Ratiba ya mgao wa umeme Tz

Ratiba ya mgao wa umeme Tz

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
9,710
Reaction score
2,251
Ivi hawa tanesco hawahwezi wakawa wanagawa umeme mchana kwa maeneo ya viwanda alafu kwenye makazi ya watu wanaleta usiku mpaka asubuhi!

Ingawa tatizo litakuja mpangilio wa miji yetu unakuta watu na viwanda pamoja. Ila in some places inawezekana let's do it.

Ni ushauri tuu
 
Mkuu Njowepo si ajabu hata katika huu mgao wa umeme kuna rushwa inafanya kazi hivyo sia ajabu kuna upendeleo fulani na hivyo sehemu fulani fulani zinapata umeme zaidi kuliko nyingine.

Kama Wabunge wanaweza kuchukua rushwa ili kupitisha uozo wa Nishati, hivyo si ajabu wahusika wa karibu na mgao ndani ya TANESCO pia nao wanatajirika na hivyo kutoa upendeleo fulani katika mgao.
 
Mkuu wala hatuna haja ya kudiscuss... ratiba ya mgao ni kudhalilishana especially after 50years of independence!!!!

Yani haina maelezo yoyote yatakayojustify mgao wa umeme mwana 2011, hakuna......... period!!
 
nenda kigamboni umeme unakatika hadi unasahau lini uliwaka..kama juzi j5 ulikatika toka j4 hadi jana ndo ulirudi halafu asubuhi ukakatika..
 
Mkuu wala hatuna haja ya kudiscuss... ratiba ya mgao ni kudhalilishana especially after 50years of independence!!!!Yani haina maelezo yoyote yatakayojustify mgao wa umeme mwana 2011, hakuna......... period!!
MTM, kweli hakuna justification, lakini ukweli ndo huu, mgao upo.Inakera sana kwa kweli, asbh nimeondoka kwangu hakuna umeme, ofisini nimefika hakuna umeme na nimetoka hali kadhalika. Nimerudi nyumbani giza! It is very stressful!Happy 50th Independence Aniv. Tanzanians!
 
Yaani mdau umeme uliopo sasa labda kwa matumiz ya kawaida sana,na sidhan kama utafika september,,,,,,,TANESCO wenyewe wamekiri kupitia msemaj wao
Ivi hawa tanesco hawahwezi wakawa wanagawa umeme mchana kwa maeneo ya viwanda alafu kwenye makazi ya watu wanaleta usiku mpaka asbi!Ingawa tatizo litakuja mpangilio wa miji yetu unakuta watu na viwanda pamoja.Ila in some places inawezekana let's do itNi ushauri tuu
 
ivi hawa tanesco hawahwezi wakawa wanagawa umeme mchana kwa maeneo ya viwanda alafu kwenye makazi ya watu wanaleta usiku mpaka asbi!
Ingawa tatizo litakuja mpangilio wa miji yetu unakuta watu na viwanda pamoja.
Ila in some places inawezekana let's do it
ni ushauri tuu

yaani hata kwenye mgawo napo tunaanza kushauri??..issue inatakiwa iwe kwa nini mgawo..tukianza kubargain mgawo tunakimbia mada..
 
Ivi hawa tanesco hawahwezi wakawa wanagawa umeme mchana kwa maeneo ya viwanda alafu kwenye makazi ya watu wanaleta usiku mpaka asbi!
Ingawa tatizo litakuja mpangilio wa miji yetu unakuta watu na viwanda pamoja.
Ila in some places inawezekana let's do it
Ni ushauri tuu


Kwanza wewe ulichangia milioni 50 wewe ya kupitisha bajeti? watapata waliochangia tu kaka
 
Kwanza wewe ulichangia milioni 50 wewe ya kupitisha bajeti? watapata waliochangia tu kaka
Khaa! yaani ww ndo umekomelea msumari wa moto kwenye kidonda eeh?
 
Mkuu inakera unatoka ofisini giza unarudi home giza sasa unajiuliza hawa watu hawajui industrial vs domestic consumption balance?
Ngoja nasi tuwachangie iyo 50mil labda watabalance mambo.
Ila ukiwa line moja na either hospital au viongozi kama rc na wengineo unapeta. Ndo maana viongozi wengi mgao wanausikia kwa wananchi wa kawaida usikute ata hawajui kuwa kuna mpaka ratiba.
 
*Yasema hali tete, ratiba ya mgawo yatupwa

Na Benjamin Masese

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kuwa hali ya mgawo wa umeme nchini kwa sasa ni tete kutokana na uzalishaji wa nishati hiyo kuzidi kupungua
na kufikia hatua za mwisho za kuzimwa kwa mitambo.

Vile vile limesema kwamba halitaweza kufuata ratiba iliyotolewa awali ya mgawo wa umeme na hivyo kuwataka wananchi kukubaliana na hali iliyopo sasa hadi serikali itakapofanikisha mipango yake kuhusu suala hilo.

Hayo yalisemwa na Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud wakati wa mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu kuhusu kutofuatwa kwa ratiba ya mgawo wa umeme iliyotolewa awali ambayo imesababisha malalamiko kwa wananchi.

Bi. Masoud alisema kuwa ratiba hiyo imeshindikana kufuatwa kutokana na kiwango kidogo cha umeme kinachozalishwa ambacho kwa muda mwingine kipanda na kushuka, hivyo kuwapa wakati mgumu wa kuwahudumia wateja wake.

Alisema kuwa hakuna njia mbadala ya kuepusha tatizo hilo, kwa kuwa tayari limeshakuwa kubwa.

Kinachotakiwa sasa, alisema ni uvumilivu na subira wakati serikali ikiwa katika mchakato wa kuepusha nchi isiingie katika giza.

"...kwa hilo ni kweli hatuwezi kufuata ratiba tuliyoitoa awali kwa sababu ya kiwango cha uzalishaji kupungua kila wakati, yaani kinapanda na kushuka...sasa ukisema unafuata ratiba utasababisha migogoro, naomba wananchi watambue kwamba hali ni tete na tukubaliane na hali hii," alisema.

Hivi karibuni, vyombo vya habari vilisema makali ya mgawo wa umeme yameongezeka kutoka saa nane hadi 18 kwa siku katika mikoa mbalimbali ikiwemo Tabora, Kilimanjaro, Arusha na Dar es Salaam.
 
Na hali iendelee hivi hivi mpaka 2015....labda ndio wabongo watatia akili kuuza kura zao kwa t-shirt na khanga!!
 
Na hali iendelee hivi hivi mpaka 2015....labda ndio wabongo watatia akili kuuza kura zao kwa t-shirt na khanga!!

Kwa sasa tu wameisha jua nini cha kufanya hata wakiambiwa uchaguzi ni kesho wanachagua chama kingine na sio CCM na wakichagua CCM basi Mtu huyo aliyesimamishwa anakubalika na wananchi. Mwezi ujao ndio kuta kuwa na kile kinaitwa mgao halali na sio huu
 
safi sana JK, endelea ku2pa raha wtz kwa mgao wa umeme.
 
Nchi isiingie gizani mara ngapi? huyo mwandishi sijamuelewa au anamaanisha kuwa tukose hata mishumaa?maana mafuta taa ya vibatari tayari tumeshayakosa..................maskini Tanzania
 
Jahazi la kikwete linazidi kudidimia..kazi ipo 2015 tutafika kweli!
 
TANESCO wawe wa kweli tu..NCHI IKO GIZANI...yaan hapa kuanza porojo ni kutafuta pa kutokea tu...Tuzime kila k2..mayb JK ndio atatuli magogoni.
 
Back
Top Bottom