Rasimu mpya ya elimu 2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rasimu mpya ya elimu 2011

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Michael Amon, Mar 2, 2012.

 1. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #1
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeamua kutoa mfumo mpya wa elimu ambapo imetoa rasimu ya mfumo mpya wa kutoa elimu kuanzia ngazi ya chekechea mpaka ngazi ya elimu ya juu.
  Katika sera hiyo mpya ya Elimu kuna mambo na mabadiliko mengi yaliyopendekezwa ikiwemo yafuatayo:

  Katika rasimu hii mpya ya elimu serikali imeruhusu wanafunzi wenye uja uzito kuendelea na masomo na kufupisha muda wa elimu ya msingi kutoka miaka saba hadi sita.

  Aidha sera hiyo pia inaeleza kuwa wanafunzi wa awali watasoma kutwa nzima kwa mwaka mzima na kupatiwa huduma mbali mbali zinazostahili.

  Pia sera hiyo inasema kuwa wanafunzi wa shule za msingi watakuwa wakisoma kwa miaka sita ikifuatiwa na elimu ya sekondari ambayo wataisoma hadi kidato cha nne. Baada ya kusoma hadi kidato cha nne, ambacho itakuwa ni lazima kufuatiwa na elimu ya juu (Kidato cha tano na sita) ambayo itaendelea kwa miaka miwili.

  Kadhalika sera hiyo inaruhusu wanafunzi wenye vipaji kupandishwa madarasa na wanafunzi wanaojifunza pole pole wataruhusiwa kurudia darasa.

  Kwa upande wa lugha sera hiyo inasema kuwa wanafunzi wa elimu ya msingi na sekondari watasoma kwa lugha ya kiswahili na kiingereza

  Kwa upande wa ada sera hiyo inasema kuwa gharama halisi zitakuwa msingi wa kupanga ada za taasisi ya elimu.

  Katika uchangiaji wa rasimu hiyo kati ya wabunge 30 waliochangia,10 wamepinga elimu ya msingi kwa miaka sita na kutaka iwe saba au nane huku waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akiahidi swala hilo kuangaliwa kiundani.

  Naye mbunge wa Makete (CCM) Dk. Benelith Mahenge, alisema elimu ya msingi iwe miaka nane na ya sekondari iwe miaka mitatu huku akiituhumu Wizara ya Elimu kuwa inaua ufundi na kutolea mfano wa Ujerumani imawesaidia katika kujikita kwenye ufundi.

  Uamuzi wa kuwaruhusu wanafunzi waliopata uja uzito kuendelea na masomo ulipingwa na mbunge wa Nkenge (CCM) Assumpta Mshama ambaye alisema utaleta tatizo kwa sababu watoto wataona kuwa kupata mimba ni jambo la kawaida.

  Na je wewe mdau mwenzangu wa Jamii Forums The Home of great thinkers una maoni gani, mapendekezo au ushauri kuhusiana na rasimu hii mpya ya elimu?
   
 2. M

  Maselle New Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa sasa life expectancy inashuka kila kukicha,hivyo tunajikuta mtu akitumia robotatu ya maisha yake katika kusoma na hivyo sehemu ndogo sana ya maisha yake anaitumia katika kutia mchango wake kwa taifa.Mbona Kenya O-level na Advanced level inasomwa kwa miaka 3 tu.Me naunga mkono kuhusu kupunguza umri wa elimu ya msingi.Nashauri wangefanya hivyo na elimu ya sekondari pia.Kitu cha msingi katika hili ni kuweka mikakati ya kutosha katika kulifanikisha.
  Kuhusu wanaopata ujauzito kuendelea na masomo,siungi mkono hoja kabisa.
   
 3. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,812
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Pamoja na mabadiliko hayo,serikali iweke mitaala ambayo itasaidia watu kujiajiri wenyewe hata baada ya elimu ya msingi na sekondari.
   
 4. N

  Njangula Senior Member

  #4
  Mar 4, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni nzuri ktk sura fulani. Wajawazito wakataliwe ktk mfumo wa kawaida ila waundiwe MEMKWA spesheli. Primary iwe ngazi nane badala ya saba kwani watoto wanahitimu wadogo mno. Halikadhalika sekondari ibaki miaka sita 1-6. Elimu ya chuo irudi miaka minne kwani miaka tatu contentwise is not satsifactory, time for rehearsal is being narrowed kwani wakurufunzi wanapelekeshwa mno! Mitaala ijikite ktk ubunifu zaidi na lugha ya kiswahili ipewe hadhi sawa sambamba na kimombo. Nawasilisha.
   
 5. I

  Ilonza Senior Member

  #5
  Mar 4, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Darasa la saba iwe sita(6) sule ya upili iwe miine, baada ya hapo wajiunge na chuo kikuu au veta.
   
 6. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Mitaala gani hiyo ambayo unegependa serikali iiweke?? Fafanua zaidi mkuu
   
 7. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  sule ya pili ndio nini mkuu???
   
 8. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Shukrani sana kwa maoni yako mkuu. Nadhani wahusika watakuwa wameliona hili wazo lako na watalifanyia kazi
   
 9. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Je, unadhani ni mikakati gani iwekwe ili serikali iweze kufanikisha azma yake hii???
   
Loading...