Rasimu ya Sera ya Gesi, Maoni yangu ya awali

Rasimu ya Sera ya Gesi, Maoni yangu ya awali

Ngoja tusome sera tujue kama tunaikataa ama lah.

Pili, sheria mpya ya gesi na mafuta inaletwa lini?
Na iliyopo ina mapungufu gani?

Je, inaathiri kutoa vitalu vya utafiti?
 
MAONI YA AWALI YA NDUGU ZITTO KABWE, MBUNGE KIGOMA KASKAZINI KUHUSU RASIMU YA SERA YA GESI ASILIA

Sera ni lazima ionyeshe kuwa katika ushindani wa soko makampuni ya mafuta na gesi asilia yatapata faida ya halali ( normal retuns) ya uwekezaji wao na kwamba lolote linalozidi litabakia kuwa mali ya wananchi wa Tanzania . Mkakati wa makampuni ya mafuta na gesi asilia ni kuhakikisha taifa linapata kiduchu na wanasaidia serikali kutoa majibu ya kipato hicho kiduchu. Watanzania hawatakubali tena.

7. Ni lazima tuseme kuwa tunataka utajiri wetu uwe neema kwa wananchi wetu, na siyo laana. Maendeleo yetu yatategemea ni namna gani tunafaidika na utajiri wetu wa maliasili kama gesi asilia. Sera ya Gesi Asilia itujengee imani hiyo. Hii Sera (Rasimu) inapaswa iangaliwe upya na hasa maeneo ya uwazi na uwajibikaji.

Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma kaskaziniTabora,
tarehe 18 Mei 2013.

Mkuu ZZK, hapo kwenye bold, huo sio uchochezi?, Unamaanisha nini unaposema Watanzania hawatakubali tena!, unamaanisha hao Watanzania wasipokubali ndio watafanya nini?!.Kwa maoni yangu, haya ni maneno ya uchochezi kutaka kuwafungua macho Watanzania ili wasikubali!.

Niwajuavyo Watanzania, Watanzania ni watu watiifu sana, watulivu sana, na wapole sana, kiasi kwanza tumeisha jizoelea kupelekwa pelekwa tuu, huku tukikubali kwa mioyo myeupe, ndio maana kila baada ya miaka 5, huwa tunakipa tena hiki chama chetu adhimu, ushindi wa kishindo, na 2015 tutakipa tena!.

Sisi Watanzania hivi ndivyo tulivyolelewa sisi ni watu wa"yes man!" kwa lolote liwe zuri au baya, sisi ni "YES!" tuu!, sasa hawa Mhe. Zitto unaowasemea kuwa hawatakubali, ni Watanzania wepi hao?!, usije ikawa ni hawa hawa wapole, watiifu na watulivu sasa mnataka kuwafungua macho sio ili waelewe na wasikubali, bali kuwachochea wasikubali kuendelea kupelekwa pelekwa!, swali langu kuu linabaki, hao wasipokubali, watafanya nini?.
Afadhali ya wenzetu wa pembezoni, wanapo kwa jirani!, sisi wengine ambao hatuna itakuwaje?
Pasco.
 
Mkuu Temba1, nakuwekea hapa sehemu ya rasimu inayohusiana na maswali yako, baada ya kutafakari tutaweza kujadili.

3.1.3 Management of Natural Gas Revenue

Issue: Managing revenue arising from natural gas with a view to benefit the present and future generations of Tanzanians.

Natural gas resource is a potential source of revenue to the Government. However, if not properly managed such resource is likely to be a curse instead of a blessing.

Since natural gas is a finite resource, it is crucial that the revenue is managed in a manner that will bring about lasting benefits and welfare to the Tanzanian society. Revenues from natural gas resource can be aligned with the national development vision by directing them into strategic investments such as infrastructure.

Successful management of this resource will require putting in place mechanisms of governance to mitigate spending pressure and preclude rent seeking opportunities; fiscal management to mitigate effects of revenue volatility due to changes in production levels or fluctuation of global oil and gas prices; and economic diversification and linkages with other sectors.

Natural Gas Revenue Fund will be established to ensure transparency and accountability over collection, allocation and management of the natural gas revenue. The fund will be structured to provide for stabilization of revenue transfer to the Government for public expenditure in strategic areas and for domestic savings for future investment. In addition, sound fiscal management of the natural gas revenue spending shall be in accordance with national development plans and strategies.

Objective: To ensure effective management of natural gas revenue to achieve the national development goals.

Policy Statements:
The Government shall:
(i) Establish Natural Gas Revenue Fund for development of natural gas industry and national strategic projects;
(ii) Ensure fiscal regime in the natural gas industry supports development of the industry; and
(iii) Ensure the local communities benefit from revenue emanating from the natural gas activities in their localities.
 
Mkuu Zitto matumizi ya hii lugha ya kimombo na uelewa wa wabunge wetu hautaleta uwezekano wa kukubali jambo wasilo lijua?

Napata shaka sana na uwezo wa wabunge wetu katika lugha, hii rasimu na mapungufu hayo uliyo jaribu kuyagusia inaweza ikapewa baraka na wabunge wetu bila kufanyiwa marekebisho yeyote.

Wito kwako na wabunge wote wenye uelewa, jitahidini kuwaelimisha wabunge wenzenu ili mfanye maamuzi sahihi ili raslimali hii ya gesi iweze kuleta matokeo mazuri itakapo anza kuvunwa kwa maslahi ya wananchi zaidi.

Lakini hapa napata fundisho, kiwango cha chini cha elimu bungeni kiwekwe maana dunia ya leo na mambo jinsi yanavyo fanywa, elimu ya darasa la 7 au kidato cha nne hazina nafasi kwenye maswala ya kimaamuzi hasa kwenye ngazi za majimbo mpaka taifa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ZZK, hapo kwenye bold, huo sio uchochezi?, Unamaanisha nini unaposema Watanzania hawatakubali tena!, unamaanisha hao Watanzania wasipokubali ndio watafanya nini?!.Kwa maoni yangu, haya ni maneno ya uchochezi kutaka kuwafungua macho Watanzania ili wasikubali!.

Niwajuavyo Watanzania, Watanzania ni watu watiifu sana, watulivu sana, na wapole sana, kiasi kwanza tumeisha jizoelea kupelekwa pelekwa tuu, huku tukikubali kwa mioyo myeupe, ndio maana kila baada ya miaka 5, huwa tunakipa tena hiki chama chetu adhimu, ushindi wa kishindo, na 2015 tutakipa tena!.

Sisi Watanzania hivi ndivyo tulivyolelewa sisi ni watu wa"yes man!" kwa lolote liwe zuri au baya, sisi ni "YES!" tuu!, sasa hawa Mhe. Zitto unaowasemea kuwa hawatakubali, ni Watanzania wepi hao?!, usije ikawa ni hawa hawa wapole, watiifu na watulivu sasa mnataka kuwafungua macho sio ili waelewe na wasikubali, bali kuwachochea wasikubali kuendelea kupelekwa pelekwa!, swali langu kuu linabaki, hao wasipokubali, watafanya nini?.
Afadhali ya wenzetu wa pembezoni, wanapo kwa jirani!, sisi wengine ambao hatuna itakuwaje?
Pasco.
Mkuu Pasco, neno uchochezi (KAMA ULIVYOLITUMIA HAPA) litatufanya tuwe taifa la watu waoga.

Kwangu mimi, iwapo serikali haitimizi wajibu wake vizuri, akitokea kiongozi anayesimamia UKWELI anaonekana mchochezi machoni pa walio madarakani. Kwa hiyo, neno hilo UCHOCHEZI linageuka kuwa ni neno la ulinzi dhidi ya hao ambao hawatimizi wajibu wao, kwani yeyote atakayekuwa tayari kusema ukweli atawachonganisha watawala na wananchi.

Kwa maoni yangu jambo lolote lililojikita katika UKWELI WA KUTETEA MASLAHI YA WANANCHI, haliwezi kuwa UCHOCHEZI. Na anayeliita neno la ukweli, linalofichua kutowajibika/kutotenda haki/kutotimiza wajibu, UCHOCHEZI anakuwa mpiga propaganda wa kunyamazisha ukweli na maslahi ya wananchi.

UCHOCHEZI wa kweli ni pale ambapo UKWELI unapindishwa ili kufanya watawala wachukiwe, japo wanafanya vema.
 
Mkuu Pasco, neno uchochezi (KAMA ULIVYOLITUMIA HAPA) litatufanya tuwe taifa la watu waoga.

Kwangu mimi, iwapo serikali haitimizi wajibu wake vizuri, akitokea kiongozi anayesimamia UKWELI anaonekana mchochezi machoni pa walio madarakani. Kwa hiyo, neno hilo UCHOCHEZI linageuka kuwa ni neno la ulinzi dhidi ya hao ambao hawatimizi wajibu wao, kwani yeyote atakayekuwa tayari kusema ukweli atawachonganisha watawala na wananchi.

Kwa maoni yangu jambo lolote lililojikita katika UKWELI WA KUTETEA MASLAHI YA WANANCHI, haliwezi kuwa UCHOCHEZI. Na anayeliita UCHOCHEZI anakuwa mpiga propaganda wa kunyamazisha ukweli na maslahi ya wananchi.

UCHOCHEZI wa kweli ni pale ambapo UKWELI unapindishwa ili kufanya watawala wachukiwe, japo wanafanya vema.

Which one has value between peace and the truth?

Muda mwingine inabidi ukweli ufichwe ili kulinda amani, mambo ya kuanika kila kitu kwa jamii kisa tu ukweli ufahamike unaweza kuleta madhara, wenda yasiwe ya moja kwa moja lakini yapo.
 
Mkuu Temba1, nakuwekea hapa sehemu ya rasimu inayohusiana na maswali yako, baada ya kutafakari tutaweza kujadili.

Mkuu nashukuru kwa kuiweka hii part hapa...
Lakini mbona ni introduction tu mkuu? Haijaonyesha methodology wa modality...
Binafsi I want to see numbers, I want to see percentages? Wanaposema to benefit local community, swali ni how? Kwa asilimia ngapi? na ya nini? Mapato? ajira? Uwekezaji? au kivipi... Who are the local community? Wanapoacha tu wazi hivi, mtu yeyote anaweza kuja na kufanya chochote jinsi anavyojisikia yeye, na kusema amewafaidisha local community... what is the dimension and scope of the benefit and the local community itself?

Hapo wanaposema wataanzisha National Gas revenue fund, wanatakiwa waonyeshe hii fund haitakiwi izidi au ipungue asilimia ngapi ya uwekezaji na mapato ya gesi. Mathalani wanaweza kuanzisha hiyo fund, ikapeleka billioni 100, wakati faida itakayopatikana ni billioni 30... hilo sio la ajabu Tanzania hii..

Pamoja na hayo, naomba kama kuna vipengele vinavyojibu maswali yangu mengine kama udhibiti wa serikali, kiwango cha uwekezaji kwa kutumia wawekezaji wa nje, ajira, nk utusaidie kuiweka hapa...

Asante...
 
Which one has value between peace and the truth?

Muda mwingine inabidi ukweli ufichwe ili kulinda amani, mambo ya kuanika kila kitu kwa jamii kisa tu ukweli ufahamike unaweza kuleta madhara, wenda yasiwe ya moja kwa moja lakini yapo.
Truth is not only more valuable, but it is the conditio sine qua non of lasting and true peace.

Amani ambayo inajengwa kwenye misingi ya UONGO, haidumu.

Historia ni shahidi wa hilo.
 
Mkuu Zitto, nimeipost rasimu yenyewe hapa, ili kusaidia wachangiaji wajue nini kimo kwenye rasimu.
Mtu wa Shamba, kama nimeelewa ni kwamba itakayojadiliwa na wabunge ni RASIMU ya 3, hii naona kama Rasimu ya Kwanza au? nimechanganya desa?
 
Which one has value between peace and the truth?

Muda mwingine inabidi ukweli ufichwe ili kulinda amani, mambo ya kuanika kila kitu kwa jamii kisa tu ukweli ufahamike unaweza kuleta madhara, wenda yasiwe ya moja kwa moja lakini yapo.
Mwana Lumumba mwenzako Chamviga umemsoma lakini, anajivua gamba wewe naona bado kwako baridi so umeng'ang'ana na koti
 
Mkuu Zitto matumizi ya hii lugha ya kimombo na uelewa wa wabunge wetu hautaleta uwezekano wa kukubali jambo wasilo lijua?

Napata shaka sana na uwezo wa wabunge wetu katika lugha, hii rasimu na mapungufu hayo uliyo jaribu kuyagusia inaweza ikapewa baraka na wabunge wetu bila kufanyiwa marekebisho yeyote.

Wito kwako na wabunge wote wenye uelewa, jitahidini kuwaelimisha wabunge wenzenu ili mfanye maamuzi sahihi ili raslimali hii ya gesi iweze kuleta matokeo mazuri itakapo anza kuvunwa kwa maslahi ya wananchi zaidi.

Lakini hapa napata fundisho, kiwango cha chini cha elimu bungeni kiwekwe maana dunia ya leo na mambo jinsi yanavyo fanywa, elimu ya darasa la 7 au kidato cha nne hazina nafasi kwenye maswala ya kimaamuzi hasa kwenye ngazi za majimbo mpaka taifa.

Pamoja na kwamba nakubaliana na wewe kuwa lugha inaweza kuwa tatizo, lakini ukweli ni kwamba ili hoja yoyote ipitishwe bungeni ni lazima iungwe mkono na wabunge walio wengi. Kwa bunge letu wabunge wengi ni wale wa CCM, sasa hawa wabunge wa CCM hata uwaandikie kwa lugha ya Kiswahili uchanganye na lugha zao za makibila haisaidii kitu sababu wao kila kitu kinacholetwa na serikali yao kazi ni kukubali tu.

Hata kusoma hawasomi. Nieleze mbunge gani wa CCM anaweza kusoma na akaja na hoja kama za Mh. ZZK kwenye uzi huu? jibu ni hakuna, lakini angalia vijana wa CDM watakavyoichambua sera hii.. utashangaa. Kule CCM hata vijana wanakuwa kama wazee vile.. Kama imefikia wabunge wanajibu hoja za wabunge wenzao kama Mawaziri unategemea nini hapo?
 
Mtu wa Shamba, kama nimeelewa ni kwamba itakayojadiliwa na wabunge ni RASIMU ya 3, hii naona kama Rasimu ya Kwanza au? nimechanganya desa?
Ok, mimi ninayo hii tu, na kwa mjadala inatoa picha. Mabadiliko katika rasimu ya 3 si makubwa.

Kama kuna mwingine anayo rasimu ya 3 atusaidie kutuwekea.
 
Mkuu, nimeipost rasimu yote (rasimu ya 1, si rasimu ya 3 waliyopewa wabunge).

Kwa kuwa ni ndefu nimeipost kwenye posts Namba 10,11,13-16. Ukiunganisha posts zote hizo sita utapata kitu kamili.
 
Kamanda ZZZK naunga mkono hoja. Serekali hii sijui imekuwaje maana sioni kwa nini tunakimbilia kuvuna rasilimali kwa haraka hivyo. Hawa wenzetu ni wajanja sana wao wanahifadhi za kwao kwa vizazi vijavyo ila wana waforce viongozi wa Africa kuvuna rasilimali kwa haraka mno hata pasipo uwelewa wa kutosha. Sasa hivi hawa watu wanatukopesha wakijua wazi tuna rasilimali na tutaweza kulipa. Itafikia mahali zitaisha unavikiri tutapata mikopo hiyo tena? Production na elimu ndo vimedidimizwa Tz tutakimbilia wapi? Vizazi vyetu vya baadae vitaishije? Watz tuamke hapa hakuna kulala!
 
Mambo muhimu kama haya tunaishia kujadilii tuu mwisho wa siku ujinga unapitishwa.

Mie naona pia malengo ya sera yapo too general
 
Questions that still need to be asked, We Tanzanian we must to look
where we are coming from, and where we will be our destination for
ower development. This our natural gas policy is present, a small
group of people, and not for all Tanzanians. The ministry need to form
a team that will write down the Law for the natural gas reasource.
No need to hurry, takes even two years time to do so, but we need to
work for the common good. For satisfactory for ower profit of Tanzania.
 
Back
Top Bottom