Rapa wa Marekani, Offset apigwa risasi Florida

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,514
Reaction score
2,290
Rapa wa Marekani Offset ameripotiwa kupigwa risasi karibu na casino maarufu ya Seminole Hard Rock Hotel & Casino huko Hollywood, Florida.

Mtu wa karibu na rapa huyo amethibitisha kuwa Offset kwa sasa yuko salama na anaendelea vizuri, ingawa mamlaka bado zinaendelea kuchunguza kilichosababisha tukio hilo.

Taarifa ya Polisi ilisema mtu mmoja alipata majeraha yasiyo ya kutishia maisha jioni ya Jumatatu katika eneo la maegesho ya magari (valet) nje ya Seminole Hard Rock huko Hollywood, Florida, ingawa hawakumtaja mhusika, Na kwamba Watu wawili walikamatwa na polisi, na uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Offset ni mzazi mwenzie Msanii Cardi B, walioana mwaka 2017 na kujaaliwa kupata watoto 3 na mwaka 2024 Card B aliweka hadharani kuwa anadai talaka kutoka kwa Offset.

Ikumbukwe mwaka 2022 Binamu yake Offset alifahamika kama 'Takeoff' ambaye pia alikuwa mwanachama wa kundi la Migos, aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka 2022.

 
RIP Rapper
 
Mkuu kama Polisi hawakumtaja muhusika, wewe umejuaje kua ni Offset?

Swali langu ni kwa mujibu wa taarifa uliyoileta hapa.
 
Ma black america celebrities wanashida hawa so bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…