RAV 4 Yateketea kwa moto Salender Bridge

RAV 4 Yateketea kwa moto Salender Bridge

Captain Phillip

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
894
Reaction score
538
Wadau,

Mida hii niko mishemishe yangu mitaa hii ya Salender Bridge mbele ya Ubalozi wa Urusi nimeshuhudia Rav 4 Nyeupe ''Kilitime'' inateketea mwanzo mwisho naamini hakuna kitu alichoweza kuokoa huyo aliyekuwa akiendesha.Fire wamekuja wakati moto umeshazimika wenyewe.Dereva wakati anashuka ameonekana kuchanganyikiwa kwani hata ile akili ya kwenda ku-disconnect battery hakupata.

Hapo nikapata wazo jinsi ambavyo huwa tunatozwa hele ya Fire tunapoenda kukata Road Licence matokeo yake tunaishia kuhonga Ma-traffic tunapokuwa hakuna nyenzo za kuzimia moto.Badili tabia.
 
Asante kwa taarifa. Weka Picha itakuwa poa zaidi.
 
Pengine ni tego hilo la bima! biashara ya bima ngumu sana! labda life assurance lakini hizi za magari hatari tupu!
 
Mara nyingi watu huunguza magari sehemu maarufu zenye watu wengi kama evidence wakati wa kudai bima!
 
hapo salender bridge si kuna mtu aliota manyoya naona vioja vinaendelea!
 
Wadau,

Mida hii niko mishemishe yangu mitaa hii ya Salender Bridge mbele ya Ubalozi wa Urusi nimeshuhudia Rav 4 Nyeupe ''Kilitime'' inateketea mwanzo mwisho naamini hakuna kitu alichoweza kuokoa huyo aliyekuwa akiendesha.Fire wamekuja wakati moto umeshazimika wenyewe.Dereva wakati anashuka ameonekana kuchanganyikiwa kwani hata ile akili ya kwenda ku-disconnect battery hakupata.

Hapo nikapata wazo jinsi ambavyo huwa tunatozwa hele ya Fire tunapoenda kukata Road Licence matokeo yake tunaishia kuhonga Ma-traffic tunapokuwa hakuna nyenzo za kuzimia moto.Badili tabia.

...ni mojawapo ya aina ya magari yanayotakiwa kurudishwa JAPANA!

"HITILAFU MAGARI YA TOYOTA: Magari
milioni 6.6 aina ya Yaris, Urban
Cruiser, RAV4, Hilux kurudishwa
kiwandani kutokana na hitilafu,
kampuni ya Toyota yasema leo."
 
kuna ambayo nimeikutaa inaunguaa ya kijvuu leo mida ya saa saba kasoro...ndoo yenyewee???
 
Gari ikishika moto vile vi fire extinguisher havizimi moto
 
...ni mojawapo ya aina ya magari yanayotakiwa kurudishwa JAPANA!

"HITILAFU MAGARI YA TOYOTA: Magari
milioni 6.6 aina ya Yaris, Urban
Cruiser, RAV4, Hilux kurudishwa
kiwandani kutokana na hitilafu,
kampuni ya Toyota yasema leo."

Source .....
 
Back
Top Bottom