Maono ya viongozi yanavyoipaisha Tanzania kimaendeleo

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
“ Kwa wale ambao wana mashaka mwanamke huyu ataweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nataka niwaambie aliyesimama hapa ni Rais, nataka nirudie kwamba aliyesimama hapa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye maumbile yake ni mwanamke”

Kauli thabiti ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kauli hiyo Tanzania imeshuhudia mabadiliko makubwa na maendeleo makubwa katika kipindi kifupi, kutokana na nia thabiti ya Rais na wasaidizi wake katika kuwatumikia Watanzania.

Mwana mama Shupavu, mpambanaji na mchapakazi ndie shujaa anayeendelea kuivusha Tanzania katika kipindi kingine na kuiweka nchi yetu katika misingi ya kiutendaji, amani na utulivu. Sasa Tanzania inasonga kwa kasi, huku sekta mbalimbali zikiendelea kuimarika, kuanzia Afya, Elimu, miundombinu pamoja na nishati.

Ni katika kipindi hiki Watanzania tumeshuhudia Ujenzi wa madarasa nchi nzima, Vituo vya afya kedekede vikijengwa kila kona ya nchi hii huku uboreshaji wa sekta mbalimbali ukiendelea.

Kwa kauli rahisi tunayoitumia sisi huku Mtaani tunasema “Mama anaupiga mwingi.” Tukianzia na Fedha za UVIKO 19, ambazo zimeingia moja kwa moja katika kutekeleza miradi mingi ya kijamii kama ujenzi wa madarasa ili kuondoa uhaba wa madarasa ambao umekuwa ukiikabili Nchi yetu kwa muda mrefu, Majengo ya hospitali na vifaa tiba, kila kona ya Nchi pamoja na maboresho ya huduma nyingine kama miundombinu.

Kama hii haitoshi angalia namna taswira ya nchi yetu ilivyoshamiri kimataifa, Mwanamama huyu shupavu kwelikweli ameiinua Tanzania na kuiweka kileleni kwenye anga za kimataifa, hili halina ubishi kila utakapogusa kimataifa neno kuu ni Tanzania, hapa sasa ndo unaikumbuka ile kauli ya Timu ya mpira wa miguu kwa “We are unstoppable”

Mchaka mchaka huu wa mafaniko yote haya ya Rais Samia, yanatokana na namna bora alivyoweza kuboresha utendaji na Ushirika miongoni mwake yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdory Mpango, pamoja na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Viongozi hawa waliopikwa wakapikika katika Nyanja mbalimbali za uongozi, wameendelea kudhihirisha kwa umoja wao namna walivyodhamiria na kujitoa kuhangaika usiku na mchana kuwaletea Watanzania maendeleo.

Kwa maelekezo na uongozi thabiti wa Rais Samia, Serikali yake imeweza kuonesha muunganiko mzuri wa kiuongozi na ushirikiano miongoni mwao, viongozi hawa wa kitaifa pamoja na Mawaziri kila mmoja anapambana kutimiza majukumu yake kwa muunganiko mkubwa.

Rais Samia ameendelea kuwa kiongozi anaetoa miongozo na maelekezo kwa viongozi wa chini na kutoa muelekeo wa namna bora ya kuwaongoza na kuwasimamia watanzania pamoja na kutoa miongozo kwa viongozi wengine wa Kitaifa.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,,,” Kazi iendelee” salamu yake yenye ujumbe madhubuti inayoiunganisha Tanzania na Watanzania katika mbio za maendeleo na mafanikio.

Makamu wa Rais Dokta Philip Mpango, Moja ya viongozi wakimya na wapole Silaha anayoitumia Rais Samia katika kuhakikisha Uchumi wa Nchi unakuwa na usimamizi wa karibu kwa viongozi, ndio amekuwa mshauri wa karibu wa Rais katika masuala kadhaa ambayo yameiwezesha Tanzania kuendelea kupaa na kuimarika kiuchumi.

Mheshimiwa Dokta Mpango, amekuwa kiongozi wa kimkakati katika kufuatilia maelekezo na malengo ya Rais na kumsaidia kwa karibu kusimamia utendaji wa viongozi wengine.

Silaha hii imekuwa ikitumika pia katika mikutano mikubwa ya kimkakati huko duniani, huyu amekuwa akihudhuria mikutano mikubwa kabisa ambayo anaitumia kuieleza dunia malengo na dhamira ya nchi yetu kukua kiuchumi.

Dkt. Mpango siku zote amedhihirisha kwamba yeye ni jembe hasa la Rais Samia Suluhu Hassan na msaidizi namba moja, utulivu wake kwenye mikutano hii inaifanya Tanzania kuangaliwa kwa jicho la pekee na kuwavuta zaidi wawekezaji na kuzivuta taasisi za kimataifa kuweka pesa zako kusaidia kusukuma baadhi ya ajenda za kimaendeleo nchini.

Mheshimiwa, Kassim Majaliwa Majaliwa huyu ni Mtendaji Mkuu wa Serikali, ni silaha nyingine ya utendaji ya Rais Samia katika kutekeleza mipango na mikakati ya Serikali, akiwa kama kiongozi wa Shughuli za Serikali amekuwa mtekelezaji mkuu wa maagizo yote ya Rais na mfuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo hayo ambaye amekuwa akikimbia huku na kule kukagua miradi na kutekeleza maagizo yote ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mafanikio ya usimamizi wa miradi ya yote ya UVIKO 19, yeye kama mwenyekiti wa kamati ya kitaifa iliyosimamia utekelezaji wa mradi huu wenye mafanikio.

Mheshimiwa Majaliwa hajakaukiwa na neno Mama Samia mdomoni mwake amekuwa akimuimba na kuisemea Serikali katika kila sehemu aliyopo, hakika ameisemea na kuitangaza Tanzania.

Amehubiri mafanikio ya awamu ya sita katika sehemu mbalimbali, Unyenyekevu na utii wake kwa viongozi wa juu umemuwezesha kuaminiwa na viongozi wake na kupewa nafasi ya kutekeleza majukumu yake kwa weledi mkubwa na kumsaidia Rais Samia kuendeleza Serikali yake kwa Amani na mafanikio makubwa.

Viongozi hawa wamejuana vyema na wamepikwa chungu kimoja na wamepikika hii labda inatokana na wao kufanya kazi kwa pamoja kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na kupikwa na utendaji na namna walivyojitoa kwa moyo wa dhati katika kuisaidia jamii ya Watanzania kupata maendeleo.

Huyu naye kama alivyo Dkt. Mpango amekuwa akiitumia vizuri sana mikutano ya kimataifa na ziara za nje ya nchi kueleza fursa zilizopo nchini pamoja na kushawishi wawekezaji, baadhi za ziara zake tumeona zikileta neema nchini kwenye sekta mbalimbali.

Pamoja na hao, ipo timu imara ya Mawaziri hawa sasa ndio washambuliaji wakuu wa Serikali, mafanikio unayoyaona huko kwenye sekta yanatokana na kazi kubwa inayofanywa na timu hizi kubwa, Rais Samia amefanikiwa kuwa ma Timu kubwa na mahiri ya vijana wabunifu wanaohangaika huku na kule kuhakikisha maagizo na maelekezo ya viongozi hawa watatu yanatekelezwa ipasavyo.

Wito wangu kwa Watanzania tuendelee kuwaombea viongozi wetu waendelee kuchapa kazi bila kuzingatia kelele za watu wasioitakia mema Nchi yetu, Muunganiko wao umeikimbiza Tanzania kimaendeleo na kufungua milango ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Samia ameichukua Nchi katika wakati mgumu sana mabadiliko ya hali ya Hewa, Uchumi wa Dunia umedorora Covid19 Mzigo wa Madeni ya mtangulizi wake Vita ya Ukrain nk.nk.

Wasaga Kuguni wengi na Viroboto wao walijua atashindwa tena walikuwa wakisema "Demu ataweza wapi?"

Lakini kwa mshangao wa wengi Mama kathibitisha kuwa wako wrong.

Sasa hivi tunalala bila khofu ya kuuliwa kwa risasi au kuchomwa sindano za sumu Biashara zimeanza kushamiri na kustawi tena.

Nchi imetulia Vijiweni watu wanaongea kwa uwazi bila kuogopa kutekwa na kutiwa kwenye viroba.

Hakika Samia amewathibitishia Wanaume suruwali kuwa kazi ya Uraisi jinsia yoyote inaweza.
 
Back
Top Bottom