RASIMU ya Katiba Mpya Tanzania yazinduliwa

Kwaharaka haraka ninamashaka makubwa katika rasimu hii, maana mambo ya msingi yapo kimzahamzaha. jaji mkuu, Tume ya uchaguzi, chaguzi ndogo,nk

1. Jaji mkuu asiteuliwe na rais, aombe kazi na aajiliwe kama ajira zingine, kwasababu ndiye atakaye simamia haki endepo uchaguzi utakuwa na dosari, akiteuliwa atakosa mamlaka kamili na kutenda kwa kumfadhili aliyemteuwa.

2. kwanini kuwe na wabunge wawili akatika jimbo moja mwanaume na mwanamke hiyo gharama nani anagharamia na kwafaida ya nani?

3. kwanini nafasi ijazwe na chama husika badala yakuwa na uchaguzi? wananchi lazima wachaguwe kwa kuzingatia uwezo wa mbunge na chama kama sifa ya ziaada. Nafasi ya mgombea binafsi yanapotokea maafa iko wapi?

4. Tume ya uchaguzi lazima iwe huru, kwanini itajulikana na isijulikane sasa?
 
Umri wa urais ubaguzi mtupu! Halafu kazi nyingi kama wamezikwepa na kuziachia serikali shirikishi kitu ambacho kitaleta shida mbele ya safari ktk shirikisho letu!
Nina hofu pia ya kuwepo rasimu zilizochakachuliwa huko mtaani!
 
rasimu hii ya katiba ni nzuri ila naona imebezi zaidi kwenye mambo ya kisiasa haijazungumzia kwa undani mambo ya kijamii kama vile rasilimali mfano madini,mbuga za wanyama
 
Wanaj
yafuatayo ni baadhi ya maoni ya watanzania waliyotegemea kuyaona katika rasimu ya katiba mpya lakini giza;
  • kutambuliwa kwa kiswahili kama lugha ya taifa
  • mikataba yote kujadiliwa bungeni

ongeza na yako tuone
 
Haya changamkieni kuandaa katiba yenu ya Tanganyika huko ndio mleta ngonjera na usanii wenu sio katika katiba ya Tanzania, Jaji Warioba kawaonea huruma kama wajuzi rejesheni identity yenu, kwa ukilaza wenu najua mutaiita Tanzania Bara, so you will never have your identity mpaka dunia itakwisha.
 
Nimefurahishwa na mapendekezo ya:
MFUMO WA BUNGE
MADARAKA YA RAIS
TUME YA UCHAGUZI
MUUNGANO WA USHIRIKA (sijui kama ndio huo huo wa Maalim WA MKATABA?)
Tukiishajipatia Tanganyika yetu - tutaandika katiba nzuri zaidi.
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Baada ya kusoma kwa makini hii rasimu nimegundua ina mapungufu mengi sana kama ulivyosema. Kwanini mahakama isijitegemee? Kama tutakuwa na mahakama huru taifa letu litakuwa huru pia. Naona wamejitahidi kuzunguka kuzunguka ila naamini haya si maoni ya wananchi. Naona tume imechakachua mapendekezo ya raia.
Kwaharaka haraka ninamashaka makubwa katika rasimu hii, maana mambo ya msingi yapo kimzahamzaha. jaji mkuu, Tume ya uchaguzi, chaguzi ndogo,nk

1. Jaji mkuu asiteuliwe na rais, aombe kazi na aajiliwe kama ajira zingine, kwasababu ndiye atakaye simamia haki endepo uchaguzi utakuwa na dosari, akiteuliwa atakosa mamlaka kamili na kutenda kwa kumfadhili aliyemteuwa.

2. kwanini kuwe na wabunge wawili akatika jimbo moja mwanaume na mwanamke hiyo gharama nani anagharamia na kwafaida ya nani?

3. kwanini nafasi ijazwe na chama husika badala yakuwa na uchaguzi? wananchi lazima wachaguwe kwa kuzingatia uwezo wa mbunge na chama kama sifa ya ziaada. Nafasi ya mgombea binafsi yanapotokea maafa iko wapi?

4. Tume ya uchaguzi lazima iwe huru, kwanini itajulikana na isijulikane sasa?
 
1."Kamati ya uteuzi itapendekeza majina ya watu wanaofaa kwa Rais ambaye atateua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wengine. Bunge litathibitisha uteuzi wao. Wabunge na viongozi wa aina hiyo hawatakuwa na sifa za kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi."
2."Tume baada ya kupitia maoni ya Wananchi, inapendekeza Rais abaki na kinga kama ilivyo sasa na anaweza kushitakiwa na Bunge kama ilivyo Katiba ya sasa. "

Haya mambo mawili yanatakiwa kupitiwa upya!! tume sio huru na kumuachia rais kinga ni kumfanya asiwajibike!!

Kamati ya ureuzi itaundwa vipi? Kwa sababu kama wao ndo watakao pendekeza majina kwenda kwa raisi na kuwateua na bunge kuthibitisha...
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Baada ya kusoma kwa makini hii rasimu nimegundua ina mapungufu mengi sana kama ulivyosema. Kwanini mahakama isijitegemee? Kama tutakuwa na mahakama huru taifa letu litakuwa huru pia. Naona wamejitahidi kuzunguka kuzunguka ila naamini haya si maoni ya wananchi. Naona tume imechakachua mapendekezo ya raia.

Mkuu nashukuru kwamba umeliona hilo.

Ni kwakuwa na mahakama huru/ijetegemee kabisa, ndipo haki, uwajibikaji na heshima ya mtanzania itarejea.

Kwasasa bado tutayumba sana na mambo ya uteuzi na malipo kama fadhila kwa anayeteuwa.
 
Katika mkutano wake na waandishi wa Habari kuhusu uzinduzi wa Rasimu ya Katiba leo Tarehe 03 Juni, 2013, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alimalizia hotuba yake kwa kusema kuwa "Rasimu ya Katiba itapatikana kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya www.katiba.go.tz."

Nimejaribu kuingia kwenye tovuti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili niweze kujipatia nakala ya Rasimu hiyo lakini mpaka sasa sijafanikiwa kuiona. Wenzangu mmefanikiwa kupata nakala kwenye hiyo tovuti?

Nimeona baadhi ya watu wanatoa tathmini zao aidha kwa kusikiliza au kusoma hotuba ya Jaji Warioba ambayo ina kurasa kama 10 hivi. Lakini kwa mujibu wa Manyerere Jackton, Rasimu nzima ina kurasa 133 za A4.

Last edited by a moderator:
1.jaji mkuu why ateuliwe na rais hali ya kuwa yeye ndiye tunahitaji asimamie uhuru wa tume hiyo??

2.jimbo moja kuwe na wabunge wawili wa kke na kiume kwa logic ipi??

Bado inahitaji maoni mengine,kama watatoa nafasi inahitaji maboresha mengi sana....
 
Namba ya mawaziri na manaibu kudhibitiwa, pia mawaziri kuthibitishwa au kutothibitishwa na wabunge: kihama cha wachumia tumbo! Nakuaminia Mzee Sinde!
 
Pia kuna suala la kuwa na spika wa bunge aliyechaguliwa, labda na wananchi asiye na mafungamano na chama chochote cha siasa kati ya vilivyo bungeni.
 
Hata mimi kuna mtu aliniahidi atanitumia ila hadi sasa hajatuma
alisema atatuma scanned copy (Pdf version). Nikipata naileta.
 
Kwangu mimi bado naona tatizo katika kujenga taasisi huru na zinazowajibika. Mfano, tunaambiwa kuwa rais anaweza kuteua kwa kupata mapendekezo kutoka tume ya utumishi wa umma au tume ya mahakama etc. Na pia anaweza kuteua mawaziri na wao kuthibitishwa na bunge. Katika kumwondoa ofisa asiyewajibika au asiye mwadilifu inakuaje. Huyo afisa au waziri anawajibika kwa nani? Uadilifu wa huyo anayeteuliwa unachunguzwa na nani? Je akiwa kinyume na rais, na case yake ya kutofautiana na rais ukaonekana ni kwa maslahi ya taifa, inakuaje? Hii katiba ni bora liende na sidhani hii tume imefanya howework yake vizuri. Nia ya mtu kuwa au kupewa nafasi Fulani ni vizuri ikawa public na hiyo tume ya maadili ikatoa sababu ya kukubali au kukataa malalamiko yeyote yaliyoletwa na mtu yeyote wakati wowote kabla ya uteuzi kufanyika. Nafasi za watendaji wakuu wa serikali ziwe za ku-apply na kufanya interview. Ziwe pia contractual. Akishindwa ku-deliver, arudi kwenye nafasi yake ya awali kama alikuwa mtendaji wa serikali au aondoke aende anakojua. Otherwise, sioni mabadiliko ya kitaasisi kufuatana na katiba hii. Too low at this era maana tatizo la Tanzania ni mfumo wa kitaasisi zaidi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom