Elections 2010 Ratiba ya kampeni CHADEMA 2010

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Pata ratiba nzima ya kampeni za CHADEMA fuatilia kwenye attachment hii hapa chini
 
Attachments

  • Ratiba ya kampeni Chadema.pdf
    36.8 KB · Views: 279
Hii RATIBA ina makosa. Waambie wasahihishe haraka sana. SIKONGE haipo kwenye RATIBA.

Dr Slaa uliahidi kufika SIKONGE. Hata kama hutapata kura za Wanyamwezi wenzangu, tafadhali UJE.

Inawezekana hatupo wengi, tafadhali ufike huko pia kwani sisi pia ni Watanzania.

Marais wote wamekuwa na tabia ya kuitembelea Sikonge kwenye kampeni tu.........

Usije na wewe ukafika Magogoni na ukatusahau Sikonge na sisi tukabaki na umbumbu wetu milele na milele

Wee Njoo tu hata kama kwa saa moja ukiwa juu ya Helcopiter. Unaweza kuamsha roho kadhaa zilizokata tamaa.
 
Kuna team mbili ya magombea urais na ya mgombea mwenza. Inaonyesha Slaa ataenda Zanzibar mara moja tu na kumwachia mgombea mwenza kuendelea huko. Ukiiangalia sana ratiba ime concentrate Kanda ya ziwa ataenda mara mbili Mbeya yaani nyanda za juu atarudi huko maeneo ya Dodoma hasa Singida mara mbilimbili. Maeneo ambayo hayajapewa umuhimu zaidi ukiacha Unguja na Pemba ni ya Kusini ambayo yatatembelewa na mgombea mwenza.
 
Hii RATIBA ina makosa. Waambie wasahihishe haraka sana. SIKONGE haipo kwenye RATIBA.

Dr Slaa uliahidi kufika SIKONGE. Hata kama hutapata kura za Wanyamwezi wenzangu, tafadhali UJE.

Inawezekana hatupo wengi, tafadhali ufike huko pia kwani sisi pia ni Watanzania.

Marais wote wamekuwa na tabia ya kuitembelea Sikonge kwenye kampeni tu.........

Usije na wewe ukafika Magogoni na ukatusahau Sikonge na sisi tukabaki na umbumbu wetu milele na milele

Wee Njoo tu hata kama kwa saa moja ukiwa juu ya Helcopiter. Unaweza kuamsha roho kadhaa zilizokata tamaa.
Angalia vizuri Sikonge ipo tena atarudi Tabora mara mbili na mgombea mwenza atafika huko.
 
SIKONGE haipo Mkuu. Hii imenihuzunisha sana.

Nilimuomba aje na Oparation Sangara hadi Sikonge na akaahidi atafika.

Nafahamu kuwa CCM imejichimbia Mizizi Sikonge na kushinda ni ndoto kwani Umasikini umewamaliza kabisa Wanyamwezi wangu. Wakipewa Pilau na Khanga wao wanagawa kura tu bila kujali kesho. Inabidi hatimaye mtu aje awaambie WABADILIKE. Ona wamemuacha mgombea ubunge safi kabisa na kumuweka Mwalimu wa shule ya Msingi Juma Nkumba, ovyo kabisaaa.

Sasa sisi inabidi tusaidiwe zaidi maana ndiyo kwanza tuko usiku wa nane.

Angalia vizuri Sikonge ipo tena atarudi Tabora mara mbili na mgombea mwenza atafika huko.
 
SIKONGE haipo Mkuu. Hii imenihuzunisha sana.
Nimeangalia hata kwa Bwana Mapesa Bariadi haendi kamwachia mgombea mwenza, labda wana maana yao kutokwenda sehemu hizo kwa sababu huwezi kufika kila sehemu. Hebu angalia hizi sehemu hazijumuishi Sikonge.

10-Oct J. Pili TABORA
Kaliua
Urambo Mjini
Usoke
Tabora Mjini

16-09-10 Alhamis TABORA Igunga
17-09-10 Ijumaa Tabora Kaskazini
18-09-10 J. Mosi Igalula
19-09-10 J. Pili Bukene

Sikonge sina hakika vizuri na machanganuo wa ratiba hii lakini nadhani viongozi wa mkoa wa Tabora wanaweza kumpangia ratiba za kutembelea huko. Zungumza nao. Hata mimi natamani angetembelea kule kijijini kwetu ili wamuone Prezidaa wetu mpya kabla ya kumuwekea tiki lakini sijui kama itawezekana. Linchi hili ni likubwa kweli.
 
Na bila shaka kutakuwa na mabadiliko kufuatiana na hali ya kampeni itakavyokwenda.

Lazima tukubali hawezi kufika kila mahali.
 
Nakubaliana kuwa hawezi kufika kila mahali. Ila walau kwenye WILAYA basi afike.

Nikisema aje Kijijini kwetu hapo itakuwa kweli inaleta mushkeli. Ila akifika walau Sikonge mjini basi kuna watu wengi tu watakuja kumuona na kumsikiliza Rais mtarajiwa. Akiwapa hope kuwa mambo yatakuwa mazuri wamchague na wasiendelee kusikiliza ahadi zilezile miaka nenda miaka rudi. Awaambie wenzao wanavyoendelea na wao wako nyuma saaana.

I hope watabadili ratiba ili walau aende kwa walau nusu saa. Helcopiter inaweza kwenda kwa muda mfupi na akakutana na wananchi na akiondoka hapo anaendelea na msafara wake majimbo mengine. La muhimu ni kuwa alifika na kuwaona Wa-Sikonge wakoje kabla hajawa Rais hapo Mwakani.
 
Mkuu wenzio atafika mpaka Matryazo-kalinzi-Kigoma, tehe tehe tehe

Fanya ka-advocacy kidogo mkuu

btn: Urais sio mwakani, ni mwaka huu huu
 
Back
Top Bottom