Ratiba ya masomo ya sheria Tanzania Law School 'inawatenga wanafunzi wa OUT' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ratiba ya masomo ya sheria Tanzania Law School 'inawatenga wanafunzi wa OUT'

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Magobe T, Jul 12, 2011.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana JF, nimekuwa nilkisikia wanafunzi wa sheria wa Tanzania Law School wakisema wana ratiba tight kuanzia asubuhi hadi mchana. Kwa upande wangu, naona utaratibu huu unawanyima nafasi ya kusoma wanafunzi wa sheria wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania (Open University of Tanzania - OUT) kwa vile wengi wao ni wafanyakazi na wangetaka pia kupata nafasi ya kusoma Law School ili wale wanaotaka waweze kuwa mawakili pia.

  Nasema haya kwa sababu si rahisi kwa hapa Tanzania, mfanyakazi aombe likizo isiyo ya malipo miezi tisa na ajilipie ada ya chuo na mahitaji mengine ya kila siku bila kuwa kwenye ajira. Na pia sina hakika kama kuna kampuni yoyote inayoweza kukubali kumlipa mshahara mfanyakazi asiyekazini kwa muda wa miezi 9 ili asome!

  Kwa nini kusiwepo utaratibu wa masomo ya jioni kuanzia mfano saa 11 hadi saa 4 usiku kulingana na mahitaji ili wale wanafunzi wa OUT nao wapate nafasi ya kwenda kwenye mafunzo ya vitendo baada ya saa zao za kazi? Au Law School ina nia ya kuwanyima wanafunzi wa sheria wa OUT wasiwe mawakili kwa vile wao watashindwa kuhudhuria hayo masomo ya vitendo muda wa asubuhi hadi mchana na hakuna njia mbadala? Naomba maoni yenu.
   
 2. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ulishawahi kuwasiliana na uongozi wa tls na walikujibu nini? Usikimbilie kulalamika pambana ukishindwa omba kuongezewa nguvu ya mapambano teh teh
   
 3. m

  mwananyiha JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani hapa suala zima ni kuangalia ni namna gani utaratibu uwekwe ili kuaccomodate watu waliopo kwenye ajira. Si suala la OUT kwani kuna ambao wanakuwa wamesoma conventional university na wanapata ajira muda mfupi kabla ya kujiunga na law school na wengine wanasoma OUT lakini hawana ajira. Hivyo ni kuungana kwa pamoja kuweka mfumo ambao utawezesha watu waliopo kwenye ajira zilizo rasmi na zisizo kuweza kupata nafasi ya masomo ya jioni.
   
Loading...