Raisi Kikwete nchi yako ya Tanzania inabakwa iokoe

nitonye

JF-Expert Member
Dec 18, 2011
7,273
3,750
Mheshimiwa sikia kelele za kuomba msaada kutoka kwa nchi yako unayoiongoza maana ni kama kelele azitoazo mwanamke anapokuwa anabakwa.
Mheshimiwa nchi yako imekuwa kama pango la wanyang'anyi kila mtu anaiba anavyotaka bila kuwepo na ulinzi wowote.
Mheshimiwa umeshindwa kumsaidia mwanamke huyu Tanzania na kupanda kwa gharama ya maisha lakini kipato kinazidi kushuka.
Mheshimiwa umeshindwa kumletea maisha bora huyu Tanzania na hivyo kuacha akibakwa kila siku na wageni
Mheshimiwa mafisadi wanaongezeka kila uchao na wewe umenyamaza.
Mheshimiwa sio kila kitu unatabasamu mda mwingine unakunja sura unatoa maamuzi
Mheshimiwa msaidie huyu mwanamke asiendelee kubakwa maana maumivu ya kubakwa hayasauliki
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Sekeseke la mama na baba mwenye nyumba kuwachungulia limekwisha mkuu?
 
ukiona manyoya ujue kachinjwa, mkuu kashatupiwa virago ndo maana kaongeza kilio..nitonye JK ni sikio la kufa,tushamuonya sana kaweka pamba,labda sauti za ndege zimeziba masikio
 
Anaebaka hawezi jua maumivu ya wanaobakwa....So ni maumivu kwa kwenda mbele imagine mishahara kwa wafanyakazi inasua na bado ni kiduchu lakini gharama za maisha zinapaa yani sipati picha 2015 ni mbali...madaktari wanataka kugoma serikali baada ya kukaa chini na kusilkilza kilio chao wanawatisha bila kujua tupo kwenye nyakati zipi....ipo siku wataikimbia nchi yao
 
Back
Top Bottom