Raisi Magufuli, kwanini mpaka sasa hujaunda Tanzania Disaster Management Agency (TDMA)?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,268
2,000
Kama ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza uanzishwaji wa wakala wa meli nchini kama ulivyoshauriwa na kamati mojawapo ya makinikia, ndivyo ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza wala kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa taasisi hii ambayo itahusika na management ya majanga mbalimbali nchini.

Licha ya Bunge kupitisha sheria ya Disaster Management Act tarehe 26/03/2015,si wewe wala mtangulizi wako ambae ameanzisha hii taasisi.

Hii Agency ingekuwa ni chombo muhimu sana katika kusimami na kuzuia majanga mbalimbali, kuishauri serikali na pia ingeshirikiana na wakuu wa taasisi kama Mamlaka ya Hali ya Hewa,TCRA, Mamla ya Chakula na Dawa, Hifadhi ya Taifa ya chakula,kikosi cha zimamoto,n.k pamoja na wizara mbalimbali katika utendaji wake wa kazi.

Nashangaa hata baada ya hii ajali kutokea, jambo hili halipewi uzito licha ya umuhimu wa taasisi hii katika kushughulikia na kudhibiti majanga mbalimbali hapa nchini na ikiwemo kutoa ushauri kwa serikali kuhusiana na maswala mazima ya majanga.

Ni ajabu hata wapinzani nao wako kimya kabisa kuhusu uanzishwaji wa hii taasisi hata baada ya kutokea kwa hii ajali.

Wabongo hatujielewi kabisa!
 
jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
3,949
2,000
Bila shaka mpaka wapinzani wote waunge mkono juhudi ndio itaanzishwa.
Wapinzani wanamchanganya sana jiwe mpaka anajiona ni kichaa na kuamua kuchagua vichaa wamsaidie.
Usitegemee hapo vitu vya msingi kupewa umuhimu.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,268
2,000
Kama ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza uanzishwaji wa wakala wa Meli nchini kama ulivyoshauriwa na kamati mojawapo ya makinikia, ndivyo ambavyo mpaka leo hii nawe haujatekeleza wala kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa taasisi hii ambayo itahusika na management ya majanga mbalimbali nchini.

Licha ya Bunge kupitisha sheria ya Disaster Management Act tarehe 26/03/2015,si wewe wala mtangulizi wako ambae ameanzisha hii taasisi.

Hii Agency ingekuwa ni chombo muhimu sana katika kusimami na kuzuia majanga mbalimbali, kuishauri serikali na pia ingeshirikiana na wakuu wa taasisi kama Mamlaka ya Hali ya Hewa,TCRA, Mamla ya Chakula na Dawa, Hifadhi ya Taifa ya chakula,kikosi cha zimamoto,n.k pamoja na wizara mbalimbali katika utendaji wake wa kazi.

Nashangaa hata baada ya hii ajali kutokea, jambo hili halipewi uzito licha ya umuhimu wa taasisi hii katika kushughulikia na kudhibiti majanga mbalimbali hapa nchini na pia kutoa ushauri kwa serikali kuhusiana na maswala mazima ya majanga.

Ni ajabu hata wapinzani nao wako kimya kabisa kuhusu uanzishwaji wa hii taasisi.

Wabongo hatujielewi kabisa!
Zitto hii taasisi mbona humuisemei licha ya umuhimu wake?
 
meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,154
2,000
Nasikitishwa na hulka ya watanzania ya ujuaji mwingi mbele giza.

Nimefuatilia kwa karibu mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii inayohusisha watu wa strata tofauti tofauti ,lakini nilikuwa interested kuona muitikio,ukosoaji na ushauri wa wanasiasa wetu ambao aghalabu hutaka kupata umaarufu katika kila tukio.

Ukweli ni kwamba kuna ombwe kubwa sana kama nchi katika kureact inapokuja issues mbalimbali haswa majanga kama hili la MV Nyerere.

Wataalamu hawaji mbele au hawaandai taarifa kwa muda muafaka ili kuelezea kitaalamu nini kimetokea na nini kinaendelea.

Wataalamu hawachangii mijadala kama wataalamu bali wanashabikia upotoshaji unaotolewa na wanasiasa.

Hili linawafanya wanasiasa kuwa vinara na thinktanks katika mambo wasiyo na ujuzi nao.

Shame upon them and all of them!

Nirejee kwenye mada yangu kwa kusema kuwa sijaona mwanasiasa yoyote au niwe specific mbunge yoyote aliyeongelea janga hili in aspects of available policy,regulations and implimentation plans.

Wabunge wanarushiana maneno ya nguoni tu,wengine wanadhihaki JWTZ au ZIMAMOTO n.k

Ipo Act ya Disaster Management 2015 iliyopitishwa na bunge kutumika katika usimamizi wa majanga kabla,pindi na baada yanapotokea ...je wabunge wetu wanaiongeleaje?
Je wanaifahamu?
Je ina mapungufu?

Je inatekelezeka ?

Je imeshaanza kutekelezwa au la?

Zitto Kabwe nilitegemea kwa nafasi yako na juhudi zako za kukosoa ujikite katika eneo hili ambalo ndio la kisiasa haswa.

Ningefurahi kuona mbunge au kiongozi wa ACT anakuja na sera mbadala ya ACT katika kushughulikia majanga.

Nilitarajia kuona Chadema wakikosoa Sera iliyopo japo vipengele kadhaa na kuainisha alternatives.

Nilitaraji kusikia juu ya wabunge wa CCM wakitafakari utekelezwaji wa mswada uliopitishwa na bunge.

Hivi ndivyo ninavyotarajia wabunge na wanasiasa wetu wajadili majanga pindi yanapotokea.

Hulka hii ya wanasiasa kwa sasa ni hatarishi kwani kuna siku tunaweza kuwa vitani na akaibuka mwanasiasa mmoja na kutaka kuwaelekeza wanajeshi jinsi ya kutumia silaha!

RIP KWA WAATHIRIKA WA MAJANGA YOTE TANZANIA.
 
Attachments

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
7,840
2,000
Kwa kuwa rais ni mpole na ni tofauti ya kagame,uhuru na museveni ndio maana wameamua kumfuata mpaka chumbani kwa kuwacha kujadili vitu vya maana wanajadili kauli zilizopita!
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,268
2,000
Hili la kupuuza hii act hata mimi linanishangaza sana na nimelisema sana humu ila watu hawaoni umuhimu.

Hapa mpaka atokee mtu maarufu aongee labda ndio itaonekane ni hoja.

Kutokuwa na taasisi kama Tanzania Disaster Management Agency(TDMA) katika nchi, ni kasoro kubwa sana katika swala zima la kukabiliana na majanga lakini watanzania wote wakiwemo wanasiasa wa chama tawala na mashabiki wao, wapinzani na mashabiki wao wote kwa ujumla wanapuuza kabisa jambo hili.

Sisi wabongo sijui tukoje!!
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,828
2,000
Hili la kupuuza hii act hata mimi linanishangaza sana na nimelisema sana humu ila watu hawaoni umuhimu.

Hapa mpaka atokee mtu maarufu aongee labda ndio itaonekane ni hoja.

Kutikuanzishwa kwa Tanzania Disaster Management Agency ni tatizo kubwa sana ambalo watanzania wote wakiwemo na wanasiasa wa chama tawala, wapinzani na mashabiki wao wote wanapuuza jambo hili.

Sisi wabongo sijui tukoje!!
Haya ndio maswala ya kujadiliwa na kutolewa ufafanuzi ili tupate suluhisho la kisomi kwenye maafa.
 
Pepat

Senior Member
Aug 7, 2018
142
500
Hivi kwani ni siri tena kwamba sheria za nchi hazifuatwi? Kuna mtu asiyefahamu kwamba tunafuata maagizo ya kiongozi wa malaika? Hata wangejadili hiyo sheria ya majanga ingesaidia nini kama kila kitu kinategemea mawazo ya mtu mmoja, wenyewe wanaita " serikali ya joni pombe magufuli" na wala hawakosei hii kweli ni "serikali ya joni pombe magufuli"
 
silver_back

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
841
1,000
Hili la kupuuza hii act hata mimi linanishangaza sana na nimelisema sana humu ila watu hawaoni umuhimu.

Hapa mpaka atokee mtu maarufu aongee labda ndio itaonekane ni hoja.

Kutokuwa na taasisi kama Tanzania Disaster Management Agency(TDMA) katika nchi, ni kasoro kubwa sana katika swala zima la kukabiliana na majanga lakini watanzania wote wakiwemo wanasiasa wa chama tawala, wapinzani na mashabiki wao wote kwa ujumla wanapuuza kabisa jambo hili.

Sisi wabongo sijui tukoje!!
Kumbe asubuhi ukitulia unaongeaga point.
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,242
2,000
Hakuna mahali au wakati ambapo wenye akili timamu wanajadili vifungu vya sheria wakati wa dharura. Ni jambo la kawaida kabisa kurushiana lawama wakati wa dharura japo si vema. Haihitaji kujadili sheria na kuidadavua na ku-debate uhalali wa day worker ambaye hana mafunzo kuendesha meli huku anazungumza au kuchati kwa simu. Haihitaji kuichambua sheria ili kujua kuwa kivuko chenye uwezo wa abiria 101 hakitakiwi kujaza zaidi, let alone kuwa na watu karibu 300. Haihitaji kuisoma sheria kujua kuwa kazi ya kuokoa walio katika hatari ya kufa haiwezi kuzuiwa na giza wakati madaraja na flyovers zinajengwa usiku na mchana na uwezo na vifaa vipo.

Huu ni wakati wa dharura na maombolezo. Disaster Management Act ilipaswa kujadiliwa kabla ya dharura kutokea ili kuboresha au kuongeza ubora wa utayari wa taifa kukabiliana na majanga. Sasa kwa sababu hilo halikufanyika, na kwasababu sasa shughuli za uokoaji na maombolezo zinaelekea mwisho, wataalamu wa sheria nacwananchi tunaweza kuanza kuilimishana kuhusu namna ambavyo tunaweza kuwa tayari wakati wowote kukabiliana na majanga kwa haraka.

Si vizuri kulaumu wawakilishi weyu na wanasiasa kwa ujumla kwa kutokujadili sheria wakati wa dharura kwasababu huu ni wakati wa utekelezaji wa sheria japo yawezekana haijulikani vizuri hasa kwa sisi wananchi wa kawsida tunaitegemeza nchi kwa kulipa kodi.

Tuwe wavumilivu sababu yawezeka MUNGU ameruhusu haya yatukute ili tuijadili sheria lakini hebu tumalize msiba na uokoaji kwanza.

Pole nyingi kwa wafiwa na watanzania kwa ujumla. MUNGU ibariki Tanzania!
 
Msengapavi

JF-Expert Member
Oct 23, 2008
8,242
2,000
Kama ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza uanzishwaji wa wakala wa meli nchini kama ulivyoshauriwa na kamati mojawapo ya makinikia, ndivyo ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza wala kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa taasisi hii ambayo itahusika na management ya majanga mbalimbali nchini.

Licha ya Bunge kupitisha sheria ya Disaster Management Act tarehe 26/03/2015,si wewe wala mtangulizi wako ambae ameanzisha hii taasisi.

Hii Agency ingekuwa ni chombo muhimu sana katika kusimami na kuzuia majanga mbalimbali, kuishauri serikali na pia ingeshirikiana na wakuu wa taasisi kama Mamlaka ya Hali ya Hewa,TCRA, Mamla ya Chakula na Dawa, Hifadhi ya Taifa ya chakula,kikosi cha zimamoto,n.k pamoja na wizara mbalimbali katika utendaji wake wa kazi.

Nashangaa hata baada ya hii ajali kutokea, jambo hili halipewi uzito licha ya umuhimu wa taasisi hii katika kushughulikia na kudhibiti majanga mbalimbali hapa nchini na ikiwemo kutoa ushauri kwa serikali kuhusiana na maswala mazima ya majanga.

Ni ajabu hata wapinzani nao wako kimya kabisa kuhusu uanzishwaji wa hii taasisi hata baada ya kutokea kwa hii ajali.

Wabongo hatujielewi kabisa!
Inawezekana bado hajui kuna hiyo sheria!
 
BIOTYPE

Member
Jul 2, 2018
94
125
Sheria zilizopo hazifuatwi kwa weledi. Kwanza, kinachotakiwa ni kuzingatia na kutekeleza kadiri ya sheria na kanuni zilivyo. Halafu, katika utekelezaji kutajitokeza changamoto zitakazosababisha kupitia (review) hizo sheria / kanuni ili kuziboresha kulingana na uhalisia unaojitokeza! Vinginevyo, itakuwa ni kumfunga punda nyuma ya mkokoteni!
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
14,530
2,000
Kama ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza uanzishwaji wa wakala wa meli nchini kama ulivyoshauriwa na kamati mojawapo ya makinikia, ndivyo ambavyo mpaka leo hii haujatekeleza wala kuanzisha mchakato wa uanzishwaji wa taasisi hii ambayo itahusika na management ya majanga mbalimbali nchini.

Licha ya Bunge kupitisha sheria ya Disaster Management Act tarehe 26/03/2015,si wewe wala mtangulizi wako ambae ameanzisha hii taasisi.

Hii Agency ingekuwa ni chombo muhimu sana katika kusimami na kuzuia majanga mbalimbali, kuishauri serikali na pia ingeshirikiana na wakuu wa taasisi kama Mamlaka ya Hali ya Hewa,TCRA, Mamla ya Chakula na Dawa, Hifadhi ya Taifa ya chakula,kikosi cha zimamoto,n.k pamoja na wizara mbalimbali katika utendaji wake wa kazi.

Nashangaa hata baada ya hii ajali kutokea, jambo hili halipewi uzito licha ya umuhimu wa taasisi hii katika kushughulikia na kudhibiti majanga mbalimbali hapa nchini na ikiwemo kutoa ushauri kwa serikali kuhusiana na maswala mazima ya majanga.

Ni ajabu hata wapinzani nao wako kimya kabisa kuhusu uanzishwaji wa hii taasisi hata baada ya kutokea kwa hii ajali.

Wabongo hatujielewi kabisa!

brilliant, good post

kinachotufanya mimi na wewe kuonekana wapuuzi ni kuwa tunakumbuka haya mambo baada ya majanga!

ndio ndio maana umesema bongo hatujielewi

mngeacha zile siasa za kupinga, kukejeli na ku focus kwenye issues za maana kama hizi, ingekuwa bora sana na kujiwekea wigo wa kuonwa ni watu wa maana

waziri husika kivuli wa upande wa upinzani alipaswa ajiuzulu kushinikiza hawa wengine wajiuzulu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom