Kitu kipi ambacho hakipo??
Au ni huelewi nini nazungumzia kaka?
Defender imetumika idara ya polisi sio jeshini.
Land cruiser unaweza ukatumia kwa matumizi ya jeshi.
Tusibishane nenda ukafuatilie.
Jeshi la Houthi lina land cruiser kibao kwa matumizi ya jeshi na suala sio kuhusu uendeshaji bali nj ugumu wa gari.
Kiufupi Land cruiser pickup ni HARD BODY.
Point yangu ipo hapo.
Ndio maana kule nilitoaga mfano,izamishe hizo RR zako kwenye tope kubwa uone kama zitatoboa tena zikiwa na mzigo mzito nyuma.
Ila land cruiser inatoboa.
POINT YANGU IPO HAPO.
Hayo masuala ya luxury baki nayo mwenyewe.
Maana kwa mimi nikitaka luxury car nitaenda kwa mercedes.
Mzee sijui tunabishana kitu kipi, na sielewi kipi huelewi, mimi sina hisa Land Rover, na sio kwamba nikisifu panapostahili kusifiwa kwenye RR nitalipwa mshahara, karibu kila post ninayoandika hapa nakuambia kabisa LC inaizidi RR reliability, hilo nalisema kila muda.
SIku LC wakitengeneza gari ambayo ina tech ya juu, ipo complex kwenye electronics na mechanical elewa haiwezi kuwa reliable kama ilivyo sasa.
LC hakuna mtu amekataa kwamba ni reliable, lakini kuhusu horsepower, speed, luxury kuanzia muziki, interior n.k LC haiwezi kufikia huko, hilo lipo wazi kiongozi, kaka huwezi linganisha RR sport SV au autobiography na LC...
Ukilinganisha kwenye reliability LC anatoka mshindi, ukilinganisha kwenye luxury, comfort, speed LC haiwezi izidi RR...
Kingine Range rover wana matoleo mengi , wana model na trims nyingi, ni wewe tu kujichagulia tokana na matumizi, Land ROver ni wakali wa kuteneneza SUVs, hujawahi kusikia hata siku moja wanatengeneza Sedan, wamewekeza heavily kwenye SUVs...
Hata rolls royce wametoa SUV yao ya kwanza ndio kama ile Diamond anayo, nachomaanisha Land rover wana uzoefu mkubwa wa kutengeneza SUVs, wao wana focus kwenye innovation na luxury, hawa focus kwenye reliability.
Na unapozungumzia kuizamisha gari kwenye tope, ingia youtube tazama hizo SUVs zikishindanishwa , binafsi sijawahi kuona kwa macho live zikishindanishwa... maana RR wana toleo lao la RR(full size) ambayo huwa ina uwezo mzuri tu unaoridhisha wa off road ukiachana na sport SV, sport n.k
Lakini LC itabaki kuwa gari imara, reliable, yenye uwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira magumu hata uki i abuse...
RR inabaki kuwa gari yenye tech ya juu, speed, comfort, luxury ....
Hivyo kila kampuni iliamua ku focus kivyake na wote wanapaa wateja. Ni wewe mteja sasa kuchagua unataka wapi..
Technology kama Matrix LED/pixel LEDs headlights kwenye Range Rover, taa ya mbele inakuwa na taa ndogo ndogo ambazo baadhi zinaweza kujizima na baadhi zikawaka kama high beam...
Hivyo kama kuna gari mbele inakuja na unaendesha Range Rover, hata kama umewasha full light huwezi kumuumiza macho dereva wa gari inayokuja mbele yako, maana RR itaona hio gari, itazima taa zinazoimulika ile hio gari na kumulika barabara pekee... hivyo dereva mwingine hawezi dhurika na mwanga wa gari lako...
Huo mfumo umeunganishwa na computer pamoja na camera, hivyo gari inatambua kama ni boda inakuja, inazima upande wa hio boda ili kutomuumiza macho, then inawasha sehemu zingine zote za barabara...
Hivyo Unapoambiwa RR ina tech za juu inabidi uelewe.. kila part ya RR unayogusa ipo complex...
Tech hio inaepusha ajali, ni kitu cha kawaida lakini kwenye RR wamejali...
HUjazungumzia Active Noise Cancellation, terrain response 2, wading sensor(sensor za kupima kina cha maji gari inapozama kwenye maji), all wheel steering na takataka zingine nyingi...
Hivyo elewa RR wamewekeza sana kwenye tech.
Tchao.