Hongera sana RC Simiyu Ndugu Anthony Mtaka, wewe ni kiongozi kweli

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,536
Uongozi maana yake kuonesha njia na ku-influence wengine wawe vile utakavyo ama inavyotakiwa wawe.

Miongoni mwa mikoa yenye jamii ngumu kuziongoza kuelekea kwenye "peak" ya mapinduzi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ni mikoa ya kanda ya ziwa inayoundwa na Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera......

Binafsi, nichukue na niitumie fursa hii pekee kuandika kukupongeza wewe binafsi na uongozi wote wa mkoa wa SIMIYU kwa ujumla chini yako, RC ndg Anthony Mtaka.

For sure, mimi si mpenzi wala shabiki wala kukubaliana na uongozi wa serikali hii ya CCM ya awamu ya tano chini ya Rais ndg John P. Magufuli lakini nimetokea kuvutiwa sana na staili na talents za uongozi kwa baadhi ya viongozi na mmojawapo ukiwa ni wewe RC wa mkoa wa SIMIYU, Bw Anthony Mtaka.

Huyu bwana ni miongoni mwa viongozi wachache ndani ya CCM wenye very strong withstanding leadership qualities....

Kiukweli umepikwa na ukakapikika na umefaa na kufiti vilivyo ktk nafasi hiyo....

Huna makeke, majivuno na ni mtu unayejua kusikiliza na kushirikisha watu katika uongozi wako ili ku - achieve malengo fulani katika mipango ya maendeleo ya kijamii....

Wewe bwana ni miongoni mwa viongozi wachache charismatic na wabunifu ktk Tanzania ya leo hususani huko CCM, wenye akili na uwezo mkubwa wa kubadili mazingira yasiyofaa ili yafae na kuwa ya manufaa kwa jamii husika around.....

Wewe ni kiongozi unayeweza kutenganisha siasa na kazi za kitaaluma kwa ufasaha na kuleta matokeo yenye manufaa ktk jamii bila kuhisi kuwa unakosa persinal - security yako dhidi ya ukada wa chama chako!!

For instance, wote tunajua kuwa Simiyu ni miongoni mwa mikoa michanga sana yenye umri wa miaka isiyozidi mitano tu tangu kuzaliwa kwake toka ktk mkoa wa Shinyanga.....

Mazingira yake ni magumu na kwa kweli ilikuwa ni mkoa wenye jamii ya watu walio nyuma sana ktk nyanja za maendeleo yote ya kiuchumi na kijamii hususani elimu.

Lakini tangu umekuja hapa na kuwa RC kuongoza mkoa huu, umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuweza kuusogeza hatua kadhaa mkoa huu kimaendeleo hususani ktk sekta ya elumu.....

Aidha umeiunganisha jamii na kuishirikisha vilivyo ktk kutenda ili kuyafikia malengo haya bila ya kutenda kwa kuongozwa na mihemuko ya itikadi za kisiasa waziwazi.....

Mfano mmoja ni huu; kwamba, katika sekta ya elimu chini ya uongozi wa huyu ndugu, mkoa huu umeweza kuwa
juu ktk ramani ya Tanzania na sasa ni miongoni mwa mikoa mitano bora inayofanya vizuri ktk sekta hii ya elimu!!

Kabla, mkoa huu katika sekta ya elimu ulikuwa unakuwa ranked sawa na mikoa ya Zanzibar, Lindi, Tabora nk. Haya ni mafanikio makubwa sana!!!

RC Anthony Mtaka na sekretariat yako yote ya mkoa wa Simiyu, pokeeni hongera zangu za dhati kabisa na kwa kweli hii ndiyo maana halisi ya uongozi.

Kwamba, kiongozi bora ni yule anayepimwa kwa matokeo bora ya malengo yaliyowekwa hii ikiwa ni pamoja na uwezo wa kuiweka na kuinganisha jamii kubwa na pana kuweza kuishi kwa umoja na ushirikiano......

For me naweza bila shaka yoyote kusema, you deserve to be the president this beautiful nation. You are far better than Mr John Pombe Magufuli...

Hatungeweza kupata maendeleo haya kama ungekuwa unaongoza mkoa kwa mtindo kama wafanyavyo maRC wengine wa kugawa watu kwa misingi ya itikadi zao za kisiasa...

Kwako wewe hili mimi sijaliona, nadhani ndiyo maana unapata ushirikiano mzuri toka kwa watu wote kwa kila mpango unaouanzisha ndani ya mkoa wako...

Hongera sana na endelea hivyo hivyo na pengine ongeza juhudi zaidi na kuboresha maeneo yenye mapungufu...

Bwana Yesu Kristo akuongoze na neema yake ikufunike daima!!

====

  • Je Mtaka ni nani?

    1. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mheshimiwa ANTHONY JOHN MTAKA CHIGANGA alizaliwa tarehe 5 Julai 1983 mkoani Mara. Yeye ni mtoto wa kwanza kati ya wanne wa Bi. Merciana Mageti na Bw. JOHN MTAKA CHIGANGA.

    2. Mheshimiwa Mtaka alisoma Shule ya Msingi Suguti, Musoma mkoani Mara ambapo alimaliza mwaka 1996.

    3. Mheshimiwa Mtaka alisoma Shule ya Sekondari ya Mwembeni, Musoma mkoani mara toka mwaka 1997 hadi 2000 na akasoma kidato cha tano na sita mwaka 2001 hadi 2003 huko Kilimanjaro.

    4. Mwaka 2004 alijiunga na Chuo cha Ualimu Marangu lakini akaacha baada ya nusu mhula na kujiunga mafunzo ya Jeshi la polisi kabla ya kujiunga ambapo yeye ni F.6886 PC A. Mtaka. Baadae mheshimiwa Mtaka akaenda kusoma Chuo Kikuu Mzumbe alikopata shahada ya Utawala mwaka 2009.

    5. Mheshimiwa Mtaka aliteuliwa na Rais DR. JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu tarehe 13 Machi 2016.

    6. Mheshimiwa Mtaka ni mmoja wa Wakuu wa mikoa wadogo kabisa kuwahi kutokea nchini.

    7. Kabla ya kuwa Mkuu wa mkoa Mheshimiwa Mtaka alihudumu PPF, pia alikuwa Mkuu wa Wilaya za Mvomero na Hai baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa JAKAYA KIKWETE, Rais wa awamu ya nne wa nchi yetu.

    8. Mheshimiwa Mtaka ana vipaji lukuki: ni mwanariadha na Mwenyekiti wa chama cha riadha nchini, ni askari, ni mwimbaji hodari wa nyimbo za injili na ametunga nyimbo zake, ni mwandishi mzuri wa makala, ni msomaji mzuri wa vitabu vya Kiswahili na Kiingereza na pia ni mpenzi kindakindaki na mwanachama wa YANGA, ambayo kihistoria, ni moja ya timu bora kuliko zote zilizowahi kutokea nchini.

    9. Mheshimiwa Mtaka ni Kiongozi Mnyenyekevu, mwenye busara na staha na asiye na mihemko. Ni aina ya viongozi wa kisasa mwenye hofu ya Mungu na aliye na heshima kwa wakubwa na wadogo.

    10. Mheshimiwa Mtaka sio mpenda ‘kiki’. Ni mwerevu, mwenye kuamini umoja katika kuleta maendeleo na kuwa uongozi si bla bla na kupandisha mabega juu bali ni kwaajili ya kuwatumikia wananchi . Aliwahi kuandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa, (namnukuu) “Niwakumbushe tu wenzangu kuwa cheo ni dhamana. Walikuwepo viongozi kabla yetu na watakuja wengine baada yetu. Mkipewa uongozi epukeni kubeba hivi vyeo mabegani” (Mwisho wa kunukuu)

    11. Mheshimiwa Mtaka ni mchapakazi hodari. Mkoa wa Simiyu ulianzishwa mwaka 2012 na ulikuwa uko nyuma sana kimaendeleo. Lakini, wakati mikoa mingine mingi bado haisomeki (ikisua sua kimikakati ya maendeleo), mkoa wa Simiyu chini ya uongozi imara wa mheshimiwa Mtaka umepiga hatua kubwa na kuwa mkoa wa kupigiwa mfano. Sherehe za Nane nane kitaifa ambazo mwaka huu zilifanyika Simiyu zilithibitisha hili.

    12. Mheshimiwa Mtaka amekuwa na mafanikio katika kuunga mkono azma ya Rais ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati. Mheshimiwa Mtaka ameasisi kauli mbiu aliyojifunza toka Japan : ‘Kijiji Kimoja, Bidhaa Moja’, inayochagiza ujenzi wa viwanda. Tayari Mheshimiwa Mtaka alizindua kiwanda cha maziwa na cha chaki alivyovizindua Novemba 2016 na vingine vipo njiani.

    13. Mkoa wa Simiyu umeweza kupata wawekezaji wazawa wengi kutokana na juhudi za Mheshimiwa Mtaka.

    14. Mheshimiwa Mtaka ni kipenzi cha wananchi wa Simiyu kutokana na mabadiliko makubwa aliyoyaleta mkoani humo.

    15. Mheshimiwa Mtaka amekuwa mstari wa mbele kuhimiza elimu ambapo ameahidi kutoa mamilioni kwa wanafunzi watakaofanya vizuri kitaifa. Aidha, amewaasa wanafunzi hao wasome hadi usiku wa manane ili wafaulu na kuja kuusaidia mkoa wao kupata maendeleo.

    16. Mheshimiwa Mtaka alipiga marufuku muhemko usio na kichwa wala miguu wa ma-DC kuwasweka ndani watumishi wa umma ambapo alisema, ” Sisi viongozi tuwalinde watumishi wetu. Nilipoteuliwa kuwa RC niliwajulisha ma-DC wangu kuwa moja ya mambo nisiyotaka kusikia ni watumishi kuswekwa ndani. Sitaki kusikia hata wabunge, madiwani kuswekwa ndani hovyo”.

    17. Tarehe 07 Septemba 2017, Mheshimiwa Mtaka alipewa Tuzo na Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania kutokana na maendeleo makubwa aliyoyafanya mkoani humo katika kipindi kifupi tu cha uongozi wake ‘Chema Chajiuza, Kibaya Chajitembeza’.
 
Mtaka yupo vzuri tangu alipokuwa DC mvomero zama za JK. Nilishawahi kumtembelea Ofisini kwake miaka hiyo 2014 wakiwa na DED ambaye ni boss wa TFF kwasasa. Katika kuzungumza naye niligundua jama ni visionary leader na anapenda kujipima kwa matokeo sio maneno. Nisiseme mengi lkn kwa uchache ni kuwa jamaa ana hekima pia kwa machache ninayoyafahamu/ kumdhania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila niwatahadharishe kidogo. Wakati polisi walipo vamia kikao cha Bawacha Bariadi na kuzuia kisifanyike na sababu za kibabe tuu kutolewa niliamua kumchunguza Mtaka ninaye msikia sana.
Nilichogundua ni kuwa Anthony Mtaka pamoja na ukweli kuwa ni tofauti sana kiutendaji na watu kama Makonda na wengine lakini pia ni bingwa wa kununua waandishi kuandika habari zake za sifa ambazo hata zisizo kuwepo.
Pascal Mayalla atakuwa amenielewa vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichogundua ni kuwa Anthony Mtaka pamoja na ukweli kuwa ni tofauti sana kiutendaji na watu kama Makonda na wengine lakini pia ni bingwa wa kununua waandishi kuandika habari zake za sifa ambazo hata zisizo kuwepo.
Pascal Mayalla atakuwa amenielewa vizuri sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
This is news to me!, ila ni kawaida unapokuwa ni kiongozi mzuri na unafanya makubwa kama Anthony Mtaka, wanga hawakosekani ili kuleta fitna na kupiga majungu. Labda kama utanitajia angalau sifa moja tuu Anthony Mtaka aliyepewa na waandishi akampa sifa zisizo zake!Kama ni kweli Mtaka analipa waandishi ili wamsifie, hebu msikilize huyu mtu anasema nini kumhusu RC Mtaka, naye amelipwa?.
Rais Magufuli amtangaza RC Mtaka kuwa ndie RC bora Tanzania – Millardayo.com
8 Sep 2018 · Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amesema Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ndie Mkuu wa ...

Magufuli ampongeza RC wa Simiyu Anthony Mtaka | Azam | Habari | Swahili
8 Sep 2018 · Rais John Magufuli amempongeza mkuu wa mkoa wa Simiyu, David Mtaka kwa kuongoza kiutendaji miongoni mwa wakuu wa mikoa. Pongezi

P
 
Pascal Mayalla, OK,OK Pascal ngoja niweke sawa data nitiririke ingawa tutakuwa hatumtendei haki Mtaka kwa kuweka hadharani mbinu hizo maana pamoja na mbinu hizo nimetahadharisha kuwa bado yeye ni bora kuliko Makonda na wenzake lakini sio kama anavyopambwa.
Na kuhusu hizo quote za sifa zilizotolewa na mzee, bado unamuamini mzee kama credible source ya information kama hizo za kusifia mtu? Bado hujajuwa yeye hata sifa inategemea kazipokeaje au lawama kazipokeaje na yuko wapi?
Kwangu mimi (na pengine wengine including wewe) ayasemayo mzee jukwaani yakuchukuwa ni 30% tuu. Mengine ni mizaha, no research Info's, chuki na propaganda tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
OK,OK Pascal ngoja niweke sawa data nitiririke ingawa tutakuwa hatumtendei haki Mtaka kwa kuweka hadharani mbinu hizo maana pamoja na mbinu hizo nimetahadharisha kuwa bado yeye ni bora kuliko Makonda na wenzake lakini sio kama anavyopambwa.
Na kuhusu hizo quote za sifa zilizotolewa na mzee, bado unamuamini mzee kama credible source ya information kama hizo za kusifia mtu? Bado hujajuwa yeye hata sifa inategemea kazipokeaje au lawama kazipokeaje na yuko wapi?
Kwangu mimi (na pengine wengine including wewe) ayasemayo mzee jukwaani yakuchukuwa ni 30% tuu. Mengine ni mizaha, no research Info's, chuki na propaganda tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kufuatia Ikulu kuwa ni mahali patakatifu, mpangaji wetu wa mahali patakatifu petu ni mtakatifu, hivyo kwa mujibu wa katiba yetu, yeye ndie the most reliable source, hata akisema tuu
"Chakaza ni msaliti na wasaliti huwa wanafanywa nini vitani, tuko kwenye vita vya kiuchumi ni mbaya kuliko vita ya silaha, msaliti kama huyu hawezi akaachwa tuu aka survive!"

Within dakika sifuri Chakaza uta chakazwa!.

Ni kwa utakatifu huu ndio maana hawezi kukosea na hawezi kushitakiwa. Akisema RC Mtaka ndie the best, Mtaka is the best.

P
 
Kufuatia Ikulu kuwa ni mahali patakatifu, mpangaji wetu wa mahali patakatifu petu ni mtakatifu, hivyo kwa mujibu wa katiba yetu, yeye ndie the most reliable source, hata akisema tuu
"Chakaza ni msaliti na wasaliti huwa wanafanywa nini vitani, tuko kwenye vita vya kiuchumi ni mbaya kuliko vita ya silaha, msaliti kama huyu hawezi akaachwa tuu aka survive!"

Within dakika sifuri Chakaza uta chakazwa!.

Ni kwa utakatifu huu ndio maana hawezi kukosea na hawezi kushitakiwa. Akisema RC Mtaka ndie the best, Mtaka is the best.

P

Pascal asante kwa tahadhari. Lakini sisi wana TANU wa zamani tunaikumbuka ile ahadi kuu ya mwana TANU. "Nitasema kweli daima fitina (uongo) kwangu mwiko"
Kuua MTU mmoja mwenye haki ni kuleta laana kwa muuaji had I kizazi cha NNE. Mwenye sikio na asikie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Apewe wizara ya elimu tuu kuna siku niliona makala moja AZAM tv Mtaka ana mipango ndomana anafanikiwa na msikilizaji sanaa kwa walimu na anawapa motisha wanaofanya vzuri
 
Pascal asante kwa tahadhari. Lakini sisi wana TANU wa zamani tunaikumbuka ile ahadi kuu ya mwana TANU. "Nitasema kweli daima fitina (uongo) kwangu mwiko"
Kuua MTU mmoja mwenye haki ni kuleta laana kwa muuaji had I kizazi cha NNE. Mwenye sikio na asikie
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuua msaliti ni ushujaa na utabarikiwa kwa baraka tele!, only if kama ni msaliti kweli, kwasababu kesi ya usaliti wa nchi, ni uhaini na hukumu yake ni kifo, No. 1 akimtangaza mtu hadharani kuwa ni msaliti, na kutolea mfano wa wasaliti vitani huwa wanafanywa nini, na kueleza vita vya kiuchumi ni ngumu kuliko vita vya kawaida!, na aliyeeleza hayo ni CinC!, what do expect kwa the "operatives", what message is he sending?, when CinC says something or speaks about something, kwa wengine ni kuongea tuu, but kwa wengine it's like a coded message, 'an order', ni amri!, likitokea la kutokea bado utashangaa?!.

Lakini kama sio msaliti kweli na anatuhumiwa kwa usaliti na kuhukumiwa kwa kupewa adhabu ya usaliti kwa maonevu, kwanza Mungu atamkingia kifua, na pili karma itawashughulikia, watesi wake wakiwemo watuhumu, japo kweli hili, "mtamka wasaliti" is exempted adhabu ya karma, kwasababu yeye emeletewa tuu taarifa na vyombo vyake!.

P
 
Mtaka yupo vzuri tangu alipokuwa DC mvomero zama za JK. Nilishawahi kumtembelea Ofisini kwake miaka hiyo 2014 wakiwa na DED ambaye ni boss wa TFF kwasasa. Katika kuzungumza naye niligundua jama ni visionary leader na anapenda kujipima kwa matokeo sio maneno. Nisiseme mengi lkn kwa uchache ni kuwa jamaa ana hekima pia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi simjui kwa karibu hivyo.

Lakini sifa za kiongozi mzuri hazijifichi, zitaonekana tu bila ya yeye kujitangaza.

Mara ya kwanza kumsikia huyu ndugu ni wakati wa shughuli za 'promotion' za mkoa wake zilizofanywa mkoani miaka mitatu au minne iliyopita na kuandikwa magazetini.

Mipango yake ya mkoa alivyoielezea na namna alivyopanga kuisimamia ilionyesha dhahiri alikuwa akizungumzia alichokijua na kukiamini.

Baada ya hapo, nimekuwa nikifuatilia kujua kama aliyokuwa ameyapanga ndio anayoyatekeleza. Sijaona popote alipotetereka na sioni akipiga kelele nyingi ili aonekane. Sijaona wala kusikia habari zozote kujihusisha na makundi mbalimbali yenye maslahi binafsi.

Huyu ni kiongozi mzuri wa kutegemewa katika nchi yetu. Bila shaka ataendelea kutumika katika nafasi stahili kuliendeleza taifa letu. Viongozi wa aina hii ni nadra sana kuwapata nyakati hizi.
 
Back
Top Bottom