Rais wangu JK kwa mara nyingine sikuungi mkono katika suala hili. Ningekuona umefanya la maana kama ungetengeneza mifumo ya kudhibiti uingizwaji, usambazaji na matumizi ya mihadarati. Kumtibu muathirika tungechangishana wenyewe kama tunavyofanya kwa wagonjwa wetu wengine waliopo mahospitalini na majumbani mwetu.
Wewe tungekushukuru sana kama ungetuwekea mifumo ya kuhakikisha huu uchafu hauingii nchini na ma don wa madawa ya kulevya wote wanafikishwa mahakamani na sheria inachukua mkondo wake.
Hivi Rais wangu utajisikiaje ukisikia kwamba wale watu uliopewa majina kuwa ndio vinara wa kuingiza na kuuza madawa ya kulevya ndio hao wamemuuzia Ray C hizo cocaine?