RASMI - UEFA yaondoa sheria ya goli la ugenini

Hii sijaipata fresh,

Ina maanisha Simba akienda Zambia kucheza na Nkana, tukapigwa 2-1

Inatakiwa ashinde goli ngapi kwa mkapa ili asonge mbele?
Watakuwa wanaangalia aggregate tu. Kama aggregate itakuwa wanalingana wanaongeza dakika 30 kisha penati.
Mfano Simba kafungwa 2-1 basi anatakiwa ashinde 2 kwa bila hivyo aggregate itasoma Simba 3 Nkana 2. Ila ikitokea Simba kashinda goli moja tu kwa bila hapo aggregate itakuwa ni Simba 2 nkana 2 hivyo dakika zitaongezwa. Simba akishinda 3 kwa 2 aggregate itakuwa Simba 4 na nkana 4 hapo dakika zitaongezwa.

N.B hii ni kwa UEFA tu CAF bado hawasema Kama wamebadili sheria la goli la ugenini hivyo Simba na nkana nimetumia kama mfano kukuelewesha
 
Hiyo sheria ilikua ya ovyo na wamecheleea kuiondoa.Kule america kusini wenye mpira wao hakuna mambo kama hayo kule ni kazi kazi mwanzo mwisho.Ngoja tuone kama na Caf wataliona hili.
 
Habari ndio hiyo, sasa kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.

Sheria hiyo iliyoanzishwa mwaka 1965 itaondolewa kuanzia msimu ujao kwenye mashindano ya UEFA ikiwemo Champions League.

Sheria hiyo iliyokuwa inaibeba timu iliyofunga magoli mengi ugenini imekuwa ikitumiwa kwenye mashindano yote ya UEFA ngazi za vilabu kuanzia Europa League na Champions League.

Rais wa UEFA Alexander Ceferin amenukukiwa akisema; sio sahihi tena kwa goli la ugenini kuwa na uzito wa ziada.

Natumai Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) nalo litafuata mfano wa UEFA kuondoa hiyo sheria iliyopitwa na wakati.

- Ushindi mechi tano wakukumbukwa zaidi wa sheria ya goli la ugenini, ligi ya mabingwa Ulaya.

1. May 2019: Ajax 2 - Tottenham 3 (Agg. 3-3), Tottenham wakapita kwa goli la ugenini.

2. Apr. 2019: Man City 4 - Tottenham 3 (Agg. 4-4), Tottenham wakapita kwa goli la ugenini.

3. March 2019: PSG 1- Man Utd 3 (Agg. 3-3) Man utd wakapita kwa goli la ugenini.

4. April 2018: Roma 3- Barca 0 (Agg. 4-4) Roma wakapita kwa goli la ugenini.

5. May 2009: Chelsea 1 - Barca 1 (Agg. 1-1) Barca wakapita kwa goli la ugenini.
Hii ya Chelsea vs Barca ni unforgettable aise ..dah! Iniesta alitufanyia kitu mbaya sana.
 
Hii ya Chelsea vs Barca ni unforgettable aise ..dah! Iniesta alitufanyia kitu mbaya sana.

Mimi siishabikiii chelsea ila mechi nayo refa alifanya madudu mpaka michael balack akawa anamfuata refa anakimbia kufuata mpira aisee ile mechi drogba alitukana balaa.hakukuwa na VAR.ila ile mechi waliibiwa chelesea
 
Inabidi Simba ishinde 2 bila, kama ikishinda moja, aggregate inakuwa 2-2, hivyo watakwenda extra time au Penalty.
Hii sijaipata fresh,

Ina maanisha Simba akienda Zambia kucheza na Nkana, tukapigwa 2-1

Inatakiwa ashinde goli ngapi kwa mkapa ili asonge mbele
 
Mimi siishabikiii chelsea ila mechi nayo refa alifanya madudu mpaka michael balack akawa anamfuata refa anakimbia kufuata mpira aisee ile mechi drogba alitukana balaa.hakukuwa na VAR.ila ile mechi waliibiwa chelesea
Ile mechi Barca waliinunua kwa Uefa, ni kama CCM wanavyonunua ushindi kwenye uchaguzi kutoka tume ya uchaguzi.
 
Mpira wa miguu siyo rede chief. Ungekua unaangalia mpira ungejua kwanini offside ilikua introduced.
Jamaa ana point. Kama mipaka ya uwanja inajulikana na idadi ya wachezaji ni sawa, sasa iweje useme hutakiwi kufunga goli ukiwa umeotea . Mzembe hapo ni yule alietakiwa kunikaba maana idadi tuko sawa.
 
Jamaa ana point. Kama mipaka ya uwanja inajulikana na idadi ya wachezaji ni sawa, sasa iweje useme hutakiwi kufunga goli ukiwa umeotea . Mzembe hapo ni yule alietakiwa kunikaba maana idadi tuko sawa.
Bwana usinichekeshe bwana
 
No. Hiyo sheria imeondolewa mashindano ngazi ya vilabu Ulaya sio Afrika.
na Mlleta Mada denooJ utuwekee hiyo Link
wengine hatuamini mpaka tupapase wenyewe
ipo siku mtayaondoa na hayo ma miligoti kkuwsiwe na magoli hata ya ugenini
Mm naona bora yaendelee Vilabu km vya Misri ni wababe sana mkienda malizia kwao
 
Mimi siishabikiii chelsea ila mechi nayo refa alifanya madudu mpaka michael balack akawa anamfuata refa anakimbia kufuata mpira aisee ile mechi drogba alitukana balaa.hakukuwa na VAR.ila ile mechi waliibiwa chelesea
Yule Refa alikuwa ni shabiki wa man u na alishawekaga wazi enzi zake kuwa Chelsea ni timu iliyozaliwa 2004( imagine pale ilikuwa 2009) hivyo mechi yeyote ikichezwa vs Chelsea basi Kuna uwezekano Chelsea ikapoteza iyo mechi. Aliitwa Howard Web huyu jamaa mashabiki wa Chelsea hatutomsahau aise.
 
Hapana yule anaitwa Ovrebo
 
Back
Top Bottom