Kamanda Francis
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 834
- 140
Wakuu, Mimi Gamba Sugu, naamini katika uwazi na uwajibikaji ndani ya Taasisi mbalimbali kama vile vyama vya Siasa na hata Serikali kwa ujumla.
Nasema haya kwa sababu, Serikali hii ya magamba wenzangu, Inaendelea kueneza upotoshaji wa wazi tena bila aibu. "Rasmu ya Katiba iliyowasilishwa Dodoma na Tume ya Warioba ndio muswada ulioandaliwa na Serikali hii hii ya CCM na ndio wenye misingi mikuu ya Katiba yetu tuitakayo huku uraiani.
Tunaposema misingi mikuu, hapa tunamaanisha Muundo wa Muungano wenye Shirikisho la Serikali tatu, kamwe huwezi kuuondoa muundo huu, na kama unauondoa, Inamaana una dhumuni la kuifumua Rasmu nzima, kitu ambacho unalenga kukomba kodi za wanyonge kwa mara ya pili.
Wananchi tuliopo nje tunasema, kama maoni yetu yaliyomo kwenye Tume ya Warioba hayatapewa kipaumbele huko Dodoma, ni bora mwezi August msirudi huko Dodoma kuharibu kodi zetu bure, ambazo zingechimba visima vya maji, kununua madawati ama vitanda kwenye Zanahati huku vijijini maana tunaseka mahali pa kujifungulia.