RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Muundo wa serikal 3 that means baada ya hii katba kuandikwa Tanzania bara inabid tuanze mchakato mwingine wa kuandika katba ya Tanzania bara kama zanzbar walivyo na katiba yao? Ebu niweken sawa hapa wanajamvi
 
Hiyo ni rasimu na yaweza kubaki hivyohivyo au yaweza kubadilishwa sana na yaweza kurudi kama ilivyokuwa awali yaani serikali mbili ya muungano na ya zanzibar.

Pamoja na yote lazima tuone mambo ya muungano ni yapi?
 
  • IDADI YA MAWAZIRI

Inapendekezwa Rais aunde Serikali ndogo iliyo na Mawaziri wasiozidi kumi na tano na mawaziri hao wasiwe wabunge. Mawaziri hawatahudhuria vikao vya Bunge isipokuwa kama watahitajika kutoa ufafanuzi kwenye kamati za Bunge.

Hapa tu mimi pamenikuna!
Pamekukuna wakati mambo yenyewe ni saba tu, na hayo mambo ya Tanganyika yatakuwa na mawaziri wangapi?
 
Hiyo ni rasimu na yaweza kubaki hivyohivyo au yaweza kubadilishwa sana na yaweza kurudi kama ilivyokuwa awali yaani serikali mbili ya muungano na ya zanzibar.

Pamoja na yote lazima tuone mambo ya muungano ni yapi?

Tatizo lenu hamsomi alama za nyakati kama ccm.Nyie ndiyo mnaweza hata kuhamasisha watu wachinjane sababu hamtaki mabadiliko.ina maana waliotoa maoni hadi kusababisha rasmi kuja kama ilivyosomwa ni MAMBURURA kama wewe??
 
Me sijaelewa kidogo!kwahiyo kutakuwa na rais wa tanganyika,rais wa zanzbar na rais wa tanzania?au inakuwaje?

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Marais watatu kisa kuwabembeleza wazanzibari, muungano ungepotelea mbali tu hatuuhitaji
 
Bado nadhani wachangiaji wengi ama kwa kutokuelewa ama kwa makusudi tunadhani mzigo umepungua. Mwl.Nyerere aliona hili ndiyo maana aka sacrifice Utanganyika ili kuipunguzia mzigo serikali.

Tunapojadili hii rasimu, tukumbuke hii ni kwa masuala ya muungano peke yake, lakini pia tukumbuke kwamba Tanganyika itakuwa na bunge lake kama ilivyo kwa zanzibar, na mawaziri wake, n rais wake na utitiri wote tunaouona leo kwenye muungano.

Wengi tunadhani hii katiba itatusaidia, lakini ukiangalia kwa kutulia,hili laserikali tatu likipitishwa, tujiandae na maumivu mengine huko mbeleni.

Tuisomeni kwa makini lakini pia tusisahau kwamba tunachokijadili ni katiba ya muungano na siyo ya Tanganyika au ya Zanzibar. tunapojadili ukubwa wa bunge au udogo, tujue hilo ni la Muungano na siyo la Tanganyika au la Zanzibar.

Warioba katutega, nasi tumetegeka kisawasawa.
 
Serikali za majimbo eti zitaleta utofauti mkubwa wa maendeleo, hivyo hazijapendekezwa ikiwemo gharama za uendeshaji.

Mbona mfumo uliyopo ndo umeleta utofauti mkubwa sana? Majimbo yawepo bhana yachuane kujipatia maendeleo. Tushuhudie watu wa kusini watakavyopiga kasi. Hapa tume ifikirie upya na wananchi tukomalie hoja hii ya majimbo.

Hoja ya majimbo ni ya kichadema sio kitaifa mkuu
 
Nashauri huku Tanganyika tuachane na urais, tuwe na waziri mkuu na atokane na uwiano wa kura/viti vya ubunge.
Mi naona hata waziri mkuu asiwepo....
tujaribu kwanza utawala binafsi tuone kama mambo yataenda
 
ARDHI wapiiiiiiiiiiiiiiiiii?

Tanzania inasheria kandamizi sana za ardhi

kisheria mwananchi hamiliki ardhi (bali anapewa kimkataba na serikali), na hili swala limesababisha serikali kunyanyasa watu kila wanapofanya uwekezaji, huwa watu wanaondolewa kwa nguvu bila kulipwa chochote.

Kukosekana kwa eneo linalozungumzia ardhi ambapo ndio kuna migogoro mingi sana kwa sasa, linanipa kuanza kuamini kwamba, business as usual kwenye swala hili.
 
Warioba kalikoroga kabisaa
sasa hili la Tanganyika ndo litazidi kuleta mapyaa kabisa..
 
Msisahau,muumgano huu ni watanganyika na zanzbr,hakuna tanzania bara hapo.
 
Kama ni serikali tatu basi Tanganyika irudi na si Tanzania Bara.Then tuanze mchakato wa Katiba ya Tanganyika
 
wana jf
kero yangu kubwa katika katiba iliyopita ilikuwa ni suala la mikataba kujadiliwa kienyeji na kutowekwa wazi na nilitaka katiba ijayo iweke utratibu wa moja kwa moja kujadili masuala ya mikataba kama vile:madini,biashara,uhusiano wa kimataifa n.k lakini hawajaweka sina imani kwani lengo kubwa la mimi kufikiri hivyo ilikuwa ni kulinda rasilimali za nchi

sijui wewe unasemaje
 
HIVI SASA, Ni matangazo ya moja kwa moja (live) kutoka ukumbi wa mikutano wa karimjee yakirushwa na TBC1. mgeni rasmi ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JAKAYA MRISHO KIKWETE... KATIBA MPYA KWA TANZANIA YENYE NEEMA

TUFUATILIE

Wakuu naomba ufafanuzi vipi ile mikataba iliyosainiwa na Serikali kwa yale masuala ambayo hayatakuwa ya Muungano kama madini. Na raslimali zingine.
 
1) Hapo kwenye Mawaziri mimi naona wangependekeza kabisa idadi ya Mawaziri, na siyo kusema wasisidi idadi fulani.
2) Kungeundwa wizara permanent, iyo kila rais anakuja na majina na idadi ya wizara kutegemea na idadi ya watu anaotaka kulipa fadhila kwao.
3) Wizara zote zinazohitaji kuwa na manaibu waziri ziwekwe wazi, na wapendekeze idadi yake, maana hapa tunaweza tukashitukia tuna mawaziri 15 na manaibu waziri 50, tutakuwa tumerudi kule kule
 
ni upuuuzi kuwa na mbunge mwanaume na mwanmke kila jimbo wakati huo kutakuwepo na bunge la tz bara.
 
Eti tume inapendekeza jambo hili liwe hivi hatakama wananchi wamependekeza hivi. Hiyo rasimu ya katiba ni maoni ya watz au wajumbe wa tume?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom