Ray C amtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar, amshukuru kwa msaada wa matibabu!

Duh bwana mkubwa nae kwa kupenda uma-harufu hajambo,yaani mateja woote wa nchi hii kamuona "kiuno bila mfupa" tu?,kama ni muungwana kiasi hicho si angefungua rehabilitation centre ili mateja wote wanufaike.

MKUU, na mimi ndo swali nimebakia nalo. Kumsaidia Ray c sawa kafanya vizuri, Je mateja wengine wao hawahitaji msaada wake pia. Kwa nini basi asifungue centre ya kuwsaidia hawa waadhirika ikiwa ni pamoja na kuzuia na kuwachukulia hatua wote wanaoingiza hayo madawa?
 
Unachezea JK wewe! Inawezekana ni nani hii wake.
 
Kilichoniacha mdomo wazi katika tukio hilo ni jinsi JK alivyokuwa anatabasamu wakati anafagiliwa na Ray.
Hakika lile tabasamu la mkuu wa nchi ni nadra, sielewi aliguswa na nini hadi kuwa na furaha ya aina ile.
Hongera JK kwa tabasamu mwanana.
 
JK agharimia matibabu ya Ray C. Sikujua kuwa jamaa ni mbaguzi kiasi hiki? Source TBC1 habari saa 2
 
Nadhani rais anatakiwa kupewa sifa kwa hili japokuwa najua Ray C kachukuliwa kisiasa zaidi.
 
Okay ahsante jei kei kwa hili. Ray c pole sana mamie,tunakupenda uendee na matibabu upone kabisa.
 
NA WALE WENGINE WANAOJAZANA VITUO VYA MAGARI WATIBIWE NA NANI!
HUU UMAARUFU BEI RAHISI HUU!UNAZIDI KUKUCHAFUA KULIKO KUKUJENGA !
wasio na majina wanatibiwa nani?
 
Thanx mr president kwa niaba ya wote walioguswa na tatizo la RAY C niko chini ya mwembe naburudika na hits kali za Ray 2 the C
pona haraka uje uwabambe !get well sooner RAY C
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…