Rambo nyeusi zimetoweka zimekuja rambo za blue 😌

whitehorse

JF-Expert Member
Aug 29, 2009
2,565
4,426
Wana JF , Ninaandika kwa wino wa masikitiko kuhusu hii mifuko ya nylon (plastick) kwa sasa inajulikana kama vifungashio .

Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)wamefeli kabisa kulinda mazingira kwa kuruhusu vifuko hivyo kuendelea kutumika kwa kiwango kile kile cha rambo nyeusi "vifuko laini" Kwa sasa imezagaa vile vile kwenye ardhi na itafanya uharibifu ule ule.

Kwa viumbe hai wanaoishi kwenye maji na nchi kavu Hizi mifuko za plastick za Blue hazifai. Na ndio zinatumiwa kwa kasi haswa uswazi kwa kina sisi wa kipato cha chini. Ukienda gengeni kukua karoti moja unawekewa kwa hizo mifuko au mihogo ya kukaanga unawekewa kwa hizo platick za blue wauza chips nao wameshavamia wanaweka huko chips za wateja.

Zimeanza kuwa kero Haziozi zikifukiwa udongoni zinadumu kama kawaida ni bora wangetuambia kuwa wanapiga marufuku nyeusi wanaleta za bluu.

Sijui nini kinawapa uhuru wa kuhatarisha afya zetu kwa urahisi namna hii. Wanashindwa vipi kusimamia kutokomeza matumizi ya vifungashio vya plastick . Pathetic 😫

01FF2397-46D9-4B53-801C-1284C772EDAC.jpeg
 
Back
Top Bottom