Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 9,009
- 13,539
BREAKING NEWS:
Jeshi la Madagascar limetangaza mapinduzi na limesimamisha katiba na kumwondoa madarakani Rais Andry Rajoelina kufuatia maandamano yaliyokuwa yakiendelea.
Kitengo maalumu cha CAPSAT (ambacho kilimweka Rajoelina madarakani katika mapinduzi ya mwaka 2009),kilimsaliti Rajoelina mnamo Oktoba 11, kikijiunga na waandamanaji wa kizazi cha Gen Z Madagascar huko Antananarivo. Askari waliendesha magari ya kivita hadi katika Uwanja wa Mei 13, bila kuwashambulia waandamanaji, huku Kamanda Lylison René de Rolland akipata uungwaji mkono.
Maandamano, yaliyoanzishwa na uhaba wa umeme na maji, yanakemea ufisadi na umaskini unaoathiri asilimia 75% ya raia milioni 32 . Yakadiriwa watu 22 wamekufa, na 100 kujeruhiwa kulingana na ripoti za UN. Rajoelina, aliyekuwa amejificha na wafuasi wake, alishutumu foreign intervention ; ripoti zinathibitisha kuwa kishakimbia kutoka mji mkuu. Jeshi sasa linashikilia mamlaka.