RAJAONARIMAMPIANINA Rakotoarimanana Hery Martial

omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,162
2,000
Huyu ni rais mtarajiwa wa nchi iliyo katika Bahari ya Hindi ijulikanayo kama Madagascar.
Naombeni wajuzi wa lugha kama mnaweza kutupa utamkaji sahihi na maana ya jina lake:
RAJAONARIMAMPIANINA Rakotoarimanana Hery Martial

Hery.jpg
 
Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,537
2,000
RAJAO-NARIMA-MPIANINA Rakoto-ari-manana

Ukitaka kusoma na kukumbuka, basi soma hivyo. Wanaunga Majina mengi kwenye jina moja.

Kama hapo mwanzo unaona ni RAJAO na linafuata NARINA na mwisho MPIANINA. Nafikiri nimekusaidia.
 
MESTOD

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
4,789
2,000
Huyu ni rais mtarajiwa wa nchi iliyo katika Bahari ya Hindi ijulikanayo kama Madagascar.
Naombeni wajuzi wa lugha kama mnaweza kutupa utamkaji sahihi na maana ya jina lake:
RAJAONARIMAMPIANINA Rakotoarimanana Hery Martial

View attachment 129844

Usicheze kabisa na kitu inayoitwa 'mnara wa Babeli'. Mtu akiandika hayo lazima group livunjike utafute wa kufanana nao msepe..
 
omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,162
2,000
Madagascar yapata Rais mpya

3 Januari, 2014 - Saa 10:23 GMT
140103100923_rais_mpya_wa_madagascar_304x171_bbc_nocredit.jpg

Rais mpya wa Madagascar Hery Rajaonarimampianina
Maafisa nchini Madagascar wanasema kuwa matokeo ya mwanzo mwanzo ya duru ya pili ya uchaguzi wa Rais uliofanyika mwezi Disemba, yanaonyesha mshindi kuwa waziri wa zamani wa fedha Hery Rajaonarimampianina.
Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo inasema kuwa bwana Hery Rajaonarimampianina alishinda asilimia hamsini na tatu ya kura zilizopigwa.
Mshindani wake, Jean Louis Robinson anasema kuwa uchaguzi ulikumbwa na wizi wa kura na sasa anasema sharti shughuli ya kuhesabu kura irejelewe.
Uchaguzi huo ulikuwa mpango wa kurejesha utulivu kwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi kufanyika miaka minne iliyopita.
Bwana Rajaonarimampianina alikuwa mgombea aliyeungwa mkono na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi, Rais wa zamani Andry Rajoelina.
 
omujubi

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
4,162
2,000
RAJAO-NARIMA-MPIANINA Rakoto-ari-manana

Ukitaka kusoma na kukumbuka, basi soma hivyo. Wanaunga Majina mengi kwenye jina moja.

Kama hapo mwanzo unaona ni RAJAO na linafuata NARINA na mwisho MPIANINA. Nafikiri nimekusaidia.
Ngoja nianze kufuatilia kwenye 'oral media' maana ndio anaonekana kushinda sasa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions
Thread starter Title Forum Replies Date
C Heri ya kuzaliwa Dr. Martin Luther King International Forum 10

Similar Discussions

Top Bottom