Ratiba ya Utoaji heshima za Mwisho na kuaga mwili wa Alfonce Mawazo

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,493
54,900
Ratiba ya shughuli ya utoaji heshima za mwisho na mazishi ya Kamanda Mawazo Alphonce Mawazo

Kesho Siku ya Ijumaa Novemba 27 saa 2 asubuhi, mwili wa Mpiganaji na Kiongozi wetu Alphonce Mawazo utachukuliwa Hospitali ya Bugando kuelekea nyumbani kwa Baba yake mdogo, eneo la Nyegezi-Swea kwa ajili heshima za familia kabla ya kuelekea Viwanja vya Furahisha ambapo Viongozi waandamizi wa UKAWA, wakiongozwa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, Mgombea Urais Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, wabunge wa UKAWA, wataongoza maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wao Mawazo.

Baada ya Viwanja vya Furahisha, mwili wa Mpiganaji Mawazo utasafirishwa kuelekea Geita kwa ajili ya kuwapatia nafasi wakazi wa Mkoa wa Geita kumuaga Kiongozi wao siku ya Jumamosi, Novemba 28 kuanzia asubuhi mapema ambapo baadae mchana mwili huo utapelekwa Mji Mdogo wa Katoro, mkoani Geita, ambapo pia wananchi watapata fursa ya kumpatia heshima za mwisho na kumuaga Mawazo ambaye alikuwa ni Mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo la Busanda.

Baada ya wakazi wa Katoro kushiriki tukio hilo, mwili wa Kamanda Mawazo utapelekwa nyumbani kwao kijijini Chikobe tayari kumhifadhi kwenye nyumba ya milele shambani kwake, siku a Jumapili, Novemba 29, baada ya familia, ndugu, jamaa na wakazi wa kijiji hicho kutoa heshima zao za mwisho.

Makene

============

Updates;

Tumaini Makene said:
Kutokana na sababu ambazo ziko nje ya uwezo tumelazimika kuwa na mabadiliko kidogo kuhusu utaratibu a ratiba nzima ya utoaji wa heshima za mwisho kumuaga Kamanda Alphonce Mawazo na hatimaye mazishi yake, tofauti na tulivyotangaza jana jioni baada tu ya hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Leo Ijumaa Novemba 27, saa 5 asubuhi, kupitia mkutano na vyombo vya habari, utakaofanyika jijini Mwanza, viongozi wakuu watazungumza na waandishi wa habari na kutoa utaratibu mzima na ratiba mpya ya shughuli hiyo ya kumuaga na kumzika Mawazo.

Chombo chako kinakaribishwa katika mkutano huo, leo saa 5 asubuhi hapa jijini Mwanza.

Makene
 
Pumzika kwa amani kamanda wetu Mawazo damu yako italeta ukombozi .
Poleni sana wafiwa wote
Hakuna giza linashinda nuru.
 
So sad! Pumzika kwa amani kamanda na rafiki yangu Mawazo
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.

Uwezo wa kufikiri ndo umeishia hapo.
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.

Wewe ndo ulihusika nini? Lazima albadri isomwe kuwalaani wauwaji, hakika hawataishi kwa amani hapa duniani, watakuwa wa kuweweseka, mizuka na majini yatawandama na ukoo wao. Allah sema na hawa wauwaji...
 
Ageni mwili wake kwa amani, hatutaki fujo hapa mjini. Na hao vingozi wenu muwaambie kuwa uchaguzi umeisha, lowassa peke yake aruhusiwe kuhutubia maana hawezi chukua zaidi ya dakika tano kuongea.

majebere;
Naamini weye umeshajilaani mwenyewe hivyo hata tukikulaani tunapoteza nguvu bure. Pamoja na hayo unayodhani unayafaidi kwa maneno yako hayo, lakini naamini wewe utakufa vibaya kuliko huyo Mawazo uliye muua. Hata maiti yako haitaonekana iagwe. Pole sana
 
Back
Top Bottom