Mmmh mkuu hapa unanipiga kamba.
Unaizungumzia LC300 au Land cruiser kiujumla??
Kama unazungumzia Land cruiser kiujumla basi hakuna nchi isiyotumia Land cruiser. Tena Toyota hupokea special order za kuunda ARMORED landcruiser.
Kipindi Rishi Sunak ni waziri mkuu kwenye convoy yake armored Land cruiser VX zilikuwemo na huyo ni waziri wa Uingereza.
Serikali nyingi Asia,South America hata baadhi ya European nations wanatumia Land cruiser.
UN tizama maeneo yote ya hatari wanayoenda hukuti wakitumia gari zingine zaidi ya landcruiser.
Iwe nchi zozote zile duniani hukuti wakitumia gari tofauti na land cruiser. Kwahiyo wao UN hawajui gari reliable!?
Toyota huwa wanapokea special order ya kuzi PIMP land cruiser ziweje.
Land cruiser utayoitumia wewe sio sawa atayoitumia mtu wa Ulaya.
Kuna land cruiser ukizipiga RPG hazilipuki. Bongo unazipata!??
Hizo ndio unakuta zinaanzia $ 500,000.
Magaidi wote na waasi wote umewahi kuona wanatumia gari za vita tofauti na land cruiser pickup za engine ya 1hz?
Ifunge rocket launcher nyuma ya Range au land rover halafu ifyatue uone kama hatujaizika hiyo Rover yako.
Embu ichukue Range rover yako kaipigishe mbizi jangwani uone kama itatoboa kwenye mchanga wa jangwani.
LABDA KAMA UTASEMEA land cruiser LC300 peke yake.
Ila kama unazungumzia LAND CRUISER KIUJUMLA weeeh! Kafanye tafiti vizuri.
Kiongozi Range rover wanayo gari yao kwa ajili ya ulinzi , ambayo ni Range Rover sentinel, ndio hio umemuona Samia anapita nayo majuzi na kwenye huu uzi juu posts za mwanzoni kuna mdau ameweka picha yake...
Sentinel zinakuwa kwa wingi kwenye misafara ya waziri mkuu wa Uingereza , ni heavily armored, luxury SUV ambayo inakuwa designed na Land Rover wenyewe kwa ajili ya ulinzi wa viongozi/watu mashuhuri n.k...
Land Cruiser ambayo ni armored haitengenezwi na Toyota wenyewe, kuna makampuni yanayohusika na kutengeneza (armoring companies), wanaiununua hio gari, wana i disassemble halafu wanaweka ballistic steel, armored glass, suspension, run flats n.k...
Na hizo gari huwa wanazi certify tokana na uwezo ilionao wa kuhimili milipuko, mashambulizi ya risasi n.k.. kwa kipimo wanaita VR, ambapo maxmum level ni VR10, hio sentinel ina VR8...
Kuna gari nyingi tu kutoka makampuni mengine ambazo ni armored na ni imara sana, mfano Audi 8L, hio anatumia hata waziri mkuu wa Uingereza, hivyo tusikariri tu Range Rover na Land Cruiser, hio A8L ni sedan lakini kwenye VR level ina VR9 huko Range rover ina VR8, Land cruiser mara nyingi zina VR7 hasa hizi wanatumia marais wa huku Africa...
Hio sentinel ina uwezo wa kuhimili bomu chini ya gari ama juu ya gari, ina emergency exit, ina uwezo wa kuzuia risasi kutoka kwenye AK47... na ni gari imetengenezwa ku escape mashambulizi which means ina mbio, hivyo inakimbia hata kama tairi zikipigwa zikawa flat....
Hivyo Range ROver hio sentinel ikitokea shambulizi, ina uwezo wa ku escape na kukimbia kutoka eneo la tukio kwa kasi kuliko hio LC 300 ambayo pia ni armored, kumbuka RR sentinel inatoka kiwandani ikiwa imetengenezwa na Land Rover wenyewe...
Hio LC 300 inakuwa modified na hizo kampuni za armoring, hivyo wanaiongezea uzito zaidi tofauti na toyota wenyewe walivyokadiria uzito wake na perfomance kutoka kiwandani...
Ndio maana katika hiki kipindi ambacho nchi yetu inapitia changamoto za kiusalama hasa kwa viongozi kamati ya ulinzi wa rais Tanzania wakaona wapendekeze hio Sentinel na kuiacha Land Cruiser....