nyamva
JF-Expert Member
- Oct 6, 2015
- 249
- 163
MREJESHO:Nilileta dukuduku langu juu ya ofisi utumishi ya halmashauri ya Kwimba kukosa maafisa utumishi baada ya waliokuwepo kutumbuliwa.
Jambo hili limekuwa na madhara yake kwetu sisi watumishi wa wilaya hiyo lakini mpaka sasa hakuna hatua yoyote ya makusudi iliyofanyika.
Kinachonishangaza ni ukimya wa ofisi ya RAS MWANZA ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuteua watumishi katika ofisi hiyo ya utumishi wilaya.
Kuna maafisa utumishi wa muda ambao kifupi hawana mamlaka kamili juu ya shida nyeti za utumishi kwa watumishi wa halmashauri hiyo.
ANGALIZO:ewe RAS usifikirie kuwa watu wote shida tunafanana. Hima tuteulie watendaji hawa ili mambo yetu yazidi kwenda kuliko kukwamishwa na uzembe wa utumishi waliopita pamoja na wewe kwa namna moja au nyingine.
Binafsi yangu nahitaji mkopo ili unisaidie kwa ajili ya matibabu ya ndugu yangu. Nimekwamishwa na Ofisi hii maana ndo masignatory. Hivi huoni kuwa naweza kumpoteza ndugu yangu kwa sababu yako?
Chonde chonde kama kuna mtu wa karibu au wewe mwenyewe uonapo ujumbe huu ufanyie kazi. Nawasilisha