, 2021
- 1,184
- 1,914
Huyu anayeitwa Anthony Mtaka ni muda sasa nimeanza kumsikia lakini sikumtilia maanani kivile. Hata wakati wa Magufuli nilikuwa namsikia sikia tu kwamba ati ni Mkuu wa Mkoa bora. Akapewa sijui na tuzo!
Binafsi sikuwahi kumfuatilia kwa sababu sikuwahi kuvutika nae. Nilikuwa namsikia sikia tu kwa juu juu sana. Hivi majuzi alivyoteuliwa kuwa RC Dodoma nilimuona anazungumza akitoa hotuba fupi.
Kwanza ni wa kawaida sana na anaonekana ana majigambo ya ujuaji. Hata lugha yake ya mwili inaonesha anajidhania kwamba yeye ni mtaaluma na mjuvi kuliko wengine.
Jana tu hapa kamfokea Waziri wa elimu na kuyapuuza maagizo yake kwa kejeli na dhihaka. Hii kiprotokali sijui imekaaje?
Udhalilishaji wake dhidi ya Waziri umethibitisha yale yote niliyokuwa nayafikiri juu yake — Kwamba ni mjuaji juaji tu.
Na si ajabu anawalipa watu mitandaoni ili wamsifie sifie. Binafsi sioni kama ana ubora wowote au maajabu yoyote.
Kwani amefanya kitu gani hicho mpaka astahili misifa yote hiyo ninayoisikia mitandaoni kutoka kwa wafuasi wake pendwa?