Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rambirambi ya CHADEMA zanzibar ikataliwe ni "WANAFIKI"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAZETI, Nov 16, 2011.

  1. GAZETI

    GAZETI JF-Expert Member

    #1
    Nov 16, 2011
    Joined: Feb 24, 2011
    Messages: 2,908
    Likes Received: 256
    Trophy Points: 180
    Ndo kwanza nimeingia ndani, nafungua TV. kama kawaida ya TBC nakutana na
    Bunge. Mbunge mmoja ambaye kwa lafudhi yake nahisi ni Mzanzibar Anasema


    "......... Naomba makamu wa pili wa rais arudishe fedha za rambirambi zilizotolewa
    na CHADEMA katika ofisi yao.......... Maana kwa hiki kilichoandikwa na Lisu humu
    CHADEMA ni wanafiki (Makofi... meza za walipa kodi zinagongwa).... Hata maiti
    hawako tayari kupokea rambirambi hizi hivyo zirudishwe (Makofi zaidi)...... Naunga
    mkono hoja mia kwa mia. Anakaa.
    Naibu spika. Ahsante Ujumbe wako umefika katika vyombo husika.

    SAMAHANI HII HABARI NIMEIKUTA MWISHO.

    Nauliza. Hivi LISU kaandika nini kuhusu wazanzibar?
     
  2. King'asti

    King'asti JF-Expert Member

    #2
    Nov 16, 2011
    Joined: Nov 26, 2009
    Messages: 27,074
    Likes Received: 1,322
    Trophy Points: 280
    Japo sijaona hiyo taarifa,natatizwa sana na watu wasiokuwa na alternative solutions. Mbunge angekua wa maana kama angetaa posho za 'wanafiki' na kutoa walau posho yake ya vikao ama basi hela zake za jimbo kama rambirambi kwa wafiwa. Na akumbuke maiti hawahitaji rambirambi bali wale wategemezi wao.
     
  3. Bushloiaz

    Bushloiaz JF-Expert Member

    #3
    Nov 16, 2011
    Joined: Nov 2, 2010
    Messages: 468
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 35
    Wanzazibar wenyewe hawautaki muungano siwaelewi hawa wabunge kutoka znz wanamwakilisha nani
     
  4. Kombo

    Kombo JF-Expert Member

    #4
    Nov 17, 2011
    Joined: Oct 29, 2010
    Messages: 1,819
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 0
    Mwajiriwa mpya kazini hulazimishwa kufanyiwa medical examination ikiwa ni mojawapo ya "masharti" ya ajira ingawa sehemu nyingine haizingatiwi sana.

    Hali hiyo pia huwakumba wanafunzi na wanavyuo wote.

    Nauliza, hivi Wabunge wanafanyiwa medical examination kabla ya kuapishwa? Hiyo medical examination inahusisha pia
    kupima uwezo wao wa kufikiri, kumbukumbu, akili nk?
     
  5. D

    Derimto JF-Expert Member

    #5
    Nov 17, 2011
    Joined: Nov 4, 2010
    Messages: 1,305
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 135
    Ni swali sasa! Kwani fedha za rambirambi ametoa Lissu kama yeye au ni chama ndiyo kimetoa?
     
  6. BongoLogik

    BongoLogik JF-Expert Member

    #6
    Nov 17, 2011
    Joined: Aug 10, 2009
    Messages: 261
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    imani nyingine ni za ajabu sana,toka lini maiti ikahitaji rambirambi?! na huyo mbunge aliyetoa hoja hiyo akili zake ni hovyo kabisa, ***** huyu anaweza kumnyang'anya mtalaka wake hata nguo za ndani alizomnunulia wakati alipokuwa mkewe! pesa ishaingia kwenye hesabu yeye anataka irudishwe! kama ana uchungu kweli basi fedha irudishwe na yeye afidie kwa gharama zake! shwain kabisa huyu!
     
  7. Globu

    Globu JF-Expert Member

    #7
    Nov 17, 2011
    Joined: Jan 12, 2011
    Messages: 7,963
    Likes Received: 133
    Trophy Points: 160
    Wabunge wa ZNZ ni wanafik, wachoyo, roho mbaya, wachawi, waongo, wajinga......malizia.....VIVA JF.
     
  8. kikahe

    kikahe JF-Expert Member

    #8
    Nov 17, 2011
    Joined: May 23, 2009
    Messages: 1,271
    Likes Received: 6
    Trophy Points: 135
    Tatizo la wabunge bara na viongozi wa serikali wanaogopa kusema ukweli. Huu muungano unalazimishwa sana hata wa-Zanzibar wenyewe hawautakii. Aliyosema Tundu Lissu ni ukweli tupu, wao mambo yao wanakuja kuyaongelea kwetu ila sisi hatuendi kuongelea mabo yetu kwao. mchezo wa ajabu kweli kweli
     
  9. Edward Teller

    Edward Teller JF-Expert Member

    #9
    Nov 17, 2011
    Joined: Oct 31, 2010
    Messages: 3,774
    Likes Received: 55
    Trophy Points: 145
    wazanzibar ni wananafiki-warudishe na zile walizopewa na makampuni ya bia
     
  10. v

    valid statement JF-Expert Member

    #10
    Nov 17, 2011
    Joined: Sep 18, 2011
    Messages: 2,730
    Likes Received: 162
    Trophy Points: 160
    Huyu mbunge alotamka ivi... Kwa kweli uwezo wake wa kufikiri upo chini sana !
    Ila hao wanaompigia makofi, nao inabidi tujiulize kama wako timamu.
     
  11. Chilli

    Chilli JF-Expert Member

    #11
    Nov 17, 2011
    Joined: Jul 17, 2011
    Messages: 1,638
    Likes Received: 23
    Trophy Points: 135
    Hawa wabunge wa Z'bar wana matatizo. Wanadhani sisi tunajigonga kwao? Kama imewauma wazirudishe, CHADEMA wakizikataa nimtumie akaunti yangu anitupie. Alaah!
     
  12. Skp2ole

    Skp2ole Senior Member

    #12
    Nov 17, 2011
    Joined: Oct 13, 2011
    Messages: 104
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    dah! Taamu kwelikweli hebu goja tuone mwisho wa haka kamchenzo ka siasa katafika wapi kama Siyo Libya basi nchi za Arabuni
     
Loading...