Raisi kuidhinisha stahili ya Spika - ndio utaratibu ?

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,065
22,758
Kodi Tsh. 120,000,000.00
Samani Tsh. 200,000,000.00
Gari Tsh. 300,000,000.00
Sitting allowance ?
Matibabu ?
Salary ?
Marupurupu mengine ?
Mafao ?

Shellukindo ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Huduma za Bunge alisema Spika ana stahili zake kama Spika, hivyo kulipiwa kodi ya pango kwa dola 8,000 kwa mwezi na samani zake za ndani kugharimu zaidi ya sh mil 200 si jambo la ajabu. Ni kiongozi mwenye hadhi hiyo. Rais anajua, ndiye anayeidhinisha stahili zote za Spika. Hivyo hakuna jambo la ajabu hapo.

Raisi ndiye huidhinisha ? Nani anayepanga ?
 
... hivyo kulipiwa kodi ya pango kwa dola 8,000 kwa mwezi ... Raisi ndiye huidhinisha ? Nani anayepanga ?

Pango la shillingi billioni 10 kwa mwezi, hilo kathiri liko Dodoma, au Oysterbay, au Manhattan au Neverland?

Na mawaziri nao wanalipiwa renti? Na makatibu wakuu? Na ma meneja wa mashirika?

I guess the right question is, nani halipiwi renti Tanzania?
 
anastahili vyote hivyo kama kiongozi wa muhimili mmojawapo wa dola, wa kulaumiwa kwa gharama hizi za nyumba ni aliyeruhusu kuuzwa kwa nyumba za serikali.gazeti la tanzania daima linaendelea kutumiwa na wapinga ufisadi kulichafua bunge na waheshimiwa walio mstari wa mbele generally ni vita ya kilinda na spika sitta chini ya mwanvuli wa ufisadi.
 
Salam.
Dola 8,000 za kimarekani ni sawa na milioni kumi za kibongo na siyo bilioni kumi, naomba rekebisha. Mbona hiyo ni kodi ya kawaida? Hapo utaona umuhimi wa nyumba za serikali ambazo ziliuzwa.
 
anastahili vyote hivyo kama kiongozi wa muhimili mmojawapo wa dola, wa kulaumiwa kwa gharama hizi za nyumba ni aliyeruhusu kuuzwa kwa nyumba za serikali.gazeti la tanzania daima linaendelea kutumiwa na wapinga ufisadi kulichafua bunge na waheshimiwa walio mstari wa mbele generally ni vita ya kilinda na spika sitta chini ya mwanvuli wa ufisadi.
naomba ufafanuzi wa hiyo sentensi niliyowekea mstari..sijakuelewa una maanisha nini
 
Salam.
Dola 8,000 za kimarekani ni sawa na milioni kumi za kibongo na siyo bilioni kumi, naomba rekebisha. Mbona hiyo ni kodi ya kawaida?.

Masaiti are you serious kwamba kodi ya mil 10 kwa mwezi ni kawaida? Basi sisi wengine hatukai bongo na huenda tumepitwa na wakati pasipokujuwa. Kwa hesabu za haraka hiyo ni mil 600 kwa miaka mi5 sasa najiuliza hiyo pesa inaweza kujenga nyumba ngapi za level anayoishi huyo mweshimiwa? Gari mil 300-hivi anapewa pesa au gari linanunuliwa yeye analitumia likiwa mali yetu au? Na lile la ubunge je? Kwa uchache tunahitaji billions kuwa na spika ambaye anaongoza wawakilishi wa wananchi ambao mlo mmoja kwao ni muujiza na miongoni mwao wanawake 500 wanakufa kwa siku kwa matatizo wakati wa kujifungua simply bse hawana dispensary. Hii kama sio kufuru ni nini?
 
Najua ni kawaida ndani ya CCM kwa makada wake kukaa kimya baada ya kulambishwa peremende kila wanapothubutu kuikosoa serikali. Spika Sitta ninayemfahamu si ajabu baada ya hapa akawa kama aliyemwagiwa maji baridi. Unafiki na ulafi ni kama pete na kidole !
 
Kodi Tsh. 120,000,000.00
Samani Tsh. 200,000,000.00
Gari Tsh. 300,000,000.00
Sitting allowance ?
Matibabu ?
Salary ?
Marupurupu mengine ?
Mafao ?

Shellukindo ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Huduma za Bunge alisema Spika ana stahili zake kama Spika, hivyo kulipiwa kodi ya pango kwa dola 8,000 kwa mwezi na samani zake za ndani kugharimu zaidi ya sh mil 200 si jambo la ajabu. Ni kiongozi mwenye hadhi hiyo. Rais anajua, ndiye anayeidhinisha stahili zote za Spika. Hivyo hakuna jambo la ajabu hapo.

Raisi ndiye huidhinisha ? Nani anayepanga ?

Halafu muwashinde uchaguzi wakubali matokeo!, thubutuuu!. Lazima wajitangaze washindi, hivi ni nani anayependa mrija wake uchomolewe kwenye buyu la asali ya taifa?, tena mrija wenye diameter 20m. Kila kiongozi wa CCM ana mrija wake kwa nafasi yake, wapo wenye mirija ya kuanzia diameter ya 1mm mpaka 1km.
 
Katika hii safari haieleweki tunapelekwa wapi mimi sijui, ni MUNGU tu ndo anajua
 
Mimi nadhani issue kubwa hapo ni akina nani walio wazalendo zaidi. Mimi nadahania pia uongozi ni karama ila imefanywa kuwa ni biashara na hasa vile vigezo halisi vya uongoziu bora ni vipi vilipoanza kutipangilwa.
 
Back
Top Bottom