Raisi Magufuli, kwanini mpaka sasa hujaunda Tanzania Disaster Management Agency (TDMA)?

Kwa kuwa rais ni mpole na ni tofauti ya kagame,uhuru na museveni ndio maana wameamua kumfuata mpaka chumbani kwa kuwacha kujadili vitu vya maana wanajadili kauli zilizopita!
Jiwe mpole??? Kapiga watu risasi, kupoteza kina Ben na wengineo, katia watu jela ili aongopwe lakini wapi, ndio kwanza wanamuona hajielewi. Kachanganyikiwa ajuhi cha kufanya

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Kama ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza uanzishwaji wa wakala wa meli nchini kama ulivyoshauriwa na kamati mojawapo ya makinikia, ndivyo ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza wala kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa taasisi hii ambayo itahusika na management ya majanga mbalimbali nchini.

Licha ya Bunge kupitisha sheria ya Disaster Management Act tarehe 26/03/2015,si wewe wala mtangulizi wako ambae ameanzisha hii taasisi.

Hii Agency ingekuwa ni chombo muhimu sana katika kusimami na kuzuia majanga mbalimbali, kuishauri serikali na pia ingeshirikiana na wakuu wa taasisi kama Mamlaka ya Hali ya Hewa,TCRA, Mamla ya Chakula na Dawa, Hifadhi ya Taifa ya chakula,kikosi cha zimamoto,n.k pamoja na wizara mbalimbali katika utendaji wake wa kazi.

Nashangaa hata baada ya hii ajali kutokea, jambo hili halipewi uzito licha ya umuhimu wa taasisi hii katika kushughulikia na kudhibiti majanga mbalimbali hapa nchini na ikiwemo kutoa ushauri kwa serikali kuhusiana na maswala mazima ya majanga.

Ni ajabu hata wapinzani nao wako kimya kabisa kuhusu uanzishwaji wa hii taasisi hata baada ya kutokea kwa hii ajali.

Wabongo hatujielewi kabisa!
Mkuu @salaryslip mada za namna hii ndio zinaonesha maturity na uwajibikaji kwa maslahi na manufaa ya Taifa.
 
brilliant, good post

kinachotufanya mimi na wewe kuonekana wapuuzi ni kuwa tunakumbuka haya mambo baada ya majanga!

ndio ndio maana umesema bongo hatujielewi

mngeacha zile siasa za kupinga, kukejeli na ku focus kwenye issues za maana kama hizi, ingekuwa bora sana na kujiwekea wigo wa kuonwa ni watu wa maana

waziri husika kivuli wa upande wa upinzani alipaswa ajiuzulu kushinikiza hawa wengine wajiuzulu
Huwa nashangaa sana wanavyotumia nguvu katika hoja za ulaghai na uzushi.
Kwa maoni yangu unaeza kuibana Serikali vilivyo kwa kutumia vipengele vya namna hii yaani bila tusi wala kejeli bali hoja zenye mshiko na zenye ukweli
 
Pamoja na hilo, waliokuwa na wajibu wa kutekeleza uanzishwaji wa taasisi hiyo ni serikali na sio wapinzani hivyo hawawezi kukwepa lawama.
 
KUNAHAJA YA KUPINGIZA TAASISI KUBANA MATUMIZI mheshimiwa rais anaweza manbo mengi pekenyake naona watumishi wanakula tu mishahara
 
Huwa nashangaa sana wanavyotumia nguvu katika hoja za ulaghai na uzushi.
Kwa maoni yangu unaeza kuibana Serikali vilivyo kwa kutumia vipengele vya namna hii yaani bila tusi wala kejeli bali hoja zenye mshiko na zenye ukweli

kabisa

na wameishajiua!! cdm is no more
 
Kwa kuwa rais ni mpole na ni tofauti ya kagame,uhuru na museveni ndio maana wameamua kumfuata mpaka chumbani kwa kuwacha kujadili vitu vya maana wanajadili kauli zilizopita!
kwann hajaenda na huwa haendagi kuzika na kuwafariji wahanga au mpaka TB joshua aseme neno?.ulozi na ushirikina unahusika
 
Back
Top Bottom