Raza awanyooshea kidole viongozi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Raza awanyooshea kidole viongozi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ochu, Mar 25, 2009.

 1. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Raza awanyooshea kidole viongozi CCM

  na Mkolo Kimenya


  MFANYABIASHARA Mohamed Raza, amewataka viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakweli katika mambo yao kabla ya kukimbilia kutoa taarifa kwa wananchi.

  Huku akionyesha kuwalenga baadhi ya wabunge, Raza alisema viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi wanapaswa kujiondoa katika Halmashauri na Kamati Kuu ya (CCM) ili kukipa heshima chama.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana, jijini Dar es Salaam, Raza alionyesha wasiwasi wake kuhusu mwenendo wa mambo yanayojitokeza katika siku za karibuni yanayoonyesha baadhi ya viongozi kujali zaidi maslahi binafsi ambayo kwa namna moja au nyingine yanaiathiri jamii.

  Alisema ubabe unaofanywa na baadhi ya watendaji, ndio chanzo cha hali zinazojitokeza za malumbano ambayo kamwe hayawezi kujenga nchi.

  Alitoa mfano kuwa mtu akivaa shati, nje likiwa safi na fulana ya ndani ikawa inatoa harufu maana yake ni mchafu, hivyo haiwezekani kutoa ukweli kwa watu wengine huku yeye hasemi ukweli unaomuhusu.

  “Lazima tuwe wakweli na tukiacha haya mambo yaendelee yawezekana uhuru wa Tanzania na Mapinduzi Zanzibar kutoweka kwa ajili ya matajiri wachache.

  “Hali ya nchi inatisha, tukiendelea kuyatazama haya yanayotokea sijui nchi tunaipeleka wapi, tunapaswa kulitazama hili ili kuinusuru nchi,” alisema Raza.

  Raza alisema sheria inapaswa kuchukua mkondo wake kwani kuna mabilioni ya fedha yamechukuliwa na matajiri huku karibu asilimia 90 ya Watanzania wakilia njaa.

  “Watu wanajulikana, hii subiri subiri inatoka wapi? Wachukuliwe hatua ili kujenga uaminifu kwa wananchi, Rais hawezi kufanya mambo yote peke yake lazima awe na wasaidizi, hivyo wamsaidie kwa kumtaarifu mabaya yanayotendeka na si kumueleza mazuri yaliyopo.

  “Nina hofu ndani ya chama changu na kama tungepata upinzani wenye nguvu, tungepata shida sana bungeni, kwani kinachoniumiza ni kuwa bado tunatakiwa kurudi kwa wananchi, tutawaambia nini?” alihoji Raza.

  Alisema kitendo cha watu kuingiza masuala binafsi na kuchafuana katika masuala yanayogusa jamii ni kutaka kuzima hoja zizilizopo.

  Aliwalaumu watu wanaohuburi ukabila na udini kwa kutaka kuficha ukweli na kuwataka Watanzania kutokaa kimya wakiangalia uovu huu ukiendelea kutendaka.

  upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM; mwalimu alisema
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nakumbuka niliwahi kufunga na kuomba kwamba CCM wameguke, naona maombi yanaanza kujibhiwa kwa hatua kwani wameanza kutoana macho ili wasione kabisa the iwe rahisi KWETU kushika hatamu (patamu)
   
 3. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #3
  Mar 25, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  UFISADI utawatoa wengi. huyu jamaa yupo????
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kandambilimarambili
  swali lako ni gumu.
  ila lets see kama yumo au la.
  Eleweni kitu kimoja kuwa Chama Chetu ni mabingwa wa propaganda na siasa za kuigiza, isije ikawa wanatufanyia maigizo ionekane kwambwa wanapingana kisha usiku wanagonganisha glass kupanga game itakayofuata.... Am curious ktk hili.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni kuwa CCM ile iliyokuwa inakubali kujikosa ilishakufa... iliyopo sasa ni ya wajuaji ambao hawakosei. Kila Mara Chiligati amekuwa akitetea kuwa wanaotuhumiwa ni individual members as if chama kinajengwa na collective members. hajui kuwa hao individuals nduio wanaotengeneza chama na iwapo wataonekana kuwa hawafai, basi na chama kitaonekana kuwa hakifai. hapa hatyujatoa mfano wa samaki akioza mmoja...
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  individuality = sisiemu
  Ila hao indivual members wakifanya mambo ya maana basi sifa itaenda kwa chama. kaazi kwelikweli
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tabia ya kukosoana ipo CCM kwa muda mrefu tu, ila wengine hupenda kukusoa huku wakitafuta umaarufu.
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Ukisikia ukuda ndio kama huo
   
 9. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nilichojifunza nalo hapa ni mambo mawili.
  Kumbe Uzalemdo si rangi wala kabila la mtu kama tulivyoambiwa na baadhi ya Wakubwa wetu kuwa Wazalendo ni wenye asili ya Uafrika tu.

  Kumbe unaweza ukawa mfanyabiashara na mwanachama wa CCM na isiwe lazima uwemo kwenye Kamati Kuu au Ubunge.

  Pengine hii migogoro ya maslahi na ufisadi ingeepukwa kama mambo mawili hayo yangefuatwa.
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Pengine ungejuiliza kwanini watu wengi wanapokuwa juu kiuchumi/kimaisha/kisiasa katika kipindi fulani maneno na kauli zao huwa tofauti na wanapokuwa chini.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ukuda inasaund very interesting, hebu tupe tuition maana ya ukuda
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  tena lakushangaza zaidi ni viongozi wa ngazi za juu za chama ambao walipaswa kuwa mfano na mstari wa mbele kulinda maslahi ya taifa hili.
   
 13. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ingawa tabia ya kukosoana CCM ilikuwepo tangu muda mrefu, haijawahi kutokea wakakosoana kama ilivyo sasa. Hizi ni dalili kwamba kuna mmong'onyoko ndani ya chama (nyufa). Kila mtu ataibuka na lake kujifanya anakemea migongano ndani ya chama lakini ukweli utabakia, hali si nzuri ndani ya CCM (mafisadi wanakitafuna chama sasa). Tuzidi kuiangalia hii sinema,bado watakuja wengi tu!
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hizo ni longolongo za waliochoka , huyo nae kwani ni fisadi kidogo ,huyo Raza ndie yule aliewanunulia mapanga watu na kutaka wayatumie katika kuuwa jamaa zao, au amesahau ,huyu nae aliwahi kuzabwa kibao na Karume hadi leo picha haziendi ,wakati Karume ni waziri wa Biashara yeye akiwa mshauri wa Salmini Amuri.
  Na ni mmoja wa anesemekana anahusika na madawa ya kulevya pale Zanzibar ,sijui kama hayumo ndani ya listi ya Mkwere.

  Tatizo la jamii za Kitanzania zenye asili ya Kihindi huwa ni watu wa maslahi na hubadilika na wakati ,kesho CUF ikiingia madarakani basi si hasha ukamsikia anawapelekea kontena la bendera , aloo bora mwambieni achunge maana CUF haitakubali kuhongwa kama anavyohonga huko kwa Sultani CCM ,mambo yatakuwa ni straight forward ,fuata sheria kwisha ,unahusika na ubadhirigfu ushahidi kidogo tu utasaidia kukukwamisha japo mwezi jela. Alimuradi wananchi waridhike basi ,maana wakisharizika wananchi ndipo hatua ya manedeleo itakapoweza kupatikana ,lakini kwa hizi longolongo zao kila mmoja anasoma shairi kumsinda mwenziwe hatufikishwi mbali tunazungulushwa humu humu mjini.
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kama unataka kuniambia Raza kwa hili si mfano mzuri.

  Amekuwa kwenye mambo ya Taifa kwa muda wote naye ni muhindi

  Hakuwahi kuomba nafasi ya Chama ili kuendesha biashara na pia kauli yake ya kupinga kujinufaisha ukiwa kiongozi zinanifanya nihisi kuwa unaweza kujinufaisha bila kutumia cheo.

  Ama la kufilisika hilo si juwi pengine wewe Kibunango na visa vya Zenji utakuwa unajuwa.
   
 16. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hebu nieleze Mzee.
   
 17. G

  Gozigumu JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwiba,

  Baniani mbaya kiatu chake dawa!

  Alichozungumza ni facts, ukabila na kutumia madaraka kujinufaisha. Ama hili la ukabila kwa upande wako naona kama unapotoka. Naona una Muhindi kule CUF anaitwa Jussa sasa huyo nae hamumuamini?
  Usimlenge mawe mwendawazimu.............!
   
Loading...