Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
na Betty Kangonga na Bakari Kimwanga
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimetakiwa kuchukua hatua za haraka kutatua mapungufu yaliyojitokeza visiwani Zanzibar wakati wa kipindi cha uchaguzi vinginevyo kuna uwezekano wa kupoteza dola katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Pia kimetakiwa kuhakikisha kinafanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu uliopita na kuangalia sababu zilizochangia viongozi wastaafu kushindwa kupewa nafasi wakati wa kampeni.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mfanyabiashara maarufu visiwani humo, Mohamed Raza, alipozungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa viongozi wa juu wa CCM wanapaswa kuyafanyia kazi masuala hayo, ili kuwatoa hofu wananchi.
Alisema kamwe kundi fulani haliwezi kuongoza visiwa hivyo na wala ndani ya chama hicho hakuna bwana wala mtu maarufu bali kinachompa haki ya kuongoza ni chama hivyo viongozi wawe wazi kuzungumzia suala hilo kwa wananchi.
Raza alisema kipindi cha kampeni mpaka uchaguzi kulikuwa na mapungufu hatua iliyosababisha CCM kuwa na ushindi wa tofauti na mwaka 2005, hali ambayo inatoa taswira ya kutopata nafasi katika uchaguzi ujao wa 2015.
Alisema inasikitisha kipindi cha kampeni viongozi wastaafu walishindwa kushirikishwa huku wakiachwa kando jambo ambalo limeonekana kutoa taswira mbaya kwa wananchi hali iliyosababishwa na kukosekana mshikamano na uzalendo wa pamoja miongoni mwa wanachama.
Wapo hata viongozi wastaafu walioamua kujipeleka wenyewe katika kampeni za chama hicho tena pale Kibanda Maiti ambapo kwa sasa panaitwa Kibanda Uhai na wananchi walishangilia walipomuoa Komandoo (Dk. Salmin Amour), alisema.
Alisema kuwa kiongozi huyo mstaafu hakupewa hata nafasi ya kuwasalimia wananchi waliokuwa katika mkutano huo licha ya kujipeleka kitendo ambacho hakipaswi kunyamaziwa.
Alisema kutokana na hali hiyo Chama cha Mapinduzi (CCM), kina kazi kubwa ya kutibu majeraha hasa kutokana na baadhi ya viongozi wastaafu wa serikali kutoshirikishwa na hata majina yao kuondolewa katika ratiba za kampeni katika Uchaguzi Mkuu uliopita.
Mimi bado nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM, ila ninatumia uhuru wangu kwa kuionya CCM ni lazima iangalie hali na kujua ni nini kinasababisha kukosekana umoja kwani 2015 tunaweza kujikuta tukiambulia nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, alisema Raza.
Alisema ilipoingia serikali ya awamu ya sita visiwani humo ilifika hatua ya kuwanyanganya magari pamoja na ulinzi baadhi ya viongozi wastaafu waliotangulia kuongoza serikali ya Zanzibar.
Kada huyo, alisema ni lazima viongozi watambue CCM inaongozwa kwa busara na sio mtu na kutoa wito kwa viongozi wa Halmashauri Kuu kuangalia katiba ya chama juu ya umuhimu wa viongozi wastafu wa serikali na nafasi zao.
Raza, ambaye alikuwa mshauri wa masuala ya michezo wa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. Salmin Amour, alisema kamwe CCM haiwezi kuzuia upepo wa kisiasa uliopo sasa Zanzibar kama wataendelea kufumbia macho hatua ya kutowapa kipaumbele wastaafu wa serikali hasa waliohudumu katika nafasi ya juu ya urais.
Kuhusu wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukacha hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, alisema hakuna budi vyama vikakutana na kuzungumza kwa kuhakikisha maslahi ya wananchi yanawekwa mbele.