Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
BAADA kuwa katika mahusiano kwa muda mrefu nyota wawili katika tasnia ya filamu Bongo Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hansy , Chuchu anafunguka kwa kusema kuwa mpenzi wake huyo yupo mbioni kubadili dini na kumfuata yeye kwani tayari anafunga naye mwezi huu mtukufu.
“Ray ananisupport kufunga mwezi huu yupo sambamba nami kufuata taratibu za kidini hivyo Inshallah tukijali siku si nyingi atabadili dini na kufunga ndoa lazima anifuate mimi,” anasema Chuchu Hansy
Chuchu aliyasema hayo akiongelea filamu yake mpya anayotarajia kuingiza sokoni ya Usiku wa Daku ikiwa ni sinema ya Kidini akiwa ameitengeneza kwa kusaidiwa na Ray sinema hiyo imemshirikisha Hemed Suleiman na wasanii wengine.
Source: Bongo Movie