Rasimu ya Katiba Mpya Ibara 113

cabhatica

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
1,081
480
Wadau,

Nimeisoma ibara ya 113(kama ilivyonukuliwa hapa chini) na nikarudia tena na tena lakini sijaielewa. Aliyeielewa tafadhali anitoe kizani.

Utaratibu
wa
kutunga
sheria
kuhusu
mambo
ya fedha


113.-(1) Bunge halitashughulikia jambo lolote kati ya mambo
yanayohusika na Ibara hii isipokuwa kama Rais amependekeza kwamba
jambo hilo lishughulikiwe na Bunge na pendekezo hilo la Rais liwe
limewasilishwa kwenye Bunge na Waziri.
(2) Mambo yanayohusika na Ibara hii ni yafuatayo:
(a) Muswada wa Sheria kwa ajili ya jambo lolote kati ya mambo
yafuatayo:
‐ 46 ‐
(i) kutoza kodi au kubadilisha kodi kwa namna
nyingine yoyote isipokuwa kupunguza;
(ii) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha
yafanywe kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya
Serikali au mfuko mwingine wowote wa Serikali au
kubadilisha kiwango hicho na namna nyingine
yoyote isipokuwa kupunguza;
(b) kuagiza kwamba malipo au matumizi ya fedha yafanywe
kutokana na Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali au mfuko
mwingine wowote wa Serikali wakati ikifahamika kwamba
fedha iliyomo katika mifuko hiyo haikupangiwa itolewe kwa
ajili ya malipo au matumizi hayo, au kuagiza kwamba malipo
au matumizi yanayofanywa kutokana na mifuko hiyo
yaongezwe;
(c) kufuta au kusamehe deni lolote linalotakiwa lilipwe kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano; au
(d) hoja au mabadiliko yoyote ya hoja kwa ajili ya lolote kati ya
mambo yaliyoelezwa katika aya ya (a) ya Ibara hii ndogo.
 
Back
Top Bottom